Marekani ndio wauzaji wakuu wa silaha duniani na soko lao linazidi kuongezeka

Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani imeongeza soko lake la uuzaji wa silaha kwa nchi zingine hadi asilimia 37 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kulingana na Taasisi ya Utafiti yenye makao yake nchini Sweden.
Kuongezeka kwa kiwango cha uuzaji silaha kwa Marekani, Ufaransa na Ujerumani kulisawazishwa na kupungua kwa uuzaji wa silaha kwa nchi za Urusi na China.
Silaha zinazouzwa na zinazonunuliwa bado idadi yake ni ya juu tangu kumalizika kwa vita baridi, ingawa hili linaweza kubadilika kutokana na athari za janga la corona.
Ukuaji wa soko la ununuaji wa silaha kulishuhudiwa Mashariki ya Kati.
"Ni mapema mno kusema ikiwa kipindi cha kuongezeka kwa haraka kwa uuzaji wa silaha katika kipindi cha miongo miwili iliyopita kimepita," amesema Pieter Wezeman, mtafiti mwandamizi katika Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti kuhusu Amani Stockholm ambaye amekusanya data.
"Athari ya kiuchumi ya ugonjwa wa Covid-19 huenda ikafanya baadhi ya nchi zikatathmini tena ununuaji wa silaha miaka ijayo.
"Hata hivyo, kipindi kama hicho, hata wakati ambapo janga la corona lilikuwa limefikia kilele chake mwaka 2020, nchi kadhaa zilitia saini mikataba mikubwa ya kununua silaha."
Uuzaji wa silaha kimataifa bado kuliendelea bila kutetereka kati ya mwaka 2016 na 2020 ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita, Sipri alisema.
Karibu nusu ya asilimia 47 ya silaha ziliuzwa eneo la Mashariki ya Kati, huku Saudi Arabia ikinunua takriban asilimia 24 ya jumla ya silaha za Marekani.
Marekani sasa hivi inauza silaha kwa mataifa 96 huku ikiendelea kukuza soko lake la uuzaji wa silaha katika kipindi cha miaka mitano.
Ufaransa imeongeza uuzaji wake wa silaha nje ya nchi kwa asilimia 44 huku Ujerumani ikiongeza soko lake kwa asimilia 21.
Israel na Korea Kusini zote ziliongeza uuzaji wake wa silaha nje ya nchi ingawa zote zimesalia kuwa washikadau wa chini katika hili.
Ununuaji wa silaha uliongezeka Mashariki ya Kati
Soko ma Mashariki ya Kati la ununuaji wa silaha lilikuwa kwa kasi zaidi, ununuaji ukiwa asilimia 25 zaidi mwaka 2016-20 ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita.
Ongezeko kubwa lilikuwa ni kutoka soko la Saudi Arabia asilimia 61, Misri asilimia 136 na Qatar ni asilimia 361.
Asia na Oceania zilikuwa wanunuaji wakubwa wa silaha zikiwa na asilimia 42 ya silaha hizo.
India, Australia, China, Korea Kusini na Pakistan walikuwa wanunuaji wakubwa wa silaha eneo hilo.
Kupungua kwa ununuaji wa silaha Urusi na China
Urusi na China zote zilishuhudia kupungua kwa soko la uuzaji wa silaha ingawa nchi hizo mbili bado ni wauzaji wakubwa wa silaha nchi za kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika.
Uuzaji wa silaha kwa Urusi ulipungua kwa asilimia 22 ukichangiwa pakubwa na kushuka kwa uagizaji wa silaha kwa asilimia 53 na India.
"Ingawa Urusi hivi karibu ilitia saini makubaliano mapya makubwa ya uuzaji wa silaha kwa nchi kadhaa, na mauzo yao yataongezeka taratibu miaka ijayo, inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka Marekani katika maeneo mengine," amesema mtafiti wa Sipri Alexandra Kuimova.
Uuzaji wa silaha kwa nchi ya China, ambayo ni ya tano katika biashara hiyo umepungua kwa asilimia 7.8.
Pakistan, Bangladesh na Algeria walikuwa wanunuaji wa silaha wakubwa kutoka China