Japan: Mwanamume akiri kuwaua watu tisa aliokutana nao mtandaoni

Japan: Mwanamume akiri kuwaua watu tisa aliokutana nao mtandaoni

Mwanamume mmoja raia wa Japan amekiri kuwauwa watu tisa baada ya kuwasiliana nao kupitia mtandao wa Twitter.kesi hio imewashutua watu wengi nchini humo.Takahiro Shiraishi alikamatwa mnamo 2017 baada ya sehemu za miili ya watu kupatikana nyumbani kwake.Je unaamini mitandao sio mahali salama pa kukutana na watu usiowajua?