Uchaguzi Tanzania 2020: Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Semistocles Kaijage amjibu Tundu Lissu

Uchaguzi Tanzania 2020: Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Semistocles Kaijage amjibu Tundu Lissu

Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania imejibu madai yaliyotolewa na Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kuhusu mwenendo wa uchaguzi nchini humo.

Akizungumza na BBC mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amejibu hoja za mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu pamoja na hoja za Baraza la wazee wa CHADEMA ya kutaka Tume hiyo iwarejeshe wagombea zaidi ya 1000 wa udiwani na zaidi ya 50 wa Ubunge wa CHADEMA walioenguliwa kwenye kinyang’anyiro.

Uchaguzi mkuu nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi Oktoba