Virusi vya corona: Ni athari gani zinapatikana katika chanjo ya Corona na kwa nini?

Persona con mascarilla.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Unaweza kuumwa na kichwa ingawaje kwa muda mfupi baada ya kupata chanjo. Kawaida maumivu hayo hupotea baada ya siku 2-3.

Kupata athari mbaya baada ya kupata chanjo dhidi ya corona ni kawaida na inaweza kuwa ishara kwamba chanjo inafanya kazi.

Baada ya chanjo, homa, maumivu, au uchovu huweza kuonekana.

Kila mtu anaweza kupata moja ya dalili hizi, mchanganyiko wa wote au hata kukosa daalili zozote .

Lakini athari hizi huondoka na kawaida kwenye saa au siku.

"Ugonjwa huo ni mbaya sana kuliko idadi kubwa ya athari za chanjo. Chanjo huokoa maisha na kiwango cha juu cha kinga ," mtaalamu wa virusi Julian Tang, kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza, ameiambia BBC Mundo.

Wataalamu wanapendekeza uwe macho baada ya kupokea chanjo kwani, ikiwa kuna athari kali za pembeni, hufanyika ndani ya dakika na saa ya chanjo.

La mwisho, hata hivyo, inaonekana kuwa haliwezekani kutokea.

Kulingana na utafiti ulioongozwa na wataalam kutoka Hospitali Kuu ya Massachusetts, huko Boston, Marekani, kuenea kwa athari mbaya za chanjo hiyo ni kati ya kesi 2.5 na 11.1 kwa dozi milioni za chanjo ya Pfizer, kwa mfano.

Na nyingi za visa hivyo hufanyika kwa wagonjwa walio na historia ya mzio.

Takwimu hii inaweza kutofautiana kidogo kulingana na aina ya idadi ya watu au chanjo, lakini inatoa tathmini ya jinsi inavyowezekana kukuza athari mbaya ya mzio.

Je, athari mbaya hutokeaje na kwa nini wataalamu wanaona ni jambo la kawaida ambalo halifai kukupa wasiwasi ?

Chanzo cha picha, Getty Images

Jinsi Mwili unavyojibu chochote kigeni

Kupata athari ya pembeni ni jambo la kawaida na mara nyingi ni ishara kwamba mfumo wa kinga unaitikia vizuri.

"Ni vigumu kutoa idadi halisi juu ya uwezekano wa kutkea kwa athari mbaya kwa sababu kila idadi ya watu au mtu hujibu tofauti," anafafanua Julian Tang.

Nchini Uingereza, moja ya nchi zilizoendelea sana katika kampeni ya chanjo, mmoja kati ya watu 10 hupata athari mbaya.

Lakini hili, wataalam wanasisitiza, ni kitu cha "kawaida kabisa."

"Chanjo, ni kama virusi, bado ni ni kitu kigeni kinachosababisha mwili kujibu kwa kutoa kingamwili," Daktari Josefina López, ambaye anashiriki katika kampeni ya chanjo huko Madrid, Uhispania, anaelezea BBC .

"Ili kujilinda, mwili hutengeneza majibu yanayoweza kuchochea kuibuka kwa uchungu au aina mbali mbali ya maumivu . Na hilo linaweza kufanya joto kuongezeka .Ni mchakato wa kawaida ambao unaweza kutokea na chanjo yoyote, sio tu ile ya coronavirus," anaongeza mtaalamu huyo .

"Kuvimba ni kitu ambacho mwili pia hupata wakati wa jeraha baya kwenye goti baada ya kuanguka. Kisha unahisi maumivu, uekundu na uvimbe katika eneo hilo," Profesa Wilbur Chen, kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Maryland huko Marekani anaelezea BBC. Kwa maana hiyo, ni kawaida "kutarajia kwamba kuna athari mbaya sio kwa chanjo tu, bali pia kwa dawa au hata chakula.

Lazima ufikirie athari hizi kama dalili ya kawaida kwamba chanjo inafanya kazi. Dalili zozote kwa ujumla humalizika baada ya siku 2 au 3' anasema Chen.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Moja ya athari inayoweza kutokea ni kuhisi uchungu katika mkono uliochanjwa.

Madhara yanaweza kutokea lini?

Tumepewa chanjo kwa miezi michache na hiyo inamaanisha kwamba maelezo yanazidi kutolewa kila mara .

"Madhara mabaya kwa vijana yanaweza kuonekana zaidi, ambayo haimaanishi kwamba hali hiyo ni mbaya zaidi ," anasema Lopez.

Hii ni kwa sababu "wazee kawaida hupata kuzorota kwa kinga ya mwili ambayo ni kawaida na ongezeko la umri," anasema Wilbur Chen.

Katika chanjo ambazo zinahitaji dozi mbili, kama Pfizer, Moderna au Sputnik V, inaonekana kuna mazoea ya kupata athari baada ya kupokea dozi ya pili.

"Dozi ya kwanza hutengeneza mwitikio wa kinga ya kati na ya pili huiimarisha. Ndio sababu ya pili hutoa matokeo yenye nguvu zaidi na inahusishwa zaidi na athari nyingine," anaelezea Dk Andrew Badley, kutoka Kliniki ya Mayo nchini Marekani.

Tang pia anaonya kuwa aina ya dalili zinaweza kukuzwa na mtazamo wa wagonjwa.

"Wagonjwa wengi, wanaogopa au wanahangaika kupata chanjo, wanaweza kupata maumivu kidogo na kisha kuripoti kwamba yalikuwa makubwa kuliko ilivyo. Hali ya kifikra pia ina wajibu," anasema mtaalam.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wazee huwa na athari chache kuliko watu wachanga.

Nini cha kufanya basi ikiwa unapata dalili yoyote?

"Kwangu mimi , wakati nilipopewa chanjo ya AstraZeneca / Oxford, nilipata homa kidogo nnikameza dawa ya acetaminophen," anafichuaJulian Tang.

Dawa kama vile paracetamol au ibuprofen zinaweza kusaidia kupunguza maumivu ingawaje ni bora kupata ushauri wa daktari kabla ya kuzitumia .

Haishauriwi kuzimeza dawa hizi kabla ya kupata chanjo kama njia ya kuzuia.

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Cha Marekani kinashauri kutumia kitambaa kilicholoweshwa maji , kusongesha na kuufanyisha mazoezi mkono mkono uliopewa chanjo ili kupunguza maumivu yoyote.

Ikiwa una homa, inasaidia kunywa maji mengi na Kuvalia nguo nyepesi