Je ni kiwango gani cha dhahabu kilichosalia duniani?

Gold bullion bars polished at the ABC Refinery in Sydney.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Janga la Covid-19 laimarisha uwekezaji wa dhahabu

Mwezi uliopita bei ya dhahabu ilikuwa ya juu zaidi ambapo gramu 28 thamani yake ilikuwa zaidi ya pauni 1,575 ya juu ya dola 2,000.

Wakati bei hii ilitokana na wafanyabiashara wa dhahabu, pia ilizua swali la usambaaji wa madini hayo adimu na ni lini hasa yatakuwa hayapatikani tena duniani.

Dhahabu ni madini ambayo uhitaji wake ni wa juu sana katika uwekezaji, na kiungo muhimu katika bidhaa nyingi za kielektroniki.

Lakini pia ni bidhaa adimu ambayo ipo siku itakuwa haipatikani kabisa duniani.

Kilele cha upatikanaji wa dhahabu

Wataalamu wanazungumzia suala la kilele cha madini ya dhahabu - wakati ambapo yamechimbwa kwa wingi zaidi kuliko kipindi chochote kile cha mwaka. Baadhi wanaamini kwamba huenda tayari tumefikia kiwango hicho.

Uchimbaji wa madini ya dhahabu kwa jumla unasemekana kuwa tani 3,531 mwaka 2019, ikiwa chini kwa asilimia 1 ikilinganishwa na mwaka 2018, kulingana na Baraza la Usimamizi wa Dhahabu Duniani. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa uzalishaji wa dhahabu kupungua tangu mwaka 2008.

"Wakati uchimbaji wa madini huenda ukakua kasi ya polepole au ukapungua kidogo miaka ijayo, kwasababu madini hayo yameisha kwenye hifadhi zake, na ugunduzi wa hifadhi mpya umekuwa nadra sana, kunaashiria kwamba suala la kuwa kilele cha uzalishaji wa dhahabu huenda bado hakijafikiwa," amesema Hannah Brandstaetter, msemaji wa Baraza la Dhahabu Duniani.

Hata ikiwa kilele chake kitafikiwa, wataalamu wanasema miaka tu baada ya hatua hiyo, huenda isishuhudie kupungua kwa kiasi kikubwa kwa madini ya dhahabu moja kwa moja, badala yake, kitakachoshuhudiwa ni kupungua taratibu kwa uzalishaji wa madini hayo kwa miongo kadhaa ijayo.

"Uzalishaji wa madini umeshindwa kuongezeka na kuna uwezekano ukapungua, lakini sio kwa haraka mno," ameongeza Ross Norman wa tovuti ya madini ya MetalsDaily.com.

Je ni kiasi gani cha madini ya dhahabu kilichosalia?

Makampuni ya migodi yanakadiria dhahabu iliyosalia chini ya ardhi kwa njia mbili:

Hifadhi - dhahabu ambayo inapatikana kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na bei yake wakati huo.

Raslimali - Dhahabu ambayo huenda ikapatikana na kutumika kibiashara baada ya uchunguzi zaidi, au ikiwa itauzwa kwa bei ya juu zaidi

Idadi ya hifadhi ya dhahabu inaweza kuhesabika kwa usahihi zaidi kuliko raslimali, ingawa hili bado sio jukumu rahisi.

Hifadhi ya dhahabu chini ya ardhi kwasasa hivi inakadiriwa kuwa karibu tani 50,000, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.

Ili kuliweka sawa, karibu jumla ya tani 190,000 za dhahabu zimechimbwa ingawa makadirio hayo yanatofautiana.

Kulingana na takwimu za makadirio, kuna karibu asilimia 20 ya dhahabu ambazo bado hazijachimbwa.

Aidha teknolojia mpya huenda pia zikawezesha upatikanaji wa madini hayo katika baadhi ya sehemu ambazo sasa hivi hazifikiwi.

Katika baadhi ya sehemu, roboti zimeanza kutumiwa na zinatarajiwa kuendelea kutumika kama hatua moja iliyopigwa kiteknolojia katika uchimbaji wa madini migodini.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Inaendelea kuwa vigumu na gharama ya juu kuchimba madini ya dhahabu

Vyanzo vikubwa

Chanzo kimoja kikubwa cha madini ya dhahabu katika historia kimekuwa eneo la bonde la Witwatersrand Afrika Kusini. Witwatersrand inakadiriwa kuchangia asilimia 30 ya madini yote ya dhahabu yaliyowahi kupatikana.

Vyanzo vingine vya dhahabu ni mgodi wa Mponeng Afrika Kusini, migodi ya Super Pit na Newmont Boddington iliyopo Australia, mgodi wa Grasberg uliopo Indonesia na ile ya Nevada nchini Marekani.

Sasa hivi China ndio yenye mgodi mkubwa wa dhahabu huku Canada, Urusi, na Peru pia nao zikiwa wazalishaji wakubwa wa dhahabu.

Changamoto katika uchimbaji wa dhahabu ni zipi?

Uchimbaji madini mkubwa unahitaji mtaji mkubwa, mashine kubwa na ya hali ya juu, na wataalamu katika maeneo ya mgodini juu na chini ya ardhi.

Leo, karibu asilimia 60 ya shughuli za uchimbaji wa madini zinafanyika juu ya ardhi, huku asilimia iliyosalia zikifanyika chini ya ardhi.

"Shughuli za uchimbaji madini zinaendelea kuwa ngumu kwasababu migodi mingi ni mikubwa, thamani yake ni ya chini, na pia ni ya zamani sana kama ile ya Afrika Kusini, madini yanakaribia kumalizika," ameongeza Bwana Norman.

"Upande mwingine, migodi ya dhahabu ya China, ni midogo, na hivyo basi thamani yake ni ya juu."

Kuna baadhi ambayo bado madini hayo yanapatikana, isipokuwa inapatikana sehemu zisizo na uthabiti, kama Afrika Magharibi.

Rekodi ya juu ya dhahabu

Ingawa bei ya dhahabu, ilikuwa juu zaidi Agosti, hii haimaanishi kwamba shughuli za uchimbaji dhahabu zinaongezeka.

"Ukiangalia shughuli zinazoendelea, inachukua muda kufanya mabadiliko ya shughuli za uchimabji migodi kwasababu nyinginezo kama vile bei ya bidhaa hiyo," ameongeza Bwana Brandstaetter.

Pia, bei ya juu ya madini hayo iliyorekodiwa, kumetokea wakati wa kipindi cha virusi vya corona, na kufanya iwe vigumu kuendesha shughuli za uchimbaji ambapo baadhi ya ama ilifungwa kwa muda au kabisa kama njia moja ya kukabiliana na virusi vya corona.

Kuongeza kwa bei ya bidhaa hiyo kumetokana na janga la corona kwasababu wawekezaji wanachukulia dhahabu kama bidhaa salama wakati wa sintofahamu za hali ya kiuchumi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Dhahabu inapatikana hadi kwenye mwezi

Maeneo ambayo dhahabu yake huenda isiwe na thamani kiuchumi

Huenda ikawa vigumu kutathmini dhahabu ya chini ya ardhi lakini sio chanzo cha pekee.

Hata hivyo, gharama ya upatikanaji wake na kuisafirisha tena hadi ardhini ziko juu mno ikilinganishwa na thamani ya dhahabu yenyewe.

Vivyo hivyo kuna baadhi ya hifadhi za dhahabu zinazofahamika huko Antaktika ambazo huenda zisiwe na manufaa ya kiuchumi, kwasababu ya hali mbaya ya hewa.

Dhahabu pia inapatikana katika sehemu nyingi za sakafu ya baharini lakini pia inachukuliwa isiyokuwa na thamani ya kiuchumi.

Tofauti na rasilimali nyingine kama vile mafuta isiyoweza kutumika tena, dhahabu inaweza kuchakatwa tena. Hilo likiwa sawa na kusema, dhahabu haiwezi ikamalizika kabisa hata itakapofikia wakati ikawa haiwezi kuchimbwa tena.

Kiasi kikubwa cha dhahabu kinatumika katika bidhaa za kielektroniki ambazo mara nyingi huchukuliwa kama za kutumiwa na mwisho wake ni kutupwa kama vile simu za mkononi. Kiwango cha dhahabu katika utengenezaji wa bidhaa kama simu kina thamani ya pauni kadhaa.

Pia unaweza kutazama:

Maelezo ya sauti,

Kupanda kwa bei ya dhahabu kwenye soko la dunia kunavyoinufaisha Tanzania