Trump sasa asema kundi la mrengo wa kulia likae kando huku mgogoro wa kundi la wazungu ukiendelea

US President Donald Trump and Democratic presidential nominee Joe Biden participate in their first 2020 presidential campaign debate

Chanzo cha picha, Reuters

Rais Donald Trump amesema kuwa kundi la mrengo wa kulia linastahili kutulia na kuacha sheria kufanyakazi baada ya kukataa kulishutumu moja kwa moja katika mdahalo wa wagombea urais ulioendeshwa kupitia televisheni na kusababisha gumzo.

Bwana Trump amesema "Sijui Proud Boys ni kina nani", siku moja baada ya kusema kwenye mdahalo na mpinzani wake Joe Biden anataka kundi hilo "kukaa kando na kuwa tayari".

Wanachama wa kundi la Proud Boys wamesema matamshi yake ni kihistoria na ameliidhinisha.

Bwana Biden alisema Bwana Trump alikuwa "amekataa kukana kundi la wazungu".

Mabadilishano hayo yaliwadia wakati wa mjadala wa kwanza wa mahojiano ya kwenye televisheni kati wawili hao kabla ya uchaguzi wa Novemba 3.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wanachama wa kundi la Proud Boyskatika mkutano kampeni huko Portland, Oregon

Mdahalo huo ulibadilika na kuwa mabishano, ugomvi na matusi huku vyombo vya habari vya Marekani vikiuelezea kama vurugu tupu na mbaya usio kifani.

Tume inayodhibiti midahalo imesema itaanzisha hatua mpya katika mdahalo utakaofuata kuhakakisha kunakuwa na mwelekeo. Bwana Trump kwa upande wake amesema wanastahili kuwa na mtangazaji mwingine atakayeendesha midahalo hiyo na mgombea mwerevu wa Democratic.

Sio mengi yaliyojitokeza kwa misingi ya sera hata ingawa moja ya kura za maoni ilimpa Bwana Biden ushindi mdogo huku maoni mingine yakiashiria asilimia 90 ya Wamarekani tayari wameshafanya maamuzi yao juu ya mgombea watakaye mpigia kura na huenda mdahalo huo ukawa na mchango kidogo kimaamuzi kwa raia.

Je Trump amesema nini kuhusu Proud Boys?

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Aliyeendesha mdahalo wa Urais ni mtangazaji wa kituo cha habari cha Fox News Chris Wallace aliyekuwa na wakati mgumu kuhakikisha haukosi mwelekeo

Mwendeshaji wa mdahalo Chris Wallace aliuliza ikiwa rais atashutumu kundi la wazungu na kuwataka wakae kando wakati wa maandamano.

Hilo limesababisha gumzo zaidi hata kuliko masuala mengine kama mauaji ya polisi na ubaguzi.

"Hakika niko tayari kufanya hivyo... lakini naweza kusema kila kitu ninachoona kinatokana na upande wa kushoto, wala sio mrengo wa kulia," Bwana Trump amesema.

Bwana Biden alisema mara mbili kundi la "Proud Boys" pale rais alipouliza ni kundi gani analoambiwa alishutumu.

Rais alisema: "Proud Boys - kaeni kando na muwe tayari. Lakini nitasema kwamba... Lazima kuna mtu alifanya kitu kuhusu kundi la antifa na kuondoka kwasababu hili sio tatizo la mrengo wa kulia."

Baada ya kuanzishwa 2016, kundi la Proud Boys ni la mrengo wa kulia, linalopinga wahamiaji, kundi la wanaume watupu wenye historia ya kufanya ghasia mitaani dhidi ya wapinzani wao wa mrengo wa kushoto. Mmoja wa kundi hilo la Proud Boys amechapisha nembo kwenye mtandao wa kijamii inayosema "Kaeni kando na muwe tayari,."

Bwana Biden pia nae alishutumiwa kwa kundi la conservatives kwa kupuuzilia mbali tishio la kundi la antifa.

Antifa ni kundi lenye kuhusishwa kwa mbali na wanaharakati wa mrengo wa kushoto ambalo mara nyingi hukabiliana na wanandamanaji wa mrengo wa kulia.

Wakati wa mdahalo, Bwana Biden alimnukuu mkurugenzi wa shirika la upelelezi Marekani FBI akisema kwamba "antifa ni wazo sio shirika".

Mkurugenzi wa kundi la FBI alisema mbele ya bunge mwezi huu kwamba antifa ni vuguvugu ambalo linajumuisha "waasi wenye msimamo mkali".

Wizara ya sheria ya Marekani imeshutumi kundi la antifa la kuchochea ghasia zenye kuhusishwa na uporaji katika miji ya Marekani mwaka huu.

Je Trump alithibitisha vipi maoni yake?

Alikuwa akizungumza katika Ikulu ya Marekani Jumatato kabla ya ziara ya kampeni huko Minnesota. Mwanahabari alimuuliza kuhuau kundi la Proud Boys na alisema: "Sijui hao kina nani. Naweza tu kusema wanastahili kukaa kando na kuacha sharia ifanye kazi yake."

Alirejelea hitaji lake kwamba Bwana Biden ashutumi shughuli za kundi la Antifa.

Hakuelezea maana ya kutumia neno "muwe tayari" wakati wa mdahalo na kusema kwamba alitaka tu "sheria kuwa jambo la msingi katika kampeni zao" alipoulizwa ikiwa anaunga mkono kundi la wazungu.

Chanzo cha picha, Reuters

Trump ameshutumiwa na nini?

Joe Biden alirejelea suala hilo katika mtandao wa Twitter Jumatatno, akisema: "Hakuna namna nyingine ya kuweka suala hili: Rais wa Marekani alikataa kukana kundi la wazungu wakati wa mdahalo jana usiku."

Katika ujumbe wake alinukuu, hotuba ya rais, kutoka kwa jukwa la kundi la Proud Boys iliyosema: "Hili linanifanya niwe mwenye furaha ajabu. Tuko tayari!

Bila shaka kundi la Proud Boys linaona ni kama limeungwa mkono na rais Trump.

Mratibu wa kundi hilo Joe Biggs aliandika: "Rais Trump ameliambia kundi la proud boys kuwa tayari kwasababu mtu anahitajika kukabiliana na kundi la antifa... Bwana! Tuko tayari!!"

Mwingine akasema kundi hilo tayari limeanza kutafuta kusajili wanachama wapya.

Baadhi ya malumbano yaliyotokea

  • Miongoni mwa matusi waliokuwa wakirushiana, Bwana Biden alimuita rais "mwanasarakasi". Alimuambia rais: "Nyamaza mwanaume wewe?" na baadae akisema "endelea kubweka tu, mwanaume"
  • Bwana Trump alisema Bwana Biden alikuwa amehitimu ama kwa kuwa wa mwisho au karibu na mwisho darasani na hana chochote alichopata licha ya kuwa kwenye siasa kwa miaka 47
  • Bwana Biden alisema Bwana Trump amepata hofu juu ya janga la virusi vya corona na watu wengi wamekufa. Bwana Trump baadae aliandika ujumbe kwamba wengi zaidi wangekufa ikiwa Bwana Biden ndio angekuwa rais.
  • Bwana Trump alitetea juhudi zake za kujaza nafasi ya jaji mkuu katika mahakama ya juu zaidi nchini humo, huku Joe Biden akikataa kujibu alipoulizwa ikiwa angejaribu kuongeza idadi ya mahakimu
  • Alipoulizwa ikiwa angehamasisha wafuasi wake kuhakikisha amani ikiwa matokeo ya uchaguzi yangetokea kutokuwa na uhakika sana, Bwana Trump alisema: "Nahamasisha wafuasi wangu kujitokeza kupiga kura kwa umakini"
  • Bwana Trump aliposema ikiwa Bwana Biden angekuwa katika upande wa kushoto wa chama cha Democratic kuhusu masuala ya afya na sera ya mazingira, Bwana Biden amejibu: "Mimi ni wa chama cha Democratic sasa hivi"