Ni mamluki gani waliokodiwa kumuuwa mtu hatari zaidi duniani

Peter in the Rhodesian SAS

Chanzo cha picha, Two Rivers Media

Maelezo ya picha,

Peter McAleese alihusika katika vita vya Rhodesia

Mwaka 1989, timu ya mamluki wa Uingereza iliyoongozwa na raia wa Scotland Peter McAleese, walisafiri hadi ngome ya mhalifu hatari zaidi duniani lengo likiwa ni kumuuwa.

Pablo Escobar alikuwa kiongozi wa genge la mihadarati katika mji wa Medellin nchini Colombia na mhalifu tajiri zaidi katika historia ya dunia.

Alikuwa mtengenezaji mkubwa na msambazaji wa dawa ya kulevya aina ya kokeini kote duniani, yeye ndiyo alikuwa msambazaji wa asilimia 80 ya mihadarati kote duniani wakati huo.

McAleese alisajiliwa na genge la upinzani nchini Colombia nia ikiwa ni kumuuwa Escobar.

Filamu mpya ya, "Mauaji ya Escobar", inaelezea simulizi ambayo lengo lake halikutimia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pablo Escobar alikuwa mmoja wa wahalifu tajiri zaidi na kiongozi hatari zaidi duniani wa genge la uhalifu

Aliyetengeneza filamu hiyo ni David Whitney, ambaye alisema McAleese ambaye alizaliwa Glasgow mwaka 1942, alikuwa mtu "asiyetabirika" "mtata" na pia "mwenye matatizo ya kisaikolojia".

Katika filamu hiyo, McAleese, ambaye sasa hivi ana umri wa miaka 78. Alisema: "Nilifundishwa kuua nikiwa jeshini".

McAleese alisema alikuwa mwanajeshi akiwa na umri wa miaka 17 hasa akiichukulia kama fursa ya kukabiliana na hasira zake. Akiwa mtoto, alikuwa mwenye kusababisha matatizo kwa kila mtu, alinyanyasa wengine na mwenye chuki nyingi sana.

Chanzo cha picha, Two Rivers Media

Maelezo ya picha,

Peter akiwa katika jeshi la Afrika Kusini miaka ya 1980

Alihudumia kambi ya Borneo akipigana vita vya msituni kabla ya kuondoka jeshi la Uingereza mwaka 1969, uamuzi ambao anauelezea kama mbaya zaidi katika maisha yake.

Baada ya McAleese kuondoka jeshini, alianza kurukaruka kutoka kwa kazi moja hadi nyingine.

Anasema alijihisi kupoteza mwelekeo na akawa mbaya zaidi kiasi kwamba alijipata gerezani kwasababu ya kumnyanyasa mchumba wake.

Baada ya kuachiwa huru, McAleese alijitahidi kufuata njia ya kutimiza taaluma yake na kujiunga katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Angola na baadaye akajiunga na jeshi la Rhodesia (ambayo sasa hivi inafahamika kama Zimbabwe), pamoja na Afrika Kusini.

Alikutana na Dave Tomkins nchini Angola mwaka 1976.

Tomkins hakuwa mwanajeshi tu wa kawaida, alikuwa na shughuli zake anazoziendesha kisiri pamoja na kuuza silaha.

Wawili hao wakawa marafiki wakubwa na Tomkins akamtafuta McAleese na wakazungumzia mipango yao ya siri ya kumuua Escobar.

Chanzo cha picha, Two Rivers Media

Maelezo ya picha,

Kitambulisho cha kijana Peter McAleese wakati akiwa mamluki barani Afrika

Jorge Salcedo, alikuwa sehemu ya genge pinzani la mihadarati nchini Colombia lililojulikana kama Cali, na yeye ndiye aliyeratibu operesheni ya kumuuwa Escobar.

Alitaka Tomkins kusajili timu yenye nguvu kutekeleza uvamizi huo na wa kwanza kumtaja alikuwa McAleese.

"Hautahitajika kupanga mauaji ya Pablo Escobar, pengine uwe na tajriba ya juu," alisema McAleese.

"Sikuwa na nia ya kumuuwa, amesema.

"Hayakuonekana kama mipango ya mauaji. Badala yake nililichukulia kama shambulizi tu."

Genge la Cali lilikuwa na uhakika kwamba Escobar anaweza kuuliwa tu kirahisi akiwa katika nyumba yake ya kifahari huko Hacienda Napoles.

Bunduki na mabomu

Nyumba yake ilikuwa na wanyama mbalimbali, magari ya zamani na kifahari, uwanja wa ndege wa kibinafsi na uwanja wa mafahali kupigana.

McAleese alisafiri kwa ndege hadi eneo la ndani ya nyumba ya Escobar kuchunguza ikiwa wanalopanga linawezekana na kukubaliana kwamba linawezekana.

Njama ya kumuua ikaanzia hapo.

Tomkins alisajili tmu ya mamluki 12, watu ambao alikuwa amewahi kufanya nao kazi au ambao alikuwa amependekezewa.

Njama yao nchini Colombia ikaanza kuratibiwa na Jorge Salcedo, wa genge la Cali. Mamluki wote walilipwa dola 5,000 kwa mwezi na pia matumizi yao wakati wa operesheni yao yakasimamiwa.

Lakini Tomkins alikuwa akilipwa dola 1,000 kwa siku.

Chanzo cha picha, Two Rivers Media

Maelezo ya picha,

Mamluki wakati wa mazoezi nchini Colombia tayari kutekeleza shambulio

Filamu hiyo inaonesha video iliyotayarishwa na Tomkins inayojumuisha wanaume waliokuwa na pesa kweli.

Mara ya kwanza walikuwa wakiishi katika mji wa Cali lakini walikuwa katika hatari ya kujulikana na wakaamua kwenda eneo la viungani ambapo walipewa kiasi kikubwa cha pesa.

"Ilikuwa kama sikukuu ya Krismasi," McAleese amesema. "Kila tulichotaka kama silaha kilipatikana."

Mamluki hao walifanya mazoezi kweli kwa ajili ya njama hiyo lakini aliyejua lengo lake hasa ni Tomkins na McAleese.

Kabla ya wengine kuarifiwa, mmoja wao alijitoa kwenye njama hiyo na akaruhusiwa kwenda nyumbani.

Alichofanya baada ya hapo ni kusema kila kitu alichokijua katika moja ya magazeti ingawa hakutaja majina yao wala hakutoa taarifa za operesheni hiyo.

Wakati shambulizi linakaribia, mamluki hao waliamua kwenda jangwani ili kufanya mazoezi kwa kutumia silaha na mabomu bila kusikika na mtu yeyote.

Chanzo cha picha, Two Rivers Media

Maelezo ya picha,

Picha halisi ya timu iliyokuwa inafanya mazoezi wakati wa shambulio

Njama ya utekelezaji shambulizi hilo ilijumuisha helikopta mbili ambazo zingepaa katika eneo la Hacienda Napoles huku mamluki hao wakifyatua risasi ikiwa sehemu ya operesheni ya kumuua mbabe wa uuzaji mihadarati Escobar na kurejea na kichwa chake kama zawadi.

Waliposikia kwamba yuko nyumbani kwake wakapanga shambulizi ambalo halikuwahi kutokea.

Helikopta iliyokuwa imembeba McAleese na Tomkins ikaanguka ikiwa inapaa chini chini tu na rubani akafariki dunia.

Ahadi kwa Mungu

Wengine walinusurika lakini McAleese alipata majeraha mabaya.

Alipitia uchungu kwa siku tatu bila kupata usaidizi hadi alipookolewa.

Escobar aliposikia kuhusu shambulizi hilo lililopangwa akatuma genge lake mlimani kuwasaka.

"Ikiwa Pablo angenipata wakati huo, bila shaka ningekufa kifo cha machungu kweli kweli," McAleese anasema.

Badala yake alifanikiwa kutoroka na akajitahidi kutimiza mazuri aliyokuwa amemuahidi Mungu wake, wakati akiwa amelala mlimani na majeraha mabaya bila usaidizi.

Chanzo cha picha, Two Rivers Media

Maelezo ya picha,

Akiwa na umri wa miaka, 78, Peter McAleese anasema kuwa anajutia mengi lakini amepata amani moyoni mwake

McAleese anakubali kwamba alikuwa mtu "mbaya, na fedhuli" lakini anasema kwamba, aligundua anahitaji kubadili mwenendo wa maisha ya

Lakini anachojutia sio matendo yake akiwa vitani, amesema, lakini ni kushindwa kwake kutekeleza majukumu yake kama mume na baba.

Akiwa na umri wa miaka 78, anasema hatimaye amepata amani moyoni mwake.

Huku Pablo Escobar, mbabe hatari wa mihadarati duniani, akifariki dunia kwa kupigwa risasi mwaka 1993 akiwa anatoroka mamkala.ke.