Kifo cha rais John Pombe Magufuli: Ratiba ya mazishi yake yabadilika

Rais John Pombe Magufuli

Chanzo cha picha, Reuters

Mwili wa rais John Pombe Magufuli hautazikwa tarehe 25 Alhamisi kama ilivyokuwa imetangazwa na rais mpya wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan na badala yake mazishi yake yatafanyika Ijumaa tarehe 26.

Hatua hii inajiri baada ya kufanyika kwa mabadiliko katika ratiba hiyo ambapo mwili huo sasa umepangiwa kupelekwa kisiwani Zanzibar ili kuagwa.

Awali mwili wa marehemu ulitarajiwa kuagwa katika katika mji wa Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Geita na Chato ambako utazikwa, kama ilivyotangazwa na rais Samia Hassan Suluhu.

Hatahivyo mwili huo utapelekwa Zanzibar ambapo wakaazi wa Pemba na Unguja watapata fursa ya kuuaga tarehe 23.

Ratiba ni kama ilivyo:

Tarehe 20 na 21 Wakaazi wa Dar es Salaam watapa fursa ya kuuaga mwili huo ili kutoa heshima zao za mwisho.

Mnamo tarehe 22 mwezi Machi , wakaazi wa mji mkuu wa Dodoma nao watapata fura ya kipekee kuuaga mwili wa kiongozi wao.

Baadaye 23 mwezi Machi mwili utasafirishwa hadi Kisiwani Zanzibar ambapo wakaazi wa pemba na unguja watakongamana katika uwanja wa Amani ili kuuaga mwili wa kiongozi wao.

Vilevile tarehe wakazi wa 24 Mwanza nao watapata fursa ya kuuona na kuuaga mwili wa rais Magufuli.

Mwili huo baadaye utasafirishwa hadi nyumbani kwa rais Magufuli huko Chato, Geita ambapo wakazi wa eneo hilo watapata fursa ya kuuona mwili wa mwana wao kwa mara ya mwisho .

Na ifikiapo tarehe 26 mwezi Machi basi mwili wa rais huyo wa Tanzania utapatiwa mkono wa buriani na kuzikwa nyumbani kwao huko Chato.

Kifo cha rais Magufuli kilitangazwa na makamu wake ambaye sasa ndio rasi mpya wa taifa hilo baada ya kiongozi huyo kuugua matatizo ya moyo.