Kura ya kutokuwa na imani na Rais Trump: Je, ni nini kinachofanyika baada ya rais kupigiwa kura hiyo Marekani?

Bill Clinton in 1998

Chanzo cha picha, Alamy

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa rais wa kwanza katika historia kushitakiwa mara mbili na Bunge la Wawakilishi - na anasalia kuwa mmoja kati ya watatu ambao tayari wameshtakiwa.

Fahamu kilichowakuta wengine.

Andrew Johnson

Chanzo cha picha, Print Collector/Getty Images

Maelezo ya picha,

Andrew Johnson alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kushtakiwa

Alifanya nini?

Chini ya kivuli cha vita vya wenyewe kwa wenyewe, Rais Andrew Johnson - wa Demokratic - alizozana mara kwa mara na bunge ambalo lilikuwa linadhibigtiwa na chama cha Republican - bungeni kuhusu namna ya kujenga upya eneo la kusini la Marekani liloshindwa.

"Warepublican wenye misimamo mikali" wakati huo walipitisha sheria ya kuwaaadhibu viongozi wa zamani wa majimbo na kulinda haki ya watumwa walioachiliwa huru. Johnson alitumia nguvu yake ya rais kupinga juhudi za Republican katika kila hatua.

Mwezi Machi, Bunge lilipitisha sheria ya ukomo wa urais, iliyobuniwa kudhibiti uwezo wa rais kuwafuta kazi mawaziri wake bila kuidhinishwa na Seneti.

Katika hatua ya kukaidi sheria hiyo, Johnson alimsimamisha kazi waziri na mpinzani wake wa kisiasa, Edwin Stanton, wakati bunge lilipokuwa mapumzikoni.

Ikiwa kesi za leo zinaonekana kuwa na mihemko ya kisiasa, ni utamaduni unaohusishwa na mashtaka hayo: Stanton alijibu hatua ya kufutwa kwake kwa kujufungia ndani ya afisi yake na kukataa kuondoka.

Kuondolewa kwa Stanton kulionekana kuwa hatua ya mwisho - wabunge katika bunge la uwakilishi walikimbilia kuandaa nakala 11 za mashtaka.

Chanzo cha picha, Library of Congress

Maelezo ya picha,

A wood engraving shows the Senate trial of Andrew Johnson

Baada ya kura iliopigwa kwa misingi ya chama, nakala za mashtaka ziliwasilishwa kwa Bunge la Seneti, ambalo lilimuondolea makosa lakini aliponea kwenye tundu la sindano. Ni kura moja tu iliosababisha kutofikiwa kwa thuluthi mbili ya kura zilizohitajika kumshtaki.

Matokeo yalikuwa nini?

Kwa mujibu wa baadhi ya walioshuhudia, Johnson alilia alipopokea taarifa za kuondolewa kwake hatiani, na kuapa kurekebisha mwenendo wake.

Haikufanya kazi.

Alihudumia muda wake wote wa urais, lakini miezi ya mwisho ya utawala wake ilikabiliwa na mzozo wa uongozi ambao ulizunguka urais wake kabla ya kushtakiwa.

Na mwaka 1869, Wanademokrat walipoteza udhibiti wa White House kwa mgombea wa Republican Jenerali Ulysses S Grant, ambaye aliruhusu mpango wa marekebisho kuendelea .

Uongozi wake ulikuwa vipi?

Kushtakiwa.

Na mwaka 1867 alinunua jimbo la Alaska kwa kima cha dola milioni 7.2.

Johnson pia alikuwa mmoja wa marais maskini. Hakwenda shule.

Chanzo cha picha, Universal History Archive/Getty Images

Richard Nixon

Chanzo cha picha, Don Carl STEFFEN/Gamma-Rapho via Getty Images

Alifanya nini?

Kushtakiwa kwa Richard Nixon kulitokana na uvamizi wa makao makuu ya chama cha Democratic mwaka 1972 katika jengo la Watergate mjini Washington DC.

Uchunguzi ulibaini kuwa wezi walilipwa fedha za kampeni ya kuchaguliwa tena kwa Nixon, huku kashfa ya Watergate ikizidi ilisambaa zaidi na kuwahusisha maafisa wa Ikulu ya White House.

Kwa karibu miaka miwili iliopita, Nixon alijitahidi kuficha jukumu lake katika njama hiyo, iliosababisha kifo chake.

Juhudi za rais wa Republican ziligonga mwamba. Mwezi Agosti mwaka 1974, wakati kamati ya haki ilipotayarisha nakala za mashtaka, Nixon alilazimika kutoa rekodi zilizonaswa katika ofisi ya rais ambapo sauti ya rais inasikika akimwelekeza mfanyakazi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA kuliambia shirika la upelelezi la FBI kukomesha uchunguzi wake kuhusu kashfa ya Watergate.

Mnamo mwezi Julai 27 mwaka huo, kamati ya bunge ya masuala ya haki ilipiga kura kuidhinisha mashtaka matatu ya - kuzuia utekelezaji wa haki, utumizi mbaya wa madaraka na kupuuza uamuzi wa bunge - na kuiwasilisha kwa bunge lote kupigiwa kura kamili.

Lakini kura hiyo haikupigwa.

Mnamo Agosti 8, 1974 Nixon alijiuzulu. Anasalia kuwa rais wa pekee Marekani katika historia kufanya hivyo.

Chanzo cha picha, Bettmann/Getty Images

Maelezo ya picha,

Nixon akiwaagia wafanyakaziwake baada ya kutangaza kujiuzulu kwake

"Sijawahi kukwepa matatizo,"katika hotuba ya kujiuzulu kwake. "Kuondoka madarakani kabla ya muda wangu kukamilika inaumiza kila sehemu ya mwili wangu. Lakini kama rais, Lazima niweke mbele maslahi ya Marekani kwanza."

Matokeo yalikuwa nini?

Makamu wa Rais Gerald Ford aliapishwa wiki sita baadae, na Nixon kusamehewa makosa yote aliyofanya akiwa madarakani.

Uchaguzi ulifanywa chini ya miaka miwili baadae, Ford alishindwa na Jimmy Carter wa chama cha Demokratic katika kinyan'ganyiro cha kuingia ikulu ya Marekani.

Uongozi wake ulikuwa vipi?

Hakukua na pingamizi kuhusu jukumu lake katika kashfa ya Watergate. Japo hakuwahi kukiri makosa, vitendo vyake vinasalia kuwa hadithi inayoangazia matumizi mabaya ya madaraka ya urais.

Nixon alifariki mwezi Aprili 1994, miaka 20 baada ya kujiuzulu kwa kufedheheka.

Akizungumza katika mazishi yake, aliyekuwa rais wakati huo Bill Clinton aliangazia mchango wa Nixon katika masuala ya kigeni.

Bill Clinton

Chanzo cha picha, GEORGE BRIDGES/Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais Clinton akihutubia taifa baada ya kustakiwa na Bunge la wawakilishi

Alifanya nini?

Miaka michache baada ya Rais Bill Clinton kuhubiri msamaha kutokana na makosa ya Nixon, manasiasa huyo wa chama cha Demokratik kutoka Arkansas Democrat alikabiliwa na mzozo wake wa kisiasa.

Ndani ya mwaka mmoja baada ya kuchukua hatamu ya uongozi, Clinton alijipata akichunguzwa na mwendesha mashtaka maalum wa Idara ya Sheria.

Chini ya uongozi wa Kenneth Starr, uchunguzi huo ulijumuisha mradi wa nyumba za kukodisha uliopanuliwa Januari mwaka 1998 hadi kashfa ya kimapenzi ya rais na mfanyakazi wa muda wa Ikulu ya Marekani Monica Lewinsky.

Kama sehemu ya kesi tofauti dhidi ya rais - unyanyasaji wa kingono wa Paula Jones - Bw. Clinton aliulizwa kuhusu uhusiano wake na Bi Lewinsky. Baada ya kula kiapo mwezi Januari 17, Bw. Clinton alikana kuwa na uhusiano na mfanyakazi huyo wa zamani wa Ikulu ya White House.

Chanzo cha picha, VINCE BUCCI/AFP via Getty Images

Maelezo ya picha,

Monica Lewinsky alikubali kuchunguzwa na baraza maalum la haki la kumchunguza Bill Clinton

Siku chache baadae Bw. Clinton alijitoa kimasomaso kukanda madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi yake.

"Naomba mnisikilize," Rais Clinton aliwaambia wanahabari waliokusanyika White House. "Sikufanya ngono na mwanamke huyo, Monica Lewinsky. Sikumwambia mtu yeyote adanganye, hata mara moja, sikuwahi kufanya hivyo."

Tarehe 9 mwezi Septemba mwaka 1998, Bw. Starr aliwasilisha ripoti yake kwa bunge. Wamarekani pia walipata fursa ya kudurusu ripoti ya Starr ya kurasa 445- iliyojumuisha ushahidi wa kusisimua kutoka kwa Bi Lewinsky, ambaye alipewa kinga ya kutoshtakiwa na baraza huru la uchunguzi ili kupata ushirikiano wake.

Chanzo cha picha, New York Times

Ripoti hiyo pia ilijumuisha mazingira 11 yanayoweza kuchangia mashtaka. Mwezi Desemba mwaka 1998, bunge la Wawakilishi lilipiga kura kwa misingi ya vyama kumshtaki Bw. Clinton kwa kufanya makosa mawili: Uongo na kuzuia bunge kutekeleza wajibu wake.

Mwezi Februari mwaka huo, Bw. Clinton aliondolewa makosa na bunge la Seneti lililokuwa likidhibitiwa na chama cha Republican..

Matokeo yalikuwa nini?

Mwaka huo ambao nchi iligubikwa na kashfa ya kimapenzi kati ya Lewinsky-Clinton, rais aliuliza wito wa kumtaka ajiuzulu.

Ni wakati huo, mwisho wa mwezi Januari mwaka 1998, ambapo Bw. Clinton aliongoza katika kura ya maoni kuhusu umaarufu wake.

Kura ya maoni ya CNN, Gallup zilibaini kuwa asilimia 67 ya Wamarekani waliidhinisha kuwa na imani na rais.

Mwisho wake, wanasiasa pekee waliyopoteza kazi kutokana na mzozo wa mashataka dhidi yao ni wa Republican.

Bw. Clinton aliondoka madarakani mwezi Januari mwaka 2001 na uungwaji mkono wa asilimia 65 - idadi ambayo ni ya juu zaidi kuliko watangulizi wake ndani ya nusu karne.

Lakini chama chake kilishindwa na katika kinyang'anyiro cha kuingia Ikulu ya Marekani wakati George W Bush alipomshinda Al Gore baada ya kura za Florida kuhesabiwa tena.

Uongozi wake ulikuwa vipi?

Inategemea yule utakayemuuliza lakini kashfa ya Monica Lewinsky itasalia jambo la kwanza linalokuja katika mawazo ya watu wengi ukiulizia uongozi wa Clinton. Mashtaka yaliyofuata? hayakuwa hivyo.

Uungwaji mkono wake wa hali ya juu wakati wa mchakato uchunguzi dhidi yake unaashiria kuwa umaarufu wake haukuathiriwa na mashtaka hayo ikilinganishwa na marais wawili waliyokabiliwa na hali kama hiyo.