Je wakati umefika kwa serikali za Afrika kuruhusu biashara ya sarafu za mauzo ya mtandaoni?

Je wakati umefika kwa serikali za Afrika kuruhusu biashara ya sarafu za mauzo ya mtandaoni?

Kampuni ya magari ya bilionea na tajiri wa kwanza duniani Elon Musk Tesla imesema kuwa ilinunua takriban sarafu bilioni 1.5 za mauzo ya mtandaoni al maarufu Bitcoin mwezi Januari na inatarajia kuanza kukubali sarafu hizo kama malipo katika siku zijazo.

Taarifa hiyo ilisababisha bei ya sarafu ya Bitcoin kupanda kwa 17% hadi $44,220, kiwango ambacho ni cha juu kuwahi kurekodiwa. Hata hivyo Licha ya faida zake, serikali nyingi za Afrika zimekua zikizuia biashara ya Bitcoin, kwa kile kilichotajwa kuwa ni vigumu kudhibitiwa. Kutaka kufahamu biashara hii inafanyikaje? Na je wakati umefika kwa mataifa ya Afrika kuruhusu watu wake kufanya biashara hii?...Dinah Gahamanyi amezungumza na mchambuzi wa masuala ya uchumi nchini Tanzania Bw Walter Nguma.