Messi atelekea wapi akifanikiwa kuondoka Barcelona?

Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Je Lionel Messi amecheza mechi ya mwisho ya Barcelona?

Mchezaji nyota wa Barcelona mshambuliaji Lionel Messi ametaka kukiacha kilabu hicho.

Muajentina huyo, 33, alituma ujumbe wa Fax kwa klabu siku ya Jumanne akisema anatamani kuondoka kwa uhuru mara moja.

Barca ilitandikwa 8-2 na Bayern Munich katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa tarehe 16 mwezi Agosti.

Mshindi mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or alianza kuichezea Barca mwaka 2004 na kushinda ligi ya mabingwa mara nne akiichezea timu hiyo.

Barcelona inaamini kifungu cha mkataba cha kumruhusu kuondoka kimekwisha na mkataba wake unakwisha mwaka 2021 na kifungu cha kumuuza cha pauni milioni 700.

Bodi ya klabu hiyo itakaa hivi karibuni na wengine wanaona kuwa jambo pekee ambalo linaweza kubadili nia ya Messi ni kujiuzulu kwa rais Josep Maria Bartomeu, na uchaguzi ufanyike mapema. Lakini Messi anaonekana kuwa amedhamiria kuondoka kilabuni hapo bila kujali chochote.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Xavi, kocha wa Al Sadd ya Qatari alicheza na Messi kwa miaka 11 wakiwa Barcelona

Baada ya taarifa hiyo, mashabiki wa Barca walikusanyike nje ya Nou Camp dhidi ya bodi na wakionesha kumuunga mkono mchezaji huyo aliyeweka rekodi nzuri ya ufungaji.

Mapambano ya kisheria sasa yatakuwa kati ya klabu na mchezaji. Messi alikuwa na kifungu cha mkataba wake kinachomruhusu kuondoka kwa uhuru, ikiwa ataijulisha klabu shauku yake kabla ya tarehe 10 mwezi Juni.

Tarehe hiyo imepita sasa Barca inaamini kuwa kifungu hicho kimekwisha muda wake, lakini Messi na timu inaamini kuwa kifungu hicho kinaweza kuongezewa muda mpaka mwezi Agosti kwa sababu ya kipindi cha janga la virusi vya corona.

Mchezaji mwenzake wa zamani Carles Puyol ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter akimuunga mkono kwa hatua aliyoichukua.

Barcelona wamesema kuwa kifungu hicho kilikwisha tangu tarehe 10 mwezi Juni na kuwa wanashawishika, kuwa watashinda mgogoro huo wa kisheria , kuhusu suala hilo.

Lakini wanasheria wameiambia klabu kuwa Messi hatashinda mgogoro huo.

Ujumbe wa Fax ni jambo ambalo limefikiriwa vyema, kwa kuwa amezungumza na familia na wanasheria, ana shaukukubwa kuondoka kwenye klabu hiyo.

Kwa Messi haya si mapambano ya mamlaka. Anachotaka ni kuondoka tu basi.

Nguvu ya Messi ndani ya klabu

Watu wanasema kuwa ana mamlaka makuja kwenye klabu. Huongea moja kwa moja ikiwa atatakiwa kufanya hivyo kama ilivyo kwa wachezaji wengine nguli kwenye vilabu vikubwa.

Lakini tutazame hili lina ukweli namna gani kwa kuangalia maoni yake hivi karibuni kuhusu:

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

'Nimchezaji mzuri ambaye sijawahi kumuonea mwenzake' - kocha Pep Guardiola alikuwa na Messi akiwa Barcelona

Kurejea kwa Neymar, ambako hakukufanyika: kuendelea kwa kocha Ernesto Valverde, ambako hakukufanyika; hakuna haja ya kumsajili Antoine Griezmann, ambako hakukufanyika, hivyo sina uhakika kama ana mamlaka makubwa.

Ni hali ya kuwa hivi sasa Messi hafurahii kuichezea Barca tena, timu ambayo kwa sasa inahitaji kufanya kazi kubwa kushinda mataji makubwa tena.

Anataka kuona Barcelona itafanya nini, lakini huenda pia hatahudhuria mazoezi.

Hatafanya vipimo pengine kabla ya msimu. Ikiwa itakuwa hivyo, klabu hiyo itatuma ujumbe wa Fax kwa Messi kuhusu kutoheshimu mkataba wake na mgogoro wa kisheria ndipo utakapoanzia- na huo utawafikisha katika mahakama ya kimichezo hatimaye.

Leo Messi anataka kuondoka sasa hivi bila kujali chochote. Lakini je ataweza? Ukizingatia mkataba wake ulipaswa kuwa kifungu kilipaswa kufanyiwa kazi tarehe 10 mwezi Juni, Klabu inaamini kuwa iko kwenye njia sahihi.

Lakini wanataka kuendelea kubaki na mchezaji ambaye hataki kubaki kilabuni ? Vilabu kama Paris-St Germain na Manchester City zilisisitiza hazijachukua hatua yoyote kuhusu kumnasa Messi. Lakini ni wazi hakuna ajuaye athari za kifedha za hatua hiyo.

Vilabu vingine vikubwa vilichukua hata mara nyingi huko nyuma kujaribu kumshawishi Messi kujiunga na timu hizo-Inter Milan na Chelsea.

Shinikizo pekee dhidi ya bodi linatoka kwenye mitandao ya kijamii- kama nguvu hiyo inamlazimu Bartomeu kujiuzulu tungeweza kushuhudia hatua tofauti. Tunachohisi ni kuwa klabu pengine itamtaka aendelee kubaki lakini anaweza akalazimika kujadili kuhusu ada kubwa ya uhamisho.

Hivyo tutaona kama Barcelona kweli wataamua kuomba kiasi hicho kikubwa zaidi cha fedha au nani yuko tayari kulipa ada ya uhamisho. Ingawa amesaliwa na mwaka mmoja tu wa mkataba wake, mzozo huu utaendelea kwa muda.