Tecno W2: Maelfu ya simu za China zilizo na programu za kulaghai zauzwa Afrika

Maelfu ya simu hizo yalipatikana kuwa na programu hiyo ya kulaghai watu

Chanzo cha picha, TECHNO

Maelezo ya picha,

Maelfu ya simu hizo yalipatikana kuwa na programu hiyo ya kulaghai watu

Programu ambayo inawasajili kisiri watumiaji wa simu katika huduma zinazotoza ada imepatikana katika maelfu ya simu zinazouzwa Afrika.

Kampuni ya Upstream ambayo hukabiliana na ulaghai wa kiteknolojia imepata nambari maalum 53,000 katika simu za Tecno, zilizouzwa Ethiopia, Cameroon, Misri, Ghana na Afrika Kusini.

Waundaji wa simu hiyo Transsion wameuambia mtandao wa Buzzefeed kwamba waliweka nambari hiyo bila kujua.

Upstream imesema imekuwa ikiwatumia vibaya wateja wao "wasiojua".

Programu ya Triada ilipatikana katika simu za Android za kampuni hiyo ikiwa imewekwa nembo maalum inayofahamika kama xHelper ambayo hutumiwa kumsajili kisiri mwenye simu katika huduma zinazotoza ada, bila idhini ya mwenyewe.

Ombi hilo likikubaIiwa, inaanza kutumia salio kwenye simu ya mteja husika, kama njia pekee ya kulipia huduma za kidijitali katika nchi zinazoendelea.

Kwa jumla, Upstream ilipata kile ilitaja kuwa "shughuli za kutatanisha" kwenye zaidi ya simu za smartphone za Tecno zaidi ya 200,000.

Kwa mujibu wa utafiti IDC, Transsion Holdings ni moja ya kamapuni inayoongoza kwa uundaji wa simu za China na inaoongoza kwa uuzaji wa simu barani Afrika.

Ikijibu madai hayo Tecno imesema suala hilo lilikua "la zamani na lilikuwa linahusiana na usalama wa simu za kimataifa" na ilishughulikia Machi 2018.

"Wateja wa sasa wa W2 huenda wanakabiliwa na suala la Triada, na wanashauriwa kupakua programu itakayotatua tatizo hilo ama wawasiliane na wahudumu wa Tecno walioidhinishwa kupata msaada," kampuni hiyo ilisema katika taarifa yake kwa BBC.

Iliongeza kuwa Inatilia "maanani' usalama wa data za wateja wake ".

"Kila programu inayoweekwa kwenye simu inapitia hatua kadhaa za usalama," iliongeza kasema.

Tatizo la kawaida

Mwanzo wa mwaka huu, kampuni ya teknolojia Malwarebytes ilionya kuhusu programu za siri kama hizo zilizowekwa kwenye simu za Android kutoka China - UMX U686CL. Simu hizo ziliuziwa watu wa kipato cha chini Marekani kupitia mpango wa serikali.

Na mwaka 2016, mtafiti Ryan Johnson aligundua kuwa simu aina za smartphone zaidi ya milioni 700 zilikuwa zimewekwa programu za siri.

Google, ambayo iliunda mfumo wa teknolojia wa Android, inafahamu kuhusu suala hilo.

Maelezo ya video,

Simu ilivyomsaidia daktari wakati huu wa janga la corona

Katika taarifa iliyochapishwa katika blogu yake mwaka jana ililaumu madalali wa uuzaji wanaotumia, na makampuni ya uundaji simu wanaoweka programu inayomwezesha mwenye simu kuifungua kwa kutumia uso wake, kwa kuweka programu ya siri ya Triada.

Imesema iliwahi kufanya kazi na waundaji simu hizo kuondoa programu hizo hatari kwenye simu.