Kuapishwa kwa Joe Biden: Safari ya miaka minne ya Trump madarakani

Umati wa watu katika sherehe za uapisho mwaka 2017

Chanzo cha picha, Reuters

Wakati Donald Trump akielekea mwishoni mwa urais wake, tumeweka pamoja taarifa kwa picha kutoka miaka yake minne ya uongozi.

Umati unaonekana kukusanyika kwenye hafla ya kuapishwa kwa Bw Trump mnamo tarehe 20 Januari 2017.

Siku chache tu baadaye, rais mpya alishutumu vyombo vya habari kwa kusema uongo kuhusu mahudhurio. Alisemekana alikuwa na hasira kwamba picha zilionekana kuonesha umati wa watu ulikuwa mdogo kuliko uzinduzi wa kwanza wa Barack Obama mnamo 2009.

Msemaji wa Ikulu Sean Spicer aliwaambia wanahabari kuwa "ilikuwa hadhira kubwa kuwahi ktokea katika kipindi cha uapisho''.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wafuasi wa mrengo wa kulia na wazungu walishiriki katika mkutano wa kuwasha mwenge kupitia Charlottesville, Virginia, mnamo mwezi Agosti 2017.

Siku iliyofuata mwanamke aliuawa na wengine 19 walijeruhiwa wakati gari lilipopita kati kati ya umati wa waandamanaji jijini.

Rais Trump alilaani vurugu hizo na kusababisha ukosoaji. Saa 48 baadaye, aliwashutumu watu wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia "KKK, Wanazi-mamboleo.

Joe Biden amesema ni namna ambavyo rais alivyoshughulikia tukio hilo ndiko kulikosababisha kuchukua uamuzi wa kuwania nafasi ya urais

Chanzo cha picha, EPA

Mahudhurio ya Bw Trump kwenye mkutano wa G7 huko Canada mnamo Juni 2018 hayakuanza vizuri, wakati kabla ya mkutano huo, rais alitangaza ushuru wa kuagiza chuma na aluminium kutoka nchi za Umoja wa Ulaya, Mexico na Canada.

Picha nyingine kutoka kwenye mkutano zilionesha uhusiano wa kirafiki zaidi kati ya viongozi - lakini picha hii kwa wengi ilionesha mvutano katika mkutano huo.

Bwana Trump aliondoka kwenye mkutano huo mbele ya viongozi wengine na kudai kwamba Marekani ilikuwa "kama benki ambayo kila mtu anapora".

Chanzo cha picha, Reuters

Mke wa Rais Melania Trump alipigwa picha akiwa amevaa koti mnamo Juni 2018 ambalo liliandikwa nyuma maneno haya "Kwa kweli sijali,wewe je!" alilolivaa wakati wa safari ya kituo cha kizuizini cha watoto wahamiaji.

Kulikuwa na uvumi kuhusu ujumbe gani Bi Trump alikusudia kutuma kwa kuvaa koti kwenye safari hiyo, na kuvaliwa wakati ambao rais alikuwa akikosolewa kwa sera yake ya kutenganisha watoto na wazazi wao mpakani.

Mke wa Rais baadaye alikiri ulikuwa ujumbe "kwa watu wa vyombo vya habari vya mrengo wa kushoto ambao wananikosoa. Ninataka kuwaonesha kuwa sijali. Unaweza kukosoa chochote unachotaka kusema. Lakini haitanifanya niache kufanya kile ninachohisi ni sawa ".

Chanzo cha picha, Getty Images

Bwana Trump alitaka maelewano katika siasa wakati wa hotuba yake kwa taifa mnamo Februari 2019 lakini Nancy Pelosi alipigwa picha akitoa kile ambacho wengi waliona kama makofi ya kejeli.

Alivunja itifaki kwa kutosubiri utangulizi wa kimila kutoka kwa Spika wa Bunge kabla ya kuanza hotuba yake.

Picha hiyo, inayoitwa "makofi ya Pelosi" ilienea haraka na ilionekana kuonesha uhasama wa kisiasa kati ya wawili hao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Bwana Trump anaingia upande wa Kaskazini wa mipaka ya kijeshi inayogawanya Korea Kaskazini na Kusini mnamo Juni 2019. Kwa kufanya hivyo, alikua rais wa kwanza wa Marekani kuvuka mpaka huo.

Uamuzi wake wa kukutana na Kim Jong-un bila masharti ya awali uliushangaza ulimwengu.

Licha ya ongezeko la msuguano katika uhusiano, hatua kidogo ilipigwa kuhusu mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kim Kardashian West azungumza katika hafla ya Ikulu kuhusu mageuzi ya magereza mnamo mwezi Juni mwaka 2019.

Mnamo mwaka 2018, mwanaharakati mashuhuri aliushawishi utawala wa Trump kwa niaba ya bibi aliyefungwa kifungo cha maisha. Alice Johnson baadaye alipewa msamaha na Bw Trump.

Rais Trump tayari ametoa msamaha kwa watu 94 na kuna uvumi anaweza kuwasamehe wengine 100 kabla hajaondoka madarakani.

Chanzo cha picha, Reuters

Bwana Trump anashikilia biblia mbele ya Kanisa la Mtakatifu Yohana, pembeni tu mwa barabara kutoka Ikulu mnamo Juni 2020.

Waandamanaji wenye amani wanaopinga ubaguzi wa rangi walikuwa wameondolewa kwenye uwanja wa karibu wa Lafayette na mabomu ya kuwasha ili rais na msafara wake waweze kwenda kanisani.

Matendo yake yalisababisha mshtuko na hasira kutoka kwa viongozi wengi wa dini, ambao walimshtaki kwa kutumia dini kwa madhumuni ya kisiasa.

Chanzo cha picha, AFP

Familia ya Trump inashuhudia wakati Donald Trump akiwa kwenye mjadala na Joe Biden, mjadala wao wa kwanza wa urais huko Cleveland, Ohio, mnamo 29 Septemba 2020.

Walivunja sheria za mjadala kuhusu watazamaji wote kuvaa barakoa - na kusababisha ukosoaji uliomlenga baba yao.

Siku chache baada ya mjadala, rais alikutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Alikaa siku tatu hospitalini akipata matibabu kabla ya kurudi Ikulu na kutangaza anajisikia "vizuri" na kuwasihi wengine wasiogope virusi.

Chanzo cha picha, Reuters

Umati wa wafuasi wa Trump wanavamia Capitol la Marekani huko DC.

Ilifuata hotuba ya dakika 70 na rais ambapo aliwahimiza kuandamana kwenye Bunge ambapo wanasiasa walikuwa wakikutana kuthibitisha ushindi wa Joe Biden wa chama cha Democrat. Umati huo ulivamia jengo la Capitol na kujaribu kuingia kwenye vyumba ambavyo wabunge walikuwa wamejificha.

Watu watano, pamoja na afisa wa polisi, waliuawa.

Bwana Trump alipigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, lakini anakanusha kuwa alichochea umati wa watu kufanya mashambulizi.