Virusi vya corona: Marekani iko tayari kufanya kazi bega kwa bega na Tanzania kuishinda Covid-19

Unalozi wa Marekani

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema kuwa Marekani iko tayari kushirikiana na Tanzania kuzuia kusambaa kwa COVID-19, na kuishinda.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao rasmi wa Ubalozi huo, Balozi wa Marekani nchini humo Dionald Wright amesema '' Ninataka kuzungumzia kuhusu Covid-19 na jinsi tunavyoweza kushirikiana kwa pamoja kuzuia kusambaa kwake na kutusaidia sisi sote kukaa salama''

Haya yanajiri baada ya Marekani kutoa tanagazo juma lililopita ikiwatahadharisha watu dhidi ya kusafiri nchini Tanzania kutokana na corona.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Hivi karibuni Rais Magufuli ashiria kubadili msimamo wake kuhusu ugonjwa wa Covid- 19

Hata hivyo hivi karibuni Tanzania imeonyesha kuimarisha juhudi za kukabiliana na virusi vya corona huku rais Magufuli akisema serikali yake haijamzuia mtu yeyote kuvaa barakoa.

Tamko hilo liliashiria kuwa Rais Magufuli amebadili msimamo wake kuhusu ugonjwa wa Covid 19.

Rais ailitoa wito kwa wananchi wenzake kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya, akisisitiza kwamba serikali yake haijamzuia mtu yeyote kuvalia barakoa...Magufuli: 'Hatujazuia matumizi ya barakoa'

Tangu wakati huo viongozi na baadhi ya watu wamekua wakionekana kuchukua tahadhari hususan uvaaji wa barakoa na unawaji wa mikono.

Waziri anayehusika na masuala ya afya nchini Tanzania Dkt Doroth Gwajima Ijumaa kupitia tangazo lililotumwa mwenye mtanda wa Twitter wa Wizara ya anayoingoza aliwaomba viongozi na wananchi kushirikiana kuongeza kasi zaidi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Dkt Gwajima amekuwa akihimiza matumizi ya dawa za asili katika kukabiliana na magonjwa ya mfumo wa upumuaji

Balozi wa Marekani amesema nini?

Katika taarifa yake iliyoanza kwa kujitambulisha na kutoa salamu, '' Habari zenu'', Balozi Wright amesema tangu Covid-19 ilipoanza karibu watu milioni mbili na nusu wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Akitoa athari za ugonjwa huo kwa nchi yake Balozi Wright amesema: ''Tuliwapoteza zaidi ya raia wenzetu 500,000. Na kuyafanya mambu kuwa magumu, aina mpya ya virusi vya corona imesababisha wimbi jingine la maambukizi kote duniani, ikiwemo Afrika . Imekuwa wazi kuwa aina ya virusi pia imewasili Tanzania'', amesema Balozi Donald Wright.

Katika taarifa hiyo yabalozi wa Marekani nchini Tanzania ameendelea kusema kuwa ametiwa moyo na taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kupambana na virusi vya corona:

''Nimetiwa moyo na taarifa za hivi karibuni kutoka kwa Wizara ya Afya kukubali COVID-19 kama kipaumbele cha afya ya umma nchini Tanzania na kuwataka raia kuchukua tahadhari za kimsingi : kama vile kuepuka umati, kuvaa barakoa, na kukaa mbali. Huu ni usahuri mzuri na ninamuomba kila mmoja aufuate, anasema.

Zaidi ya kutekeleza tahadhari za dharura za kimsingi kuzuia kusambaa kwa Covid-19, Balozi Wright ameishauri Tanzania kutumia walau mbinu nyingine mbili muhimu katika kudhibiti janga la corona ya kwanza ikiwa ni kukusanya na kuripoti taarifa kuhusu upimaji na visa.

''Kwanza ili kujua kama hatua ulizochukua zinaathari ulizozilenga, ni muhimu kukusanya na kuripoti taarifa kuhusu upimaji na visa'', alisema katika taarifa hiyo.

Mbinu ya pili ni chanjo:''Kama Waziri wetu wa mpya wa mambo ya nje Tony Blinken alivyosema "hadi kila mtu atakapokuwa amechanjwa, hakuna yeyote ambaye ni salama kabisa."

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Balozi wa Marekani nchini Tanzania ameitolea wito serikali ya Tanzania kuchukua tahadhari za kimsingi za kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya Covid -19

Akitoa mfano wa kampeni ya chanjo inayoendelea nchini mwake alisema '' Ninaitolea wito Serikali ya Tanzania kuwakusanya wataalamu wake wa afya na kutathmini ushahidi kuhusu chanjo.

Unaweza pia kusoma:

Amesema Marekani kama muhisani mkubwa zaidi wa afya na msaada wa kibinadamu inaendelea kuongoza juhudi za dunia za kukabiliana na janga la Covid-19 , ikichangia zaidi ya dola bilioni 1.5 kwa ajili juhudi za kupunguza COVID-19 kote duniani na iliahidi dola bilioni 4 kwa ajili ya kuharakisha usambazaji wa chanjo.

'' Hapa nchini Tanzania, tulijitolea kutoka dola milioni 16.4 kwa ajili ya kupambana na janga la Covid-19 tangu kisa cha mtu wa kwanza kupatikana na virusi mwezi 2020. Marekani iko tayari kuongeza juhudi zetu na tuko tayari kujitolea kufanya kazi bega kwa began a Tanzania kuishinda Covid-19', amesema.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Hatudharau chanjo ya corona Tanzania, tunasubiri majaribio zaidi kabla kuitumia