Mawasiliano yana uwezo mkubwa kutatua tatio la afya ya akili

Mawasiliano yana uwezo mkubwa kutatua tatio la afya ya akili

Septemba 10 kila mwaka ni Siku ya Kuzuia Kujiua Ulimwenguni .

Siku hii ni ya ufahamu ya kila mwaka iliyoundwa ili kuweza kufahamu matatizo yanayowakumba watu wanaotaka kujiua na nama ya kuwasaidia.

Utafiti unaonyesha kuwa mawasiliano ya wazi na ya kweli juu ya ugonjwa wa akili husaidia hatua za kuzuia kujiua, kwa sababu mazungumzo haya muhimu yana uwezo wa kuongeza ufahamu na uelewa, kuwaondolea upweke na kusaidia kuondoa unyanyapaa ambao unaweza kuwa kikwazo kwa wale wanaotafuta msaada.

Takriban watu laki nane hujiua kila mwaka, hivyo inaonesha kwamba kujiua ni jambo linaloikumba dunia nzima na hufanyika katika kipindi chote cha maisha.

Je! Tunajuaje kwamba mtu yuko katika hatua ya kujiua? Tunawezaje kumasaidia?

Mwandishi wa BBC, Scolar Kisanga alifanya mazungumzo na wataalamu wa afya ya akili