Wanyama pori wanaangamia kwa kasi kutokana na uharibifu unaofanywa na binadamu, wameonya wanasayansi

Wanyamapori wanakabilkia na tishio la ukosefu wa makaazi ikiwemo ukataji wa miti

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanyamapori wanakabilkia na tishio la ukosefu wa makaazi ikiwemo ukataji wa miti

Idadi ya wanyama pori imepungua kwa zaidi ya thuluthi mbili katika kipindi kisichopungua miaka 50 , kujlingana na ripoti muhimu ya kundi la uhifadhi wa wanyama pori WWF.

Ripoti hiyo inasema kwamba kushuka kwa idadi hiyo hakuoneshi ishara za kupungua.

Na imeonya kwamba asili inaharibiwa na wanadamu kiwango ambacho a hakijawahi kuonekana awali.

Wanyama pori wanapungua kwasababu ya uchomaji wa miti, kuvua samaki kupita kiasi, na kufanya uharibifu katika maeneo ambayo wanyama pori wanaishi kulingana na Tanya Steele, afisa mkuu mtendaji katika WWF.

''Tunaharibu dunia yetu mahali tunapoita nyumbani - tukihatarisha afya yetu , usalama na kuishi duniani''.

''Sasa asili inatutumia ujumbe wa kwamba muda unayoyoma''.

Je idadi hiyo ina maana gani?

Ripoti hiyo iliangazia spishi tofauti za wanyama wanaochunguzwa na wanasaansi wa uhifadhi katika maeneo wanaoishi kote duniani.

Walirekodi upungufu wa wastani wa asilimia 68 katika zaidi ya wanyama 20,000 wanaoshirikisha wale wanaoishi porini, ndege, wanyama wanaoishi ardhini na majini, wanyama wa kutambaa na samaki tangu 1970

''Upungufu huo ni ushahidi tosha wa uharibifu unaofanywa na wanadamu katika asili ya duniani'' , alisema Dkt. Andrew Terry , mkurugenzi wa uhifadhi katika mbuga ya wanyama ya London ambayo ilitoa takwimu hizo.

Iwapo hakuna kitakachotokea , idadi ya wanyama itazidi kupungua na kuangamia hatua itakayotishia uadilifu wa mazingira ambayo tunategemea , aliongezea.

Ripoti hiyo inasema kwamba mlipuko wa Covid- 19 ni ukumbusho kuhusu jinsi asili na wanadamu wanaingiliana.

Sababu zilizodaiwa kusababisha mlipuko huo ni pamoja na ukosefu wa makazi na ufanyaji wa biashara ya wanayama pori.

Ushahidi mpya unaonesha kwamba tunaweza kuzuia na hata kusitisha upungufu wa makazi na ukataji wa misitu iwao tutachukua hatua za uhifadhi na kubadili jinsi tunavyozalisha chakula na kukitumia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sokwe wa milima ya DRC wanakabiliwa na tishio kutokana na uwindaji haramu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tembo wapo katika hatari ya uwindaji haramu na ukosefu wa makazi