Korea Kaskazini yazindua kombora jipya 'linaloweza kurushwa kutoka kwa manowari

Kombora hilo lilizinduiwa katika gwaride la kijeshi baada ya mkutano wa kisiasa na usio wa kawaida

Chanzo cha picha, KCNA

Maelezo ya picha,

Kombora hilo lilizinduiwa katika gwaride la kijeshi baada ya mkutano wa kisiasa na usio wa kawaida

Taifa la Korea Kaskazini limezindua kombora jipya la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka kwa manowari ambalo vyombo vya habari vya vya taifa hilo vimelielezea kuwa kama 'kombora lenye uwezo mkubwa duniani'.

Makombora kadhaa ya aina hiyo yalioneshwa katika gwaride la kijeshi lililosimamiwa na rais Kim Jong un, viliripoti vyombo vya vya habari vya taifa hilo.

Hatua hiyo inajiri kufuatia mkutano wa kisiasa usio wa kawaida ambapo bwana Kim aliitaja Marekani kama 'adui yake mkubwa zaidi'.

Onesho hilo la uwezo wa kijeshi linajiri siku chache kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden kuwa rais.

Picha zilizotolewa na vyombo vya habari vya Korea Kaskazini zilionesha makombora manne makubwa yenye rangi nyeusi na nyeupe yakiendeshwa na kupitishwa mbele ya rais huyo huku kundi kubwa la watu likipunga mkono.

Wachambuzi wanasema kwamba ni kombora ambalo lilikuwa limefichwa.

Mwaka Mpya kombora jipya la Pukguksong,"Mtaalamu wa Korea kazkazini Ankit Panda, akitumia jina la kombora jipya linaloweza kurushwa kutoka kwa (SLBMs).

Akiwa amevalia koti na kofia, bwana Kim amepigwa picha akitabasamu na kupunga mkono huku akitazama onesho hilo katika bustani ya Kim Il Sung Square iliopo Pyongyang ambalo pia lilishirikisha wanajeshi wa vitengo mbali mbali, silaha na mizinga.

Chanzo cha picha, KCNA

Maelezo ya picha,

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisimamia onesho hilo la uwezo wa kijeshi

''Kombora hilo lenye uwezo mkubwa duniani , manuwari inayoweza kurusha kombora la masafa marefu ziliingia katika bustani hiyo zikifuatana , likionesha kwa kishindo kikubwa uwezo wa jeshi la taifa hilo'', kilisema chombo cha habari cha Korean Central News Agency said.