Uchaguzi wa Marekani 2020: Papa Francis akataa kuonana na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo

US Secretary of State Mike Pompeo is in Italy on a state visit

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo yuko Italia kwa ziara rasmi

Vatican imemkatalia waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo kuonana na Papa Francis.

Kiongozi huyo wa juu wa Kanisa Katoliki ameelezwa kuwa hawapokei wanasiasa wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Hatua hiyo inaongeza hali ya mzozo wa kidiplomasia baada ya kauli ya Bwana Pompeo kuhusu China na Kanisa Katoliki.

Vatican ilimshutumu Pompeo kuwa anajaribu kutumia suala hilo kuvutia wapiga kura wa uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba nchini Marekani.

Katika makala ya mwanzoni mwa mwezi Septemba, Bwana Pompeo alisema kanisa Katoliki linapoteza ''mamlaka yake ya kinidhamu'' kwa kufanya makubaliano mapya na China kuhusu uteuzi wa maaskofu.

Donald Trump anapata uungwaji mkono kutoka kwa mashirika ya kidini ya kihafidhina, pamoja na wapiga kura wa Kikatoliki wa kihafidhina, ambao wengine wanadhani Papa Francis ni mtu mwenye uhuru sana.

Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa Wakatoliki wengi nchini China wanateswa kwa kuahidi utii kwa Papa badala ya chama rasmi cha Wakatoliki nchini China.

Pamoja na hayo, mnamo 2018 Vatican ilifanya makubaliano na China kuwa na maoni juu ya uteuzi wa maaskofu wa China.

Wakati huo Papa Francis alisema alikuwa na matumaini kuwa mpango huo "utaruhusu vidonda vya zamani kupona" na kuleta umoja kamili wa Kikatoliki nchini China.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kufanywa upya mwezi ujao kukiwa na upinzani kutoka kwa Wakatoliki wengine, pamoja na Marekani.

Katika hotuba yake Jumatano huko Roma Bw Pompeo alitaka Vatican kutetea uhuru wa kidini nchini China, akisema "hakuna mahali popote palipo na uhuru wa kidini unaoshambuliwa zaidi ya China."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

vatican imesema Papa haonani na wanasiasa wakati wa uchaguzi

Wanadiplomasia wa juu wa Vatican, Waziri wa mambo ya nje Kadinali Pietro Parolin na waziri wa mambo ya kigeni Askofu Mkuu Paul Gallagher, amesema Papa Francis hatampokea Bwana Pomp

''Papa aliweka wazi kabisa kuwa wanasiasa hawatapokelewa katika kipindi cha uchaguzi. Hii ndio sababu,'' Kadinali Parolin alisema, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Wanasiasa wawili pia wamegusia ukosoaji wa hadharani wa Bwana Pompeo dhidi ya Papa kama jambo la kushtusha na Askofu Mkuu Gallagher amesema kuwa masuala ya mjadala yanapaswa kuzungumzwa ''faragha''.

Kadinali Parolin pia amesema inawezekana kauli ya Pompeo imelenga kuwahamasisha Wakatoliki kumuunga mkono Trump katika kura za mwezi Nove

"Wengine wametafsiri kwa njia hii - kwamba maoni yalikuwa juu ya matumizi ya kisiasa ya nchini Marekani. Sina uthibitisho wa hii lakini kwa hakika hii ni njia moja ya kuiangalia," alieleza.

Aliongeza kuwa mpango wa Vatican na China hauhusiani na Marekani.