Mahojiano ya Harry na Meghan: Mwandishi wa habari aliyefukuzwa kazi baada ya kukosoa mahojiani ya Harry na Meghan asema hajuti

Piers Morgan and the Duchess of Sussex

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Morgan, asema kuna uhuru wa kujieleza, nitafurahi kufa kwa sababu hiyo"

Piers Morgan amesema kuwa hakwepi ukosaji wake wa Mwanamfalme Harry na Meghan alioutoa kwenye kipindi cha televisheni ya ITV nchini Uingereza maarufu kama-Good Morning Britain mara ya kwanza kwenda hewani baada ya kuondoka kwake.

Ilitangazwa kuwa Bw Morgan ambaye alikuwa ndiye mtangazaji wa kipindi hicho maarufu aliacha kazi ya utangazaji wa kipindi hicho baada ya kusema "hakuamini hata neno moja " alilosema Meghan katika mahojiano na Oprah Winfrey.

Akielezea kuondoka kwake, mtangazaji mwenza Susanna Reid alisema kuwa alisema kuwa hakubaliani na kauli zake, na kuongeza kuwa: "Kipindi kinaendelea."

Ofcom inapeleleza kauli zake baada ya kupokea malalamiko 41,000.

Katika ujumbe wake wa Twitter alioutuma wakati kipindi kilipokuwa kinaanza, Morgan alisema: "Jumatatu, nilisema sikumuani Meghan Markle katika mahojiano yake ya Oprah. Nimekuwa na muda wa kutathmini maoni haya, na bado nasema simuamini."

Aliongeza kuwa: "Uhuru wa kujieleza ni mlima ninafurahi kufa juu yake. Asante kwa upendo wote na chuki. Ninaondoka kuishi kwa muda na maoni yangu."

Ujumbe wake uliambatana na picha ya Winston Churchill wenye nukuu kuhusu uhuru wa kujieleza.

Jumanne, kabla ya kuondoka kwenye kipindi, Morgan aliibua malumbano baada ya mjadala na mtangazaji mwenzake Alex Beresford kuwahusu Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan.

Piers Morgan alisema nini kingine?

Akizungumza kutoka mbele ya nyumbani kwake mjini London Jumatano, mtangazaji huyo alielezea kuondoka kwake kwenye kituo cha ITV kama "faraja", akiongeza kuwa : "Nilikuwa na mazungumzo mazuri na ITV na tulikubaliana kutoafikiana ."

Alifafaniua: "Ninaamini katika uhuru wa kujieleza, ninaamini katika haki ya kuruhusiwa kuwa na maoni.

Kama watu wanataka kumuamini Meghan Markle, ni haki yao.

"Siamini karibu kila kitu kilichotoka mdomoni mwaka na ninadhani uharibufu alioufanya kwa Ufalme wa Uingereza na Malkia katika wakati ambapo Mwanamfalme Philip amelazwa hospitalini ni mkubwa na wa kudharauliwa kusema kweli.

"Kama itabidi nichukie simu yangu kwa kujieleza maoni yangu kumuhusu Meghan Markle na machungu yake aliyoyatoa kwenye mahojiano, basi na iwe hivyo."

Pia alisema kuwa: "Ninadhani ni haki kusema, ingawa watu wengi watafikiria kuwa wamenifuta mimi, ninadhani badala yake wataka tamaa wakati nitakaporejea tena ."

Ameelezea kutoonekana kwake katika televisheni kwa siku zijazo kama "kwa muda tu", akiongeza kuwa "wakati wote hufanya mazungumzo na watu " kuhusu kazi .

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alikuwa anatangaza kipindi na Susanna Reid

Nini alichokisema Susanna Reid -mtangazaji mwenza wa Morgan?

Mtangazaji mwenza wa Morgan wa muda mrefu alianza kipindi hicho cha asubuhi cha Jumatano kwa kuwafahamisha watazamaji kuhusu kuondoka kwa Morgan.

"Watu wengi watafahamu taarifa na wengi miongoni mwenu hamtajua, na itakua ni taarifa ya kushitukiza kwamba Piers Morgan hayupo pale asubuhi ," alisema.

"Sasa,Piers na mimi hatukukubaliana juu ya mambo mengi, nan a kutokubaliana kwetu huko ndiko kulikowafanya watazamaji w wengi wapende kipindi . Bila shaka ni mtu aliyesema alichokitaka, alikosoa, alitoa maoni yake, na mtangazaji aliyevuruga matangazo.

"Anawakosoaji wengi na mashabiki wengi. Utafahamu kuwa sikukubaliana naye kuhusu mahojiano ya Meghan. Yeye mwenyewe binafsi alidhihirisha kauli zake kuhusu afya ya akili katika kipindi jana.

Kulikuwa na maoni mengi kuhusu kilichosemwa, na kila mtu alisema lake.

"Lakini sasa, Piers ameamua kuondoka katika kipindi kama mtangazaji wake. Baadhi yenu mnaweza kumshangilia na wengine watamzomea.

"Amekuwa mtangazaji mwenza, Jumatatu hadi Jumatano, kwa zaidi ya miaka mitano, na wakati wa Brexit na janga na masuala mengine, amekuwa sauti ya wengi na sauti ya wengi wenu mmempinga.

"Itakuwa tofauti, lakini kipindi kinaendelea, kwahiyo tunaendelea ."

Singh aliongeza kuwa added Moghan alikuwa "mtu mwenye haiba kubwa " ana akakiri kuwa watazamaji wengi "watamkosa".

Chanzo cha picha, Ken McKay/ITV/Shutterstock

ITV inajitolea kwa afya ya akili '

Jumla ya malalamiko 41,015 yalitolewa kwa chombo cha habari kinachosimamia televisheni hiyo Ofcom ilipofika saa nane mchana Jumanne, idadi hiyo ikiwa ni kubwa ya pili ya watu waliowahi kutoa malalamiko yao katika historia ya miaka 17 ya Ofcom.

Jumanne Mkurugenzi Mkuu wa Televisheni ya ITV Dame Carolyn McCall alieleza bayana kutokubaliana na msimamo wa Morgan kwa kusema kuwa "anaamini kabisa kile ambacho Meghan [the duchess] anakisema", akiongeza kuwa Televisheni ya ITV "inajitolea kikamilifu " katika suala la afya ya akili.

Shirika la misaada ya afya ya akili-Mind, ambalo ni mshirika wa ITV katika kampuni yake ya Britain Get Talking, pia lilimkosoa Morgan, likisema "limesikitishwa "na kauli za mtangazaji huyo.

Kufuatia malalamiko yaliyojitokeza baada ta kauli hizo, Morgan alisema katika kipindi cha Jumanne kwamba alikuwa na "alikuwa na hofu kubwa kuhusu ukweli wa mengi yay ale ambayo " Meghan aliyasema, "sio jukumju langu kuhoji kama alihisi kujiua".