Mzozo wa Tigray: Mwanadiplomasia bandia na taarifa nyingine za upotoshaji

Mzozo katika eneo la Tigray ulianza mwezi Novemba

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mzozo katika eneo la Tigray ulianza mwezi Novemba

Hali ya wasiwasi bado ni ya juu katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray huku kukiwa na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na hatari ya kuendelea kutokuwepo kwa uthabiti.

Mzozo uliibuka mwezi Novemnba mwaka 2020 wakati vikosi vya serikali ya Ethiopia vilipoanzisha mashambulio dhidi ya vikosi vya jimbo la Tigray , ambavyo vilishambulia na kudhibiti ngome za jeshi za serikali.

Huku kulifikia jimbo hilo kwa watu na taasisi huru vikizuiwa sana, vita vya propaganda vimekuwa vikiendelea katika mitandao ya kijamii huku pande zote mbili zikihusika katika kusambaza taarifa zisizo sahihi na za upotoshaji.

'Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa' ambaye hawezi kupatikana

Shirika rasmi la habari la Ethiopia (EPA) limeripoti kuwa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu, ambaye zamani alifanyia kazi Umoja wa Mataifa, amekuwa akituma jumbe za Twitter kuiunga mkono Ethiopia katika vita hivyo.

Akaunti ya Facebook ya EPA ilituma mara mbili jina la George Bolton, akitumia anwani ya Twitter ya @GboltonUN.

"Bw Bolton" - anajielezea kama mchanganuzi wa masuala ya siasa na afisa wa zamani wa Umoja wa mataifa - akiuita uongozi wa Tigray kama ''katili'', akisema kiongozi wa Ethiopia alishinda Tuzo ya amani ya Nobeli, na kwamba Marekani inapaswa kuwa nje ya mzozo.

Ujumbe huo huo uliandikwa kwenye kurasa za Facebook za EPA za lugha za Amharic na Tigrinya.

Lakini tumebaini kuwa hakuna utambulisho wa mtu huyu, na Umoja wa Mataifa hauna rekodi ya mfanyakazi wa sasa au wa zamani mwenye jina hili - katika rekodi zao za miongo mingi.

Picha ya utambulisho iliyotumiwa ni sawa kabisa na ile iliyokuwa sehemu ya uchunguzi wa gazeti la Financial Times mwaka jana kuhusiana na ubunifu wa sura wa programu bandia ya intelijensia.

Ilikuwa ni mojawapo ya mifano ambayo ripoti hiyo iliielezea kama iliyotengenezwa kwa teknolojia ya mtandao (GANs)

Tumegundua kuwa kwa wakati mmoja jumbe zote katika Twitter hii ziliondolewa katika kipindi cha wiki moja, halafu picha ya utambulisho ikabadilishwa mara kadhaa.

Wakati mmoja, akaunti ilikuwa na picha ya utambulisho ya katibu wa sasa wa Umoja wa Mataifa Secretary-General Antonio Guterres - lakini ilikuwa bado inatumia anwani ya Twitter ya @GboltonUN.

Baadae ilibadilika ikawa na picha ya mtu mwingine, ila ikaendelea kuwa na anwani ile ile ya Twitter.

Hapa ni mahali ambapo kanisa liliangamizwa katika uvamizi wa mabomu uliofanywa na majeshi ya Ethiopia zaidi ya miaka 20 iliyopita, mwaka 1999.

Tumepata picha ya eneo la tukio baada ya shambuli na inaonesha wazi jengo lililoharibiwa likifanana na picha inayoonekana.

Picha ya upotoshaji ya 'uharibifu wa kanisa'

Mzozo katika jimbo la Tigray uharibifu wa majengo mengi, yakiwemo makanisa

Hatahivyo, picha zinazosambazwa sana kwenye mtandao za wanaume wawili wanaosali kando ya jengo lililoharibiwa zikiwa na dai kuwa ni kanisa lililoangamizwa katika jimbo la Tigray ni upotoshaji.

Picha hizo sio za kutoka Tigray.

Utafiti kuihusu picha hii ulifichua picha hiyo ikionekana kwenye ujumbe wa Facebook kuanzia mwezi Julai 2018, ambapo ilifichua mahala ilipokuwa ilikuwa ni katika mji wa Adi Keih in Eritrea.

Hapa ni mahali ambapo kanisa liliangamizwa katika uvamizi wa majeshi ya Ethiopia zaidi ya miaka 20 iliyopita, mwaka 1999.

Tumebaini picha za baada ya shambulio na inaonesha wazi jengo linafanana na lile linalooonekana kwenye picha.

Watoto hawa wenye kiu hawako Tigray

Picha inayoonesha wavulana wakinywa maji ya matope kwenye mtaa imeshirikishwa kwenye mtandao sana ikiwa na kauli zinazosema inafichua hali mbaya ya kibinadamu katika Tigray.

Katika ujumbe wa Twitter ulitumiwa mchoro wa eneo sambamba na kampeni za twitter - na alama ya reli - hashtags, ukisema kuwa lilikuwa ni "wazo kwa ajili ya mchoro mpya wa kutoa uelewa kuhusu watu wanavyokumbwa na njaa Tigray."

Lakini picha sio ya kutoka Tigray kabisa - Ni kutoka katika jimbo la kusini-mashariki mwa Ethiopia katika jamii inayozungumza kisomali.

Sayid Abdirahman, ambaye aliiambia BBC kuwa alipiga picha hiyo katika kijiji cha Awil kusini mwa nchi mwezi Disemba.

Jumbe za Bw Abdirahman zimekuwa mara kwa mara zikihusu masuala ya maji na usafi katika jamii inayozungumza kisomali nchini Ethiopia

'Uchunguzi wa Marekani' ambao haukufanyika

Mwezi Februari, Amnesty International ilichapisha ripoti kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu ambao ilisema ulitekelezwa na vikosi vya Ethiopia na Eritrea katika shambulio dhidi ya mji wa kihistoria wa Tigray wa Axum Novemba 2020.

Madai haya yalikanushwa na serikali ya Ethiopia, ambayo iliyaelezea kama "uzushi."

Baadaye, ripoti ya gazeti linaloegemea upande wa serikali Herald lilidai kuwa timu ya uchunguzi kutoka Shirika la maendeleo ya kimataifa la la Marekani (USAID) ilitembelea mji wa Axum lakini "haikupata eneo hata moja la kaburi wala kukutana na ndugu" wa watu ambao ripoti zilisema waliuawa katika mauaji ya kikatili.

Lakini USAID inasema haijawahi kutuma wachunguzi wake mjini Axum.

"USAID haijaendesha uchunguzi au kutuma ujumbe wake kuchunguza matukio yaliyoripotiwa kufanyika katika Axum," ilisema katika taarifa yake kwenye mtandao wa Twitter.