Femi Otedola: Bilionea wa Nigeria aliyewanunulia watoto wake magari ya Ferrari Portofino

DJ Cuppy father Femi Otedola gift Ferrari Portofino to im daughters

Chanzo cha picha, DJ Cuppy

Bilionea wa Nigeria awazawadia watoto wake magari ya Ferrari Portofino.

Hatua ya bilionea Femi Otedola kuwanunulia mabinti zake watau magari ya kifahari imezua gumzo katika mitandao ya kijamii nchini Nigeria.

Femi Otedola, ambaye ni tajiri mkuwa katika sekta ya mafuta, aliwazawadia mabinti zake magari aina ya Ferrari Portofino.

Florence Ifeoluwa Otedola anayefahamika kwa jina maarufu kama DJ Cuppy aliweka mtandaoni picha ya magari waliyonunuliwa na baba yao siku ya Jumatano.

Aliandika baba yao amenunua magari matatu kwa watoto wake watatu- Tolani, Temi na Ifeoluwa Otedola.

Data kutoka kwa Wikipedia inaonesha Femi Otedola ana mali ya zaidi ya dola bilioni 1.85 za Kimarekani.

"Baba yetu alitupeleka dukani na kutununulia kila mtu gari lake!", kwa mujibu wa ujumbe uliowekwa kwenye Twitter na Temi Otedola.

Maelezo kuhusu magari hayo

Bei ya Ferrari Portofino inakadiriwa kuwa dola 218,750.

Gari hilo sio kubwa sana na muundo wake ni wa V8 lakini mwendo wake ni wa kasi sana.

Cha kushangaza licha ya muonekano wake haitumii mafuta mengi.

Mwaka 1947, Enzo Ferrari alianza kuunda magari ya Ferrari katika mji wa Maranello, Italia.

Ni watu waliokula chumvi kisawa sawa walio na uwezo wa kununua gari hili.

Magari hayo yalivyozua gumzo kwenye Twitter

Laycon Brother alisema, huu ni ufujaji wa pesa za umma! hata hatujui thamani ya gari walilotengeneza. Je! Otedola anapaswa kutoa pesa kwa masikini, badala ya kufanya hivi? Natumai EFCC itachunguza. Laycon da Nengi

Adionne aliuliza, Mamlaka ya kukabiliana na uhalifu wa kiuchumi EFCC inaingia wapi suala hili? Mtu amewanunulia watoto wake magari sasa mwataka EFCC ichunguze? Mnashangaza sana.

YorubaBoy anasema baba awanunulia Ferrari 3 kwa watoto wake. Nataka kuwa na Baba kama Otedola . Cuppy niko tayari kuwa na jina lako la mwisho. Mahari ni nafuu.

Chanzo cha picha, DJ Cuppy

Chanzo cha picha, DJ Cuppy

Chanzo cha picha, DJ Cuppy

Chanzo cha picha, DJ Cuppy

Chanzo cha picha, DJ Cuppy

Maelezo ya picha,

Bei ya Ferrari Portofino inakadiriwa kuwa dola 218,750.

Chanzo cha picha, DJ Cuppy

Maelezo ya picha,

Watoto wa Otedola: Tolani, Temi na Ifeoluwa kila mmoja amepata Ferrari Portofino

Chanzo cha picha, DJ Cuppy

Chanzo cha picha, DJ Cuppy