Mafanikio ya Afrika katika kupambana na polio

Boy being vaccinated against polio

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Polio inaweza tu kuzuiwa kupitia chanjo

Afrika imetangazwa kuumaliza ugonjwa wa polio na Tume ya Ukanda wa Afrika ya kupambana na Polio.

Polio huathiri watoto wa chini ya umri wa miaka mitano, wakati mwingine husababisha kupooza.

Kifo kinaweza kutokea iwapo kupooza huko kutaathiri misuli inayosaidia mfumo wa upumuaji.

Hakuna tiba lakini chanjo dhidi ya ugonjwa huo kuwalinda maisha yao yote.

Ugonjwa huo sasa uko Afghanistan na Pakistan pekee.

Hakuna tiba lakini chanjo ya polio ni kinga ya maisha ya watoto.

Nigeria ni nchi ya mwisho kutangazwa kuutokomeza ugonjwa huo mbaya, ikiwa na wagonjwa zaidi ya nusu ya wagonjwa wote wa polio duniani chini ya miaka kumi iliyopita.

Wild polio cases in Nigeria. 2000-2020. Cases of wild polio in Nigeria .

Polio ni nini na je sasa hivi imetokomezwa barani Afrika?

Polio ni kirusi ambacho husambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia maji yaliyochafuka. Kirusi hicho kinaweza kusababisha kupooza kwa kushambulia mfumo wa fahamu.

Aina mbili kati ya tatu ya virusi vya polio vimeondolewa duniani. Siku ya Jumanne, Afrika itatangazwa rasmi kuwa imeweza kukabili virusi vya polio.

Zaidi ya asilimia 95 ya watu wote barani Afrika wamepatiwa kinga ya ugonjwa. Hii ilikuwa moja ya masharti yaliyowekwa na kamisheni kabla ya kulitangaza bara kudhibiti polio.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chanjo ya polio ilibuniwa 1952

Shirika la Afya duniani (WHO) limebainisha kuwepo kwa wagonjwa nchini Nigeria, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamuhuri ya Afrika ya Kati na Angola.

Afrika imetokomeza vipi Polio?

Bila dawa, chanjo ilitengenezwa mwaka 1952 na Dkt Jonas Salk ilitoa matumaini kuwa watoto wanaweza kulindwa dhidi ya ugonjwa huo.

Mwaka 1961 polio iliwaathiri watoto zaidi ya 75,000 barani Afrika - kila nchi iliathirika.

Mwaka huo hayati Nelson Mandela alianzisha programu ya ''Ondoa Polio Afrika'', akiwahamasisha wafanyakazi wa afya ambao walikwenda vijijini kutoa chanjo.

Tangu mwaka 1996 chanjo za matone bilioni tisa zimetolewa. 'Virusi vya corona, 'dharura ya kiafya kubwa zaidi' kuwahi kutokea duniani

Kumekuwa na changamoto zipi?

Jamii zilizokuwa hatarini kuathiriwa na polio zinaishi katika baadhi ya maeneo yaliyo magumu kufikiwa na kampeni ya chanjo.

Nigeria ni nchi ya mwisho Afrika kuripoti polio - katika jimbo la Borno Kaskazini maeneo ya mbali ya kaskazini mwamashariki na kitovu cha wanamgambo ya Boko Haram yalivamia mwaka 2016.

Mbali na Nigeria, sehemu ya mwisho kushuhudia wagonjwa wa polio ilikuwa Puntland Somalia mwaka 2014.

Mzozo na wanamgambo wa Boko Haram umefanya kuwa vigumu kwa sehemu kadhaa za Nigeria kufikiwa, hasa katika jimbo Borno.

Map: Nigeria's north-eastern Borno state

Zaidi ya watu milioni mbili wamekimbia kutokana na mapigano.

Wafanyakazi wa mstari wa mbele, asilimia 95 miongoni mwao wanawake, waliweza kusafiri kuelekea kwenye maeneo yenye mizozo kama vile kupitia Ziwa Chad kwa boti na kuwapatia chanjo jamii ziishizo maeneo ya mbali.

Tetesi zilizosambaa na taarifa za kupotosha kuhusu chanjo zimeonesha kurudisha nyuma jitihada za chanjo.

Mwaka 2003 Kano na maeneo mengine kadhaa ya majimbo ya kaskazini yalisitisha chanjo baada ya kuwepo ripoti za viongozi wa dini ya kiislamu kuwa chanjo ilikuwa na dawa ya kufunga kizazi kama sehemu ya mpango wa Marekani kuwafanya wanawake wa kiislamu wasizae.

Vipomo vya maabara vilivyofanywa na wanasayansi wa Nigeria vilitupilia mbali shutuma hizo.

Kampeni za chanjo zilianza mwaka uliofuata lakini tetesi dhidi ya chanjo ziliendelea.

Mwaka 2013 watoa chanjo wanawake tisa waliuawa baada ya kufyatuliwa risasi na watu waliodhaniwa kuwa Boko Haram katika vituo vya afya katika jimbo la Kano.

Imechukua miongo kadhaa kufanikiwa kuondokana na taarifa za kupotosha kuhusu chanjo.

Je ugonjwa wa polio unaweza kurejea?

Maelezo ya picha,

Misbahu Lawan Didi amejitahidi kushawishi wazazi waruhusu watoto wao kupata chanjo

Polio inaweza kuingia kwenye nchi isiyo na ugonjwa huo na kusambaa haraka sana na kuathiri watu ambao hawana kinga.

Hii ilitokea Angola, ambayo pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe, waliweza kudhibiti ugonjwa mwaka 2001.

Nchi hiyo iliendelea katika hali hiyo kwa miaka minne mpaka mwaka 2005 ambapo kuliibuka ugonjwa huo tena ikiaminika kuwa maambukizi yalitoka nje ya nchi.

WHO imesema kuwa ni muhimu kwa nchi kubaki katika hali ya tahadhari mpaka pale ulimwengu utakapokuwa umeutokomeza ugonjwa huo kabisa.