Jinsi ya kutengeneza asali bila nyuki na maziwa bila ng'ombe

Vyanzo vya asali katika kiwanda cha MeliBio

Chanzo cha picha, MELIBIO

"Nikiwa binafsi mtu asiyekula nyama, kusema kweli ninakosa kula asali," anasema Darko Mandich, muasisi mwenza na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya MeliBio.

Si jambo la kawaida kwa mtu asiyekula nyama kuhisi kuwa anavikosa vyakula vya aina fulani. Jambo ambalo sio la kawaida, hata hivyo, ni suluhu ya Bw. Mandich: Kuamua kubuni aina ya asali, inayofanana kwa kila kiungo na asali ya kawaida tunayoifahamu lakini yake inatengenezwa bila nyuki kuhusishwa kabisa.

"Unapotazama asali na jinsi ilivyotengenezwa, ilianza kwa nyuki kukusanya nta na kisha kujenga ukuta wa asali, ambao ni mchanganyiko wa Flactose na glucose," anasema.

"Tunachanganya mchanganyiko huu katika maabara, kwa kutumia vimelea wadogo -micro-organisms ambao hawatumiki kwa kawaida katika kujenga kuta za asali ."

Kwa miaka michache iliyopita, mimea iliyotumiwa kutengeneza nyama na maziwa mbadala imesambaa zaidi. Hata hivyo, kwa wengi haifikii kiwango cha ladha, na utamu wa nyama ya kawaida au maziwa.

Lakini sasa, idadi ya makampuni madogo kama MeliBio, yanaangalia namna ya kutumia chachu kutengeneza bidhaa za wasio kula nyama yaani (vegetarians) ambazo zinaweza kufanana kibaiolojia na bidhaa halisi.

Kupitia mchakato wa kuchachisha, vimelea wadogo humeng'enya chakula na kutengeneza bidhaa muhimu- chachu, kwa mfano, hula sukari na kutengeneza kileo cha kutengeneza pombe.

Lakini kwa kuwatunza vimelea wadogo kwa uangalifu na kuchagua magala sahihi, inawezekana kubuni bidhaa tofauti kuanzia asali, mayai meupe, hadi maziwa.

Chanzo cha picha, SOPHOTOGENIC PHOTOGRAPHY

Kampuni moja inatumia mtindo huu kutengeneza maziwa bora- Better Dairy, kituo cha kwanza kinachotengeneza maziwa na jibini kwa njia ya uchachishaji.

"Jinsi inavyofanyika ni kwamba unaweza kutumia chachu kutengeneza pombe - lakini tunabadili kidogo chachu ili badala ya kutengeneza bia, inatengeneza kile tunachotaka," anasema Jevan Nagarajah, muasisi mwenza na mkurugenzi mtendaji.

Mbinu sawa na hizi zinatumiwa kutengeneza mayai meupe, huku kampuni ya Clara Foods ya mjini San Francisco -inayotengeneza bidhaa kwa wingi ikitumai kuwa itakuwa kampuni kubwa zaidi inapotengeneza protini itokanayo na mayai duniani ifikapo mwaka 2028.

Chanzo cha picha, CLARA FOODS

"Teknolojia yetu tunayoimiliki ya kuchachisha inaturuhusu kudhibiti au hata kupitisha muundo, ladha ya mayai mbadala ya yale ya kuku," anasema muasisi na Mkurugenzi mtendaji Arturo Elizond.

Pamoja na kuwafanya wasio kula nyama kuwa wenye kufurahia bidhaa zinazotengenezwa kwa kuchachishwa zinaweza kuwa na manufaa ya kimazingira.

Kulingana na Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) nyama na bidhaa zitokanazo na maziwa huchangia utoaji wa hewa chafu kwa kiwango cha asilimia 14.5 ya hewa chafu inayotolewa duniani.

Wakati huohuo, hamu ya wakazi wa dunia ya asali inawadhuru vizazi vya nyuki, anasema Bw. Mandich.

Chanzo cha picha, MELIBIO

Tuna uwezekano wa kushuhudia bidhaa za kibaiolojia zinazofanana kwa viungo katika bidhaa nyingine katika maboksi au chupa madukani.

"Takriban theluthi mbili ya asali huuzwa madukani kama kiungo cha bidhaa nyingine - na viwanda kama vile chakula, vinywaji, vipodozi na dawa.

Kwahiyo, sisi kama kampuni tunaanza na muundo wa biashara kwa biashara kwanza," anasema Bw. Mandich. "Tayari tuna makampuni 15 nchini Marekani ambayo yamesaini barua ya nia ya kufanya kazi nasi."

Wataalamu wa kampuni ya MeliBio wanatarajia kuanza kusambaza bidhaa ya asali mbadala kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka huu.

Chanzo cha picha, MELIBIO

Kwa mfano asali, hakuna sababu ya ni kwanini, uzalishaji wake hauwezi kutumiwa kutengeneza nakala yake ya asali ya manukato -inayodaiwa kuwa na faida za afya, na kukugarimu takriban mara 100 ya gharama ya asali ya kawaida.

Fursa sawa zipo kwa maziwa na jibini.

"Kwa kufanya hivi, hatukulazimika kuweka bidhaa za maziwa. Tutatumia sukari badala ya maziwa ambayo humeng'enywa katika tumbo za binadamu ," anasema Bw. Nagarajah.

Wakati huo huo, Bw. Nagarajah anaweza kula asali tena-kama tu ni ya kiwango kidogo kwa sasa.

"Nilionja asali mbadala ya majaribio ya 23 siku mbili zilizopita," anasema.