Kuapishwa kwa Biden: Biden aanza kazi kwa kutengua sera za Trump

US President Joe Biden signs documents after being sworn-in

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Biden akisaini haraka amri za rais juu ya virusi vya corona, mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa usawa

Rais mpya wa Marekani Joe Biden ameanza kutengua sera kadhaa muhimu za Donald Trump, saa chache baada ya kuapishwa.

Rais Biden tayari amesaini maagizo ya watendaji 15 yanayolenga kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Amri nyingine ni kubadilisha msimamo wa utawala wa Trump juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na uhamiaji.

Biden ameanza kufanya kazi katika Ofisi ya Oval baada ya kuapishwa mapema Jumatano kama rais wa 46 wa Marekani.

Kuapishwa kwa Biden kulikua na utofauti na nyakati nyingine yoyote kutokana na vizuizi vya maambukizi ya corona, na wachache walikuwepo kushuhudia viapo na sherehe.

Maelezo ya picha,

Demokrasia imeshinda," Rais Biden alisema baada ya kuapishwa kuchukua mamlaka na Jaji Mkuu John Roberts

Donald Trump - ambaye bado hajakubali rasmi urais kwa Biden alikataa kuhudhuria hafla badala yake alikua na sherehe zake binafsi katika makazi yake.

Biden ameapa kuwa Rais wa Wamarekani wote sambamba na kuwa Rais anayefuata sheria ya katika ya nchi huku akizitaka jamii za kimataifa kuitegemea Marekani mpya.

Watangulizi wake watatu waliudhuria shughuli ya kuapishwa kwake: Barack Obama - ambaye bwana Biden alikuwa makamu wake wa rais kwa miaka nane - Bill Clinton na George W Bush, pamoja na aliyekuwa makamu wa rais wa Trump, Mike Pence.

Maelezo ya picha,

Kamala Harris aliapishwa na Jaji wa Mahakama ya Sonia Sotomayor

Kamala Harris ameapishwa kama makamu rais wa bwana Biden. Ni mwanamke wa kwanza - mweusi kupata wadhifa huo nchini Marekani.

Ulinzi ulikuwa umeimarishwa zaidi katika shughuli hiyo katika jengo la Capitol baada ya wafuasi wa Trump kuvamia Januari 6.

Bwana Biden na mke wake Bi.Jill Biden, pamoja na Bi. Harris na mume wake Doug Emhoff, walitembea kutoka katika makutano ya Pennsylvania mpaka Ikulu ya Marekani, wakiwasalimia marafiki na wafuasi wao.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Bwana Biden na mke wake Bi.Jill Biden, pamoja na Bi. Harris na mume wake Doug Emhoff, walitembea kutoka katika makutano ya Pennsylvania mpaka Ikulu ya Marekani

Katika sherehe za uapisho huo zilijumuisha maonesho ya muziki ; Lady Gaga - aliimba wimbo wa taifa - pamoja na Jennifer Lopez na Garth Brooks.

Amanda Gorman, ni mwanamashairi mdogo zaidi alighani shairi lake katika shughuli hiyo.

Katika tamasha la jioni katika mji wa kumbukumbu wa Lincoln ulitumbuizwa na Tom Hanks pamoja na Bruce Springsteen, John Legend, Jon Bon Jovi, Justin Timberlake, na Demi Lovato.

Ni amri zipi Biden amesaini?

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Amri mpya ni pamoja na mkakati dhidi ya kukabiliana na corona, mabadiliko ya tabua nchi na usawa

Rais Biden "atachukua hatua - na si kubadili sera peke yake ya uharibifu uliofanywa na utawala wa Trump- lakini pia kuanza kuliendeleza taifa," taarifa inayofafanua amri hiyo inaeleza.

Mfululizo wa hatua zitakazotekelezwa kukabiliana na janga la virusi vya corona ambalo limesababisha zaidi ya vifo 400,000 nchini Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bwana Biden anataka Wamarekani milioni 100 kupewa chanjo ndani ya siku 100 za mwanzo wa madaraka yake

Kutakuwa na amri ya uvaaji wa barakoa na kukaa kwa umbali katiika maeneo yote ya umma.

Ofisi mpya itaweka mkakati wa kukabiliana na janga hilo la corona - na kuanzia na hatua ya utawala wa Trump - kuiondoa Marekani katika Shirika la Afya (WHO).

Bomba lililofadhiliwa kibinafsi - linalokadiriwa kugharimu karibu dola bilioni 8, itakayobeba malighafi za mafuta kutoka Alberta, nchini Canada, mpaka Nebraska.

Barack Obama alipiga kura ya kuidhinisha muswada wa ujenzi wa bomba mnamo 2015 lakini uamuzi huo ulibatilishwa na Rais Trump.

Kuhusu uhamiaji Bw Biden amebatilisha tangazo la dharura la utawala wa Trump ambalo lilisaidia kufadhili ujenzi wa ukuta kando ya mpaka wa Mexico na pia kumaliza marufuku ya kusafiri kwa nchi nyingi za Waislamu.

Amri zingine zinahusu usawa wa kijinsia.