Kifo cha Magufuli: Familia iliyopoteza watu watano wakimuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania yapata msiba mwingine

Kifo cha Magufuli: Familia iliyopoteza watu watano wakimuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania yapata msiba mwingine

Familia moja jijini Dar es Salaam, Tanzania iliyopoteza watu watano kwenye tukio linalodaiwa la kukanyagana wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli, imesema imepata mwili mwingine wa msichana wa kazi.

Kupatikana kwa mwili huyo, sasa familia hiyo ya Denis Mtua, imepoteza jumla ya watu sita akiwemo mke wake, watoto wawili, wapwa zake wawili, na msaidizi wa kazi.

Wote hao walienda kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli siku ya Jumapili katika Uwanja wa Uhuru, lakini hawakurejea tena nyumbani.

Kwa siku tatu familia hiyo ilikuwa ikimtafuta binti huyo, bila mafanikio kabla ya kuukuta mwili wake kwenye moja ya vyumba vya kuhifadhia maiti.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi nchini Tanzania halijatoa taarifa rasmi, ingawa Kamanda wa Polisi wa kanda ya kipolisi ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa aliiambia BBC kuwa angezungumzia tukio hilo hapo jana.

Bwana Denis Mtua amezungumza na Scolar Kisanga.