Bakteria wa mdomo wanaohusishwa na kuwashwa kwenye uke

BV bacteria covering cells

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bakteria wanaosababisha ugonjwa wa kuwashwa kwenye uke waliozunguka seli

Tendo la ndoa kwa kutumia kinywa kunaweza kusababisha mazingira ya maambukizi ukeni, kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye jarida la bailojia la PLoS

Kuwashwa kwenye uke sio ugonjwa unaotokana na ngono. Badala yake, unatokana na ukosefu wa msawazo wa homoni kwenye uke.

Wanawake wenye ugonjwa huo huenda wasioneshe dalili lakini wengine hutoa harufu mbaya.

Utafiti ulibaini nini?

Wanawake wasio na ugonjwa huo huwa wana bakteria wazuri waitwao lactobacilli kwa Kiingereza ambazo zinafanya uke kuwa na kemikali nyingi na kiwango cha pH cha chini.

Kinachosababisha hicho kutokea hakifahamiki vyema lakini kuna uwezekano mkubwa ukapata tatizo hilo iwapo:

  • Unafanya mapenzi lakini wanawake ambao hawashiriki mapenzi pia wanaweza kupata tatizo hilo
  • Umebadilisha mwenza wako
  • Unatumia njia ya kupanga ya uzazi kwa kutumia kitanzi
  • Unatumia bidhaa za marashi karibu na uke

Utafiti uliofanywa pia unaonesha vile aina fulani ya bakteria inayopatikana kwenye mdomo inahusishwa na magonjwa ya kwenye ufizi na utando wa meno yako unavyoweza kuchangia kupata ugonjwa huu

Walifanya majaribio kwa mwanadamu na panya kuangalia mwenendo wa bakteria.

Bakteria wa mdomo, Fusobacterium nucleatum, walionekana kusaidia ukuaji wa bakteria wengine kwenye tatizo la kuwashwa kwenye uke. Watafiti, Dkt Amanda Lewis kutoka chuo cha California na wafanyakazi wengine, wanasema kuwa utafiti huo unaonesha vile matumizi ya mdomo kwenye tendo la ndoa yanavyoweza kuchangia ugonjwa wa kuwashwa kwenye uke.

Wataalamu tayari wanajua kwamba ugonjwa huo unaweza kuchangiwa na tendo la ndoa ikiwemo kati ya wanawake.

Profesa Claudia Estcourt, msemaji wa Chama cha Maswala ya afya ya uzazi na HIV, amesema utafiti kama huo ni muhimu katika kuelewa tatizo hilo.

"Tunajua kwamba tatizo hilo haliko wazi."

Alisema kuwa matumizi ya mdomo kwenye tendo la ndoa kunaweza kusambaza magongwa ya maambukizi na bakteria ambako huenda ama kukawa na mchango mkubwa katika hali nyingine za afya.

Ugonjwa wa kuwashwa kwenye uke

Kawaida huo unaonekana kuwa wa kawaida, lakini unastahili kutibiwa kwasababu huwa unafanya wanawake kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya maambukizi ya mkojo.

Ikiwa mwanamke ni mjamzito, kunaongeza hatari ya kupata mtoto njiti.

Unawezaje kujua umepata maambukizi?

Ni kawaida sana na huenda ikawa tayari wanawake walio na tatizo wameshahafahamu kwamba wanatokwa na majimaji yasio ya kawaida yanayonuka vibaya.

Pia unaweza kutambua mabadiliko ya rangi na jinsi maji maji yanavyoendelea kutoka kwenye uke kama vile kuwa ya rangi ya kijivu na weupe miembamba na maji maji.

Unaweza kufanyiwa vipimo katika kliniki kwa kutumia uchafu unaotoka

Ikiwa utathibitishwa kupata maambukizi unaweza kutibiwa kwa matibabu ya vidonge ya dawa ya kujipaka.