Washawishi walemavu wanaoacha historia kwenye mitandao

Tess Daly anasema hapendi kutumia neno ''mshawishi wa kimtandao'', licha ya kuwa mmoja wao.

Chanzo cha picha, Tessy Daily

Maelezo ya picha,

Tess Daly anasema hapendi kutumia neno ''mshawishi wa kimtandao'', licha ya kuwa mmoja wao.

"Lazima ufanye kazi kwa bidi ili kuwa wewe uanetaka kuwa mkweli na kuamini nembo unayoinadi."

Maneno ya ushauri kutoka kwa mshawishi mwenye ulemavu mwenye umri wa miaka 32 Tess Daly kutoka Sheffield, ambaye hutumia wafuasi wake zaidi ya 200,000-kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kunadi mafunzo yake ya vipodozi na pia nembo za urembo.

Tess ambaye ni mlemavu anatumia kiti cha umeme, na ambaye ana ulemavu wa uti wa mgongo, amefanya kazi kama afisa masoko katika mitandao ya kijamii akinadi bidhaa za makampuni utrembo kama Boohoo Pretty Little Thing, pamoja nembo nyingine za vipodozi.

Anafurahia neno "mshawishi wa mitandao ya kijamii ", lakini anasema anatamani kungekuwa na watu wengi kama yeye wakati alipokuwa akikua.

"Watu wengi sana wenye ulemavu wameniambia kuwa nimewapa ujasiri wa kujiamini, sio tu kwa kuukubali ulemavu wao, lakini pia kuweza kujipodoa wenyewe,"anasema.

Tess ni mmoja washawishi walemavu ambao idadi yao inaendelea kuongezeka wanaofanya kazi katika kampuni ya Martyn Sibley na shirika lake la masoko ya kimtandao linalofahamika kama Purple Goat, ambalo lilizinduliwa mwanzoni mwa maagizo ya kukaa nyumbani (lockdown) mwaka jana.

Chanzo cha picha, TESSY DALY

Maelezo ya picha,

Tess Daly anasema anapenda neno "mshawishi wa mitandao ya kijamii", licha ya kuwa wa aina yake

Tess Daly anasema anapenda neno "mshawishi wa mitandao ya kijamii", licha ya kuwa wa aina yake

Martyn, ambaye alizaliwa na ulemavu, alianza shirika lake kama sehemu ya mpango wake wa kujumuisha dunia nzima

"Ninaamini kwa kusaidia biashara kubwa kupata faida zaidi kupitia wanunuzi wenye ulemavu kupitia walemavu wenye ushawishi, tutaweza kujumuisha watu wote haraka," alisema. "Kwa njia hii kila mtu ananufaika ."

Purple Goat imefanya kazi na watu wenye ushawishi zaidi ya 75 hadi sasa, lakini Martyn yuko makini kusema kuwa kuwa sio shirika la vipaji ambalo lina watu binafsi liliowapanga kufanya kazi nao.

"Tunafanya kazi kwa ajili ya wateja na kutafuta washawishi wanaofaa kwa kila anaeleza.

Takriban watu milioni 14.1 nchini Uingereza wana aina fulani ya ulemavu, na idadi hiyo ya watu inakuwa ni kubwa inapokuja katika soko la biashara.

Chanzo cha picha, MARTYN SIBLEY

Maelezo ya picha,

Martyn Sibley anaongoza harakati za ujumuishaji wa watu wa tabaka mbali mbali

Hii ilikuwa ni sababu kubwa iliyomfanya Martyn afungue kampuni ya Purple Goat. Anadhani kuwa dunia ya masoko na utangazaji wa biashara sasa inatambua zaidi jamii, na iko tayari kwa mabadiliko.

" Ninaamini kuwa kwa sehemu ni njia ya maoni ya umma ambayo yameboreshwa kuhusiana na ujumuishwaji wa watu mbali mbali ," anasema. "Nembo zimekuwa na hofu ya kufany amakosa katika kuwazungumzia walemavu, lakini sasa wanahofu ya kuitwa kwa kutofanya chochote."

Tess ameshuhudia kuongezeka kwa idadi ya watu wenye ulemavu kuajiriwa na kuwa maarufu katika mitandao ya kijamii . Hadi mwaka jana, lilikuwa ni jambo alilofanya kama kazi ya ziada, lakini kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, alichukua jukumu kamili la kuwa mshawishi katika mitandao ya kijamii na sasa nafanya kazi na wakala kumpunguzia kazi nyingi.

Haikuwa rahisi kama watu wanavyoweza kufikiria, anasema. "Huwezi tu kuamka siku moja na kuamua unataka kuwa mshawishi wa mitandao ya kijamii ."

'Kudai kuonekana'

Mwaka jana nembo ya viatu vya thamani ya mjini London- Kurt Geiger ilianza kufanya kazi na mwanamitindo na mshawishi mlemavu ambaye hana baadhi ya viungo wa Ireland Kaskazini Bernadette Hagans.

Mtendaji mkuu wa kampuni, Neil Clifford, anafikiria kwamba kuongezeka kwa washawishi walemavu kumetokana na mabadiliko ya umma.

"Maendeleo ya mitandao ya kijamii yamefanya wale ambao awali walikuwa hawawakilishwi machoni mwa umma kupaza sauti na kwa na sasa hivi ndio wanataka kuonekana hasa," alisema.

Kujitokeza kwa makampuni makubwa makubwa na kuonesha kuunga mkono hatua hii, ni jambo ambalo wanahisi kuwa jukumu lao ili kuepuka ukosaji, amesema.

Chanzo cha picha, PIPPA STACEY

Maelezo ya picha,

Ujumbe wa Pippa katika mitandao ya kijamii kuhusu ugonjwa "usiojulikana"

Ameongeza kuwa: "Washawishi walemavu wanahitaji kuwa na uhusiano na kile wanachokihamasisha ili kuwa na maana. Kuwa na msemaji mwenye ulemavu pia kunaongeza kiwango cha uaminifu katika kampuni."

Caroline Casey ni muasisi wa kampuni ya Valuable 500, ambayo kote duniani inahamasisha makampuni kupigania mahitaji ya watu walemavu katika kiwango cha bodi.

Chanzo cha picha, Caroline Casey

Maelezo ya picha,

Caroline Casey ni muasisi wa kampuni ya Valuable 500

Bernadette Hagans, aliyefanyakazi na Kurt Geiger, pamoja na Ellie Goldstein, mwanamitindo aliyezaliwa na tatizo la kasoro katika vinasaba yaani 'Down syndrome', mwaka jana picha yake ilikuwa iliyopendwa zaidi katika mtandao wa Instagram wa kampuni ya vipodozi ya Gucci.

Laura anasema wameshuhudia ongezeko la makampuni makubwa makubwa yanayotumia washawishi walemavu kufikia walengwa mbalimbali katika biashara zao.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya sauti,

Ulemavu wa macho wabadilisha maisha yangu