Unyanyasaji mitandaoni: 'Nilibaini mume wangu anatengeneza picha za ngono'

laptop keyboard

Chanzo cha picha, Thinkstock

Watu wanaombwa kubaini ishara zinazoonesha watu wa familia zao wanatazama picha chafu mitandaoni.

Pia simu zinazopigwa kupitia nambari zilizotolewa kukabiliana na unyanyasaji wa mitandaoni nchini Uingereza zimeongezeka kwa karibu asilimia 50 wakati wa janga la corona, ripoti imesema.

Shirika la kutoa msaada kwa waathirika la Stop it Now! limesema kuwa na muda mwingi nyumbani wakati huu wa kusalia ndani kumeonesha ishara katika baadhi ya nyumba.

Sarah - sio jina lake kamili - kutoka Wales ameshirikisha wengine katika simulizi yake akiwa na matumaini kuwa itasaidia wengine.

Mume wake ambaye amekuwa naye kwa miaka 25 alikamatwa karibu miaka 5 iliopita kwa kutengeneza picha chafu za watoto.

"Sikujua alichokuwa anafanya hadi siku moja, polisi walipovamia nyumba yetu ghafla saa za asubuhi nikiwa kwenye chumba changu nikijayarisha kwenda kazini," alisema.

"Lazima awe alifahamu athari zake lakini akaendelea kusema, 'Mimi sio watu wanaovutiwa kingono."

Chanzo cha picha, Stop it Now

Polisi walimkamata mume wake akiwa nyumbani kwenda kumuhoji na kuondoa vifaa vyote vya kielektroniki kutoka nyumbani .

Baadaye siku hiyo, Sarah aliweza kuzungumza naye katika kituo cha polisi na huko ndipo alipokiri kwamba amekuwa akitazama picha za ngono kwa miaka 10 ikiwemo utumiaji nyenzo haramu kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

"Nilipatwa na mshutuko nikakosa la kusema," Sarah aliongeza.

"Nilipojua kile ambacho mume wangu amekuwa akifanya, bila majadiliano yoyote ili maanisha kwamba ndoa yetu imeishia hapo.

"Wanawake wengi huamua kusalia na wapenzi wao, lakini nilijua kwamba mambo hayawezi kuwa kama kawaida tena."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sarah alikuwa akidhania mume wake anasoma vitabu kuhusu anayopenda kama vile michezo.

Sarah alianza kutafuta talaka kwasababu alihisi hawezi tena kumuamini.

Pia, suala hilo lilimueka pabaya kama mwalimu wakati huo huo akihitajika kutoa taarifa hizo kwa wasichana wao vijana ambao walikuwa wanasoma chuo kikuu.

"Ilikuwa vibaya sana kuwaelezea wasichana wangu nilichofanya, hatua ambayo nililazimika kuchukua kwasababu wote walikuwa wameenda kusoma," Sarah alisema.

"Nilikuwa na hofu kwamba ikiwa nitashindwa kuchukua hatua mapema, huenda wakasikia niliyoyafanya kupitia mitandao ya kijamii.

"Polisi waliwasili kwa magari yao na pia walikuwa wameenda kazini kwa mume wangu kuchukua kompyuta yake, kwa hiyo, sikujua ni kipi kinachojulikana na jamii."

Mabinti wote wawili wamejitahidi kujenga tena uhusiano wao na baba yao, ingawa Sarah ambaye aliolewa tena, anasema kuwa sasa hivi amepata msongo wa mawazo na anaishi maisha ya umaskini tu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sarah alianza kushuku kuna kitu ambacho hakiko sawa kwasababu ya ishara alizokuwa anaziona.

Amesema ni muhimu watu kufahamu ishara za tabia hiyo nyumbani.

Mume wake alikuwa na historia ndefu ya msongo wa mawazo na kutojiamini, alikuwa na wakati mgumu kufanyakazi na kila wakati alikuwa na wasiwasi huenda akapigwa kalamu.

Sarah alifikiria kwamba mume wake kulala saa za usiku wa manane na matatizo ya kupata usingizi kulitokana na kusoma sana juu ya kile anachopenda, michezo.

"Sasa hivi ndio huwa natamani kama nisingemuamini, na pia ningekuwa na mshuku," Sarah alisema.

"Watoto walionyanyaswa ndio waliokuwa waathirika wakuu wa uhalifu huu."

Anasema kuwa ni muhimu kwa watu kuchukuwa hatua ikiwa utaanza kumshuku mtu na kusifia usaidizi aliopata kutoka shirika la Stop it Now!