Mahojiano ya Oprah kwa Meghan na Harry: Fahamu umuhimu wa Binti mfalme Diana

Chanzo cha picha, Getty Images
Meghan Markle na Binti mfalme Diana
Mahojiano ya Oprah Winfrey na Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan Markle yaliyogonga vichwa vyaa habari yalikuwa muhimu kwasababu kadhaa.
Moja wapo ilikuwa ni mara ambazo marehemu mama yake Mwanamfalme Harry, Princess Diana alizitaja.
Meghan Markle alisema alizungumza na mmoja wa rafiki za bintimfalme Diana kuhusu kujiunga na familia yaa kifalme, "kwasababu ... nani mwingine tena angeelewa ndani kuko vipi?"
Wanawake hao wawili walijiunga na familia ya Windsor na kuanza kuwa na nguvu kutoka siku ya kwanza, hivyobasi ulinganisho wao hauwezi kuepukika.
Mwanamfalme Harry alisema katika mahojiano kwamba alihofia historia huenda "ikajirudia" kabla ya yeye na Meghan kuacha majukumu yao ya kifalme.
Chanzo cha picha, Getty Images
Bintimfalme Diana anadaiwa kufuatwa na waandishi wa habari kila alipokwenda
Pande mbili za vyombo vya habari
Princess Diana alikuwa anachukuliwa mmoja kati ya wanawake maarufu duniani na kila mara taarifa zake zilikuwa zinaandikwa kwenye magazeti, kuhusiana na kazi yake ya kusaidia maskini na maisha yake binafsi.
"Diana alikuwa mfano wa kuigwa. Alitambuliwa kimataifa ," mwandishi na mtaalam katika nyumba ya Kifalme Katie Nicholl ameelezea BBC Radio 1 Newsbeat.
Lakini alivyokuwa anaangaziwa na vyombo vya habari haikuwa kwa mtazamo mzuri kila wakati.
"Diana alikosolewa na vyombo vya habari. Alikuwa mtu maarufu kabisa duniani lakini wanahabari wapekuzi walikuwa wakimuandama kila sehemu ya maisha ya Mwanamfalme William na Harry," Nicholl amesema.
Mwanahabari James Brookes anakubaliana na hilo.
"Wakati mwingine alikuwa na uhusiano mzuri na vyombo vya habari na walikuwa wanamuunga mkono. Wakati mwingine alilalamika kwama vyombo vya habari vilipenda kuingilia mambo ya watu. Ulikuwa uhusiano mchanganyiko," aliongeza.
Diana alikuwa akifanya mahojiano binafsi ambayo yalipelekea wengine kufikiria kwamba alikuwa anatafuta umaarufu na kuvutia nadhari.
Kwa upande wake, Meghan alifunga blogi yake binafsi alipojiunga na familia ya kifalme na mahojiano yake mengi kabla aliyofanya na Oprah Winfrey, yalikuwa ni kuhusu kazi za kusaidia maskini.
'Watu wanahoji maisha ya faragha waliodai ndio wanayotaka'
Januari 2020, wanandoa hao walisema kwamba wanaacha kutekeleza majukumu ya kifalme baada ya kuangaziwa sana magazetini.
Wakahamia Canada na baadaye California. Na siku za hivi karibuni ilitangazwa kwamba hawatarejea tena Uingereza kama wanaotekeleza majukumu yao ya familia ya kifalme.
Nicholl amesema kuwa mahojiano na Oprah "yameweka wazi mengi kuhusu maisha yao ya sasa hivi kuliko walivyokuwa Uingereza."
Tangu walipoacha kutekeleza majukumu ya kifalme, wanandoa hao wamezindua podcast chini ya makubaliano na mtandao wa urushaji filamu wa Neflix na kufanya mahojiano na James Corden na Oprah Winfrey.
"Watu wanahoji kwamba wawili hao walihama Uingereza kwasababu walitaka maisha yenye faragha lakini 'Kwanini wanazungumza na James Corden na Oprah Winfrey na kutoa mengi hadharani kuhusu kijana wao?'" Nicholl ameongeza.
"Wazo la kuondoka Uingereza na kuangaziwa sana na vyombo vya habari linaonekana kuwa lisilo na ukweli na watu wengi ambao sasa hivi wanamuona sana Harry na Meghan waliokuwa hawaonekani wakiwa Uingereza."
Harry alimwambia Oprah kwamba makubaliano ya Netflix na Spotify hayakuwa sehemu ya makubaliano lakini familia yake "ilikuwa imekatisha ufadhili wa kifedha" mapema mwaka 2020.
Kifo cha Princess Diana na paparazzi
Chanzo cha picha, Getty Images
Kila mara alipokwemda alikuwa aikifutwa na waandishi wengi wa habari
"Kila alipokwenda (Diana), kulikuwa na wanahabari wengi na wapiga picha wakiangazia kila hatua anayopiga," anakumbuka James Brookes.
Brookes anaamini kuwa maoni ya Mwanamfalme Harry kuhusu vyombo vya habari aliangazia tangu wakati wa kifo cha Princess Diana.
"Mengi ya Harry na William kuhusu mtazamo wa vyombo vya habari ni hasi, machoni mwa Harry, mama yake alinyanyaswa na paparazzi," amesema.
Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamfalme Harry anaasema kwamba wanahabari wanamnyanyasa Meghan Markle
Princess Diana aliaga dunia katika ajali ya gari kwenye handaki nchini Paris Agosti 31, 1997. Mwanamfalme Harry wakati huo alikuwa na miaka 12 wakati huo.
Dereva, Henri Paul, amekuwa akinywa pombe na gari yao ilikuwa inafuatiliwa na wapiga picha wasiri waliokuwa kwenye pikipiki.
Baadaye, uchunguzi ulibaini kwamba Diana alifariki dunia kwasababu ya "uzembe" wa dereva na paparazzi.
Mwaka 2017 katika makala iliyoandaliwa na BBC, Mwanamfalme Harry alizungumza kuhusu kifo cha mama yake na mchango wa wanahabari katika hilo.
"Nafikiri moja ya matukio magumu kuamini ni ukweli wa kwamba watu waliokuwa wanamfukuza hadi akatumbukia kwenye mtaro ndio haohao waliompiga picha wakati anaaga dunia akiwa kitu cha nyuma cha gari," alisema.
Kuangaziwa na vyombo habari kwa mtazamo hasi
Licha ya Mwanamfalme Harry kusema mwezi Oktoba mwaka 2019, Katie Nicholl anaamini kwamba "Meghan hafuatiliwi au kunyanyaswa na paparazzi kama ilivyokuwa kwa Diana."
Hata hivyo, anafikiri pia Mwanamfalme amechoshwa na simulizi zinazomkosoa Meghan.
"Anavamia wanahabari ambao anaamini kuwa kila saa wanazungumza mabaya kumhusu mke wake," amesema.
"Kulikuwa na simulizi nyengine nyingi tu hasa kuhusu matumizi ikiwemo gharama za kuboresha nyumba yake ambazo zilisimamiwa na walipa kodi," aliongeza.
Chanzo cha picha, Getty Images
Katie anasema kwamba mwanamfalem huyo anamtetea Meghan
Pesa hizo zilikuwa takriban dola milioni 3.3 ambazo baadaye wanandoa hao walizirejesha.
Kuna wale wanaosema kwamba Meghan Markel alitaka kupata angalizo kwasababu tofauti na Princess Diana, yeye alikuwa maarufu kabla ya kuolewa na Harry.
Ingawa Nicholl anapinga hilo.
"Nafikiri hata kama alikuwa na maisha ya kifahari kabla, huwezi kulinganisha hilo na kuwa ndani ya familia ya kifalme," amesema.
"Ndio, alikuwa na hadhi ya mtu maarufu lakini hakuwa mwigizaji wa ngazi ya juu sana kama vile Angelina Jolie au Nicole Kidman. Aliwahi kusema kwamba hajawahi kuangaziwa na umma kiasi hiki," aliongeza.
Ni kweli kwamba watu wanahamu ya kujua kuhusu maisha ya Harry na Meghan lakini pia kuna mpaka wa kile kinachokubalika, mwandishi huyo anaamini.
"Kazi ya vyombo vya habari ni kuripoti kuhusu familia ya kifalme lakini lni lazima kuwe na usawa na bila upendeleo," aliongeza.