Virusi vya corona: Amri ya kukaa nyumbani inawalazimisha waalimu kuchuuza mitaani

Virusi vya corona: Amri ya kukaa nyumbani inawalazimisha waalimu kuchuuza mitaani

Wakati Uganda ilipotangaza amri ya kukaa nyumbani na kufunga shule, waalimu wengi wa shule za binafsi hawakuwa wanalipwa tena mishahara yao. Wengi walilazimika kutafuta ajira mbadala, kama vile kuuza bidhaa mitaani (umachinga). Hata hivyo kazi hiyo haikosi changamoto.