Tazama vita vya sokwe vilivyodumu miaka 4 Tanzania

Tazama vita vya sokwe vilivyodumu miaka 4 Tanzania

Tafiti mbalimbali zilizofanywa kuhusu Wanyama aina ya Sokwe, matokeo yake mengi ikiwemo tabia za nyani hufananishwa na binadamu. Kama ilivyo kwa binadamu Sokwe pia huwa na migogoro baina yao.

Huko nchini Tanzania kulitokea vita vya Sokwe vilivyodumu kwa miaka minne. Vita hivyo vilihusisha jamii mbili za Sokwe zilizojulikana kama Kahama na Kasekela.

Mtafiti nguli wa masuala ya nyani Jane Goodall alitoa taarifa za kwanza za migogoro baina ya jamii ya Sokwe.

Kwa mujibu wa vitabu vya tafiti zake Jane anasema kuwa vita vya Sokwe vilimshtua sana hakutarajia kama viumbe hao wangefanana sana na binaadamu kiasi cha kupigana vita.

Taarifa ya Munira Hussein inasimuliwa na Eagan Salla