Jinsi mpango wa waasi wa Sudan unavyotoa njia ya kuokoa amani

L-R: Gibril Ibrahim Mohammed, leader of Sudan's Justice and Equality Movement (Jem) and Minni Minnawi of Sudan Liberation Movement/Army (SLM/A) gesture after the signing of the peace agreement - 31 August 2020

Chanzo cha picha, Reuters

Makubaliano ya amani ya Sudani hatimaye yalitiwa saini juma lililopita yaliyoahidi kumaliza vita vibaya mjini Darfur , Kordofan Kusini na Blue Nile ambavyo vimegharimu maisha ya mamia kwa maelfu ya watu, lakini wakati Alex de Waal na Edward Thomas wanaeleza hatua hii imekuja na malipo makubwa.

Makubaliano haya yalifanyika kati ya serikali ya mpito na wa viongozi wa muungano wa waasi mjini Juba nchini Sudani Kusini.

Nguvu yake itategemea nia njema ya pande zote mbili.

Udhaifu wake ni kwamba Sudan inajaribu kuitekeleza demokrasia katikati ya msukosuko wa mizozo bila msaada wowote wa kimataifa.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Vijana wengi wa Darfur wamekulia katika kambi

Mnamo Agosti 2019, viongozi wa jeshi na raia wa Sudan walikubaliana kushiriki pamoja katika serikali ya mpito, kutimiza mayakwa ya waandamanaji ambao walipindua utawala wa miaka 30 wa Rais Omar al-Bashir.

Kipaumbele cha juu ilikuwa ni kumaliza vita ambavyo vimekumba nchi hiyo kwa muda mrefu.

Waasi walikuwa wanaamini kuwa wale walio kwenye baraza la raia lililoongozwa na Waziri Mkuu, Abdalla Hamdok ni wakweli.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagolo, ajulikanaye kwa jina ''Hemeti''

Hawakuwaamini majenerali, hasa Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagolo, ajulikanaye kwa jina ''Hemeti'' ambaye wanajeshi wake walifanya kampeni za kutisha za kupambana na waasi.

Makubaliano yamefikiwa baada ya karibu mwaka mmoja wa mazungumzo ya amani.

Nafasi iliyo nadra

Mwenyekiti wa baraza la kijeshi la serikali ya mpito, Luteni jenerali Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake, Hemeti, wanahitaji kupata uhalali wa jumuiya ya kimataifa ambao kutoka kwenye makubaliano hayo.

Kundi kikubwa zaidi, Chama cha Sudan Revolutionary, ni muungano dhaifu. Na ingawa inashiriki malengo mengi sawa na waandamanaji wasio na vurugu wa Khartoum, wanatoka asili tofauti sana.

Waandamanaji wa mijini walivumilia miongo kadhaa ya ukandamizaji wa polisi.

Viongozi wao wamechukuliwa kutoka kwa wasomi wa kitaalam na wanatarajiwa kurithi serikali, kama ilivyotokea kwa ''ghasia za Khartoum'' zilizopita mnamo 1964 na 1985.

Waasi walipigana vita vya umwagaji damu katika vumbi na matope

Walitengwa na serikali zilizopita na hawana uzoefu wa siasa za kiraia

Hivyo, ilichukua muda kwa waasi kuliamini tabaka la wanasiasa wa mjini- ingawa mapinduzi ya mwaka 2019 yalitoa nafasi adimu ya kuibadili Sudan.

Mgawanyo wa madaraka

Makubaliano ya amani yanawaleta waasi katika serikali ya mpito.

Wamepatiwa mamia ya nafasi za ubunge na nafasi za juu za uongozi, ambazo watazishikilia mpaka uchaguzi utakapofanyika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Maelfu ya wapiganaji waasi watajumuishwa kwenye jeshi.

Mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita watasaidiwa kurejea nyumbani.

Mfumo wa shirikisho uliowekwa upya utatoa nguvu zaidi kwa tawala za mitaa.

Lazima kuwe na marekebisho ya sheria ya ardhi na mahakama ili kuleta watuhumiwa wa uhalifu wa kivita mbele ya sheria.

Matakwa haya ya amani sio mpya.

Mikataba na miongozi kama hiyo ilisambaratika katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Wakati huu ni tofauti: Ni makubaliano ya Wasudani, yaliyojadiliwa na Wasudani bila mashinikizo ya muda kutoka nje .

Pande zote mbili zinajua kuwa zinapaswa kufanyia kazi makubaliano hayo au mchakato mzima uanguke.

'Wapingaji wakubwa'

Kuna makundi mawili ya waasi, lakini kua uwezekano kuwa hatimaye watakubali.

Kiongozi mmoja ambaye hajatia saini ni Abdel Aziz al-Hilu wa chama cha Sudan People's Liberation Movement-North cha milima ya Nuba Kordofan Kusini.

Ana misimamo yake na mkaidi na madai yake - ujamaa na haki ya Nuba ya kujitawala - haruhusu majadiliano mengi.

Lakini Waziri Mkuu Hamdok anaheshimu msimamo wa Bwana Hilu na wameapa kuendelea na mazungumzo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Abdel Wahid al-Nur, kiongozi wa chama cha Sudan Liberation Movement (SLM), bado hajasaini makubaliano hayo

Mwingine ni Abdel Wahid-al Nur wa chama cha Sudan Liberation Movement (SLM) huko Darfur.

Ni mpinzani mkubwa.

Lakini makubaliano haya yanakidhi madai yake, na ikiwa yatatekelezwa, msimamo wake hautadumu kwa muda mrefu.

Kikwazo cha ugaidi

Lakini hapa ndio hatari ilipo haswa.

Sudan iko katika mtikisiko wa uchumi, uliosababishwa na usimamizi mbaya wa serikali ya Bashir na kuzidishwa na janga la Covid-19 na sasa na mafuriko.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo, alipokutana na waziri mkuu Abdalla Hamdok mwezi uliopita

Kuna jambo muhimu linalohitajika kwa ajili ya kuunasua uchumi.

Marekani iliitaja Sudan kuwa '' mfadhili wa ugaidi'' mwaka 1993 - na mpaka itakapofuta msimamo huo, vikwazo vya kiuchumi vitabaki

Sudan iliacha kuunga mkono "magaidi" miaka 20 iliyopita lakini Washington DC inataka malipo, na wakati Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alipotembelea Khartoum mwezi uliopita, juu ya ajenda yake ilikuwa ikishinikiza Sudan iitambue Israel.

Chanzo cha picha, AFP

Bwana Hamdok alijibu kuwa serikali itakayochaguliwa ndio pekee itakayokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.

Makubaliano ya amani yamekuja na gharama.

Mkataba unaahidi kuwepo kwa mfuko wa maendeleo wa kuyajenga maeneo ya vijijini na kusaidia watu kurejea majumbani mwao.

Umeahidi kutanua huduma za afya na shule pia vyuo vikuu.

Kuwahusisha waasi katika jeshi la kitaifa kutagharimu fedha.

Na hiyo yote ni pamoja na pesa za dharura zinazohitajika kuuinua uchumi na kuzuia mgogoro wa kibinadamu ijayo.

Mpaka Washington itakapotambua rasmi kuwa Sudan si ''mfadhili wa ugaidi'', hakutakuwa na nafuu ya madeni wala uwekezaji wan chi za kigeni.

Hali hii inaiacha Sudan katika hali mbaya kiuchumi katika mikono ya Saudi Arabia na Umoja wa falme za kiarabu, ambazo hutoa pesa kwa maswahiba wake wenye nguvu ndani ya jeshi kama Jenerali Burhan na Hemeti.

Wasudani wamemuangusha dikteta na kutia saini mkataba wa amani, wao wenyewe na bila msaada wa kimataifa.

Wanahisi kuwa ulimwengu wote unachoweza kufanya ni kuwapa nafasi.

Edward Thomas ni mhadhiri Taasisi ya Rift Valley nchini Kenya na Alex de Waal ni mkurugenzi mtendaji wa Mfuko wa amani Duniani katika Shule ya Sheria na Diplomasia ya Fletcher katika Chuo Kikuu cha Tufts nchini Marekani.