'Niligundua kuwa dada yangu alikuwa mama yangu mzazi'

Albert alikuwa na miaka 21 alipogundua ukweli kuhusu mama yake mzazi
Maelezo ya picha,

Albert alikuwa na miaka 21 alipogundua ukweli kuhusu mama yake mzazi

Albert Gilmour aligundua 21, 1965 siri ya familia yake kuhusu kuzaliwa kwake. Kwa mara ya kwanza ameamua kusimulia BBC kisa hicho cha kuvunja.

Anasema mwanamke ambaye amekuwa akimchukulia kama dada yake mkubwa ni mama yake mzazi, kwasababu hakuambiwa ukweli tangu alipozaliwa.

Baba yake Gilmour alikuwa mmoja wa maafisa 300,000 wa kikosi cha Marekani waliopelekwa Ireland Kaskazini wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

"Niligundua kuwa dada yangu mkubwa alikuwa mama yangu mzazi. Ilikuwa vigumu sana kwangu kukubali ukweli. Ikiwa ulizaliwa nje ya ndoa ni sawa na mtu ambayo hana utambulisho," alisema Albert.

Ruby alikuwa na miaka 17 alipokutana na askari mmoja katika kambi ya kijeshi ya Eglinton County. Walitenganishwa baada ya mwanamume huyo kuhamishwa kisiri hadi kambi nyingine ya kijeshi.

Maelezo ya picha,

Albert hajawahi kumsimulia mtu yeyote kisa hiki

Alipomzaa mwanawe wa kiume, alimpatia jina la Alberto ambalo pia ni jina la baba yeke, na kumlea kana kwamba alikuwa dada yake, kwa sababu aliamini aliuawa katika vita.

Alisimulia BBC kisa chaka akiwa na hisia mseto,wakati mwingine anacheka, wakati mwingine anatekwa na mawazo akikumbuka maisha yake yalivyokua.

"Nilitamani sana kukutana na baba yangu baba yangu, na nilitaka kujumjua na kuona anakaa vipi.

Wakati mwingine ningelisimama mbele ya kioo na kuangalia usu wangu, nikitafakari jinsi ningefananisha sura zetu laity angelikwa amesimama kando yangu." Alisema.

Miaka 30 baadae, binti ya Albert hatimae amekutana na familia yake ya Kimarekani.

Akielezea kisa hicho Karen Cook, alisema: " Zawadi nzuri zaidi anayoweza kumpatia baba yake ni kukutana na jamaa zake wengine ambao watasalia kuwa jamaa zangu nchini Marekani."

Maelezo ya picha,

Baba yake Albert alikuwa mwanajeshi wa Marekani

Hata hivyo aliamua kusafiri hadi jimbi la Maine, kukutana na jamaa wengine katika familia ya baba yake.

"Nilipofika Marekani, punde ndege ilipotua nchini humo nilijihisi nipo nyumbani. Nilisema na mama yangu Ruby Gilmour na niliporudi nyumbani kutoka Marekani alitaka kujua kama nilipata picha ya baba. Na ile niliyopata ilikuwa inamuonesha mama.

"Nilimuonesha mama yangu ili aone sura yake tena na alilia sana.

Aliichukua hiyo picha na kuiweka kwenye kipochi chake hadi alipofariki."

Mama na baba yangu hawakufurahia kuwa mbali mbali

Chanzo cha picha, ALBERT GILMOUR

Maelezo ya picha,

Wapenzi hao walifariki katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia

Albert anasema hali iliyomfanya atenganishwe na wazazi wake ilikuwa ni jambo ambalo haliwezi kuepukika.

"Mama yangu alianiambia alisononeka sana alipoondoka na kwamba yeye pia alipata usumbufu wa akili kwa sababu hakuwa na ufahamu ikiwa yuko hai ama amefariki na hakuwa na jinsi ya kuwasiliana naye.

Nilimletea picha na kumfahamisha kuwa amefariki. Alinishika mkono na kusema, 'Samahani,' nami nikamjibu, 'Huna haja ya kuniomba msamaha.'

Albert atakuwa na miaka 75 kufikia mwezi Novemba.

Kisa chake hakikua kimeangaziwa katika vyombo vya habari, anatumai kitakuwa kielelezo kwa watu wengine wanaokabiliwa na hali kama yake watafuata nyayo zake ili nao wapate utulivu.