Ufaransa 'ilifumbia jicho' mauaji ya kimbari ya Rwanda, ripoti imesema

Hutu militia/French military jeep in Rwanda, June 1994

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Juni 1994: Wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa wakishika doria, wakiwapita waasi wa kabila la Wahutu nchini Rwanda

Ufaransa imebeba "mzigo mzito na inawajibika pakubwa" katika vita vya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, kulingana na ripoti iliyotolewa na wanahistoria wa Ufaransa lakini hawana ushahidi wowote unaoonesha Ufaransa ilihusisha katika vita hivyo.

Tume ya wataalamu imewasilisha ripoti hiyo kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Ripoti hiyo inasema Ufaransa "ilifumbia jicho" matayarisho ya vita hivyo vya kimbari.

Watu karibu 800,000 waliuawa pale waasi wa Kihutu wenye msimamo mkali walipowauwa Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa kati.

Timu hiyo ya maafisa wa Ufaransa imesema.

Rwanda, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiishutumu Ufaransa kwa kuhusika na vita hivyo, ilisema kuwa imepokea ripoti hiyo.

Serikali imesema kuwa "imewakilisha hatua muhimu katika ufahamu wa jukumu lililotekelezwa na Ufaransa katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi".

Kiongozi wa Mhutu alitawala Rwanda wakati mauaji ya kimbari yanatokea, Aprili-Juni 1994, lakini baadaye akaondolewa madarakani na Watutsi walioongozwa na chama cha Rwandan Patriotic Front (RPF) chini ya Rais Paul Kagame, ambaye sasa hivi ndiyo rais wa nchi hiyo.

Ripoti hiyo ina mlaumu aliyekuwa wakati huo Rais wa Ufaransa, François Mitterrand, kwa sera yake dhidi ya nchi ya Rwanda mwaka 1994, "iliyoshindwa".

Taarifa ya ripoti hiyo inawekwa wazi mbele ya umma baada ya usiri wa miaka kadhaa wa kuwa maafisa wa Ufaransa walihusishwa na Wahutu waliotawala Rwanda.

Rais Macron aliteua tume ya wajumbe 15 miaka miwili iliyopita, aliyowawezesha kufikia nyaraka za siri katika ngazi ya rais, kidiplomasia, jeshini na kijasusi.

Miongoni mwa data zilizokuwa zimehifadhiwa ni pamoja na zile za aliyekuwa rais wa Ufaransa aliyekuwa na uhusiano wa karibu na Rais wa Rwanda Juvénal Habyarimana, ambaye ni wa kabila la Wahutu.

Soma zaidi kuhusu mauaji ya kimbari Rwanda:

Mauaji hayo ya kimbari yalisababishwa na kudunguliwa kwa ndege, Aprili 6, 1994 iliyokuwa imebeba Rais Habyarimana na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira, ambaye pia alikuwa wa kabila la Wahu

Wanachama wa tume hiyo siyo wataalamu wa Rwanda - ikiwa ndivyo ilivyokusudiwa kuhakikisha hakuna upendeleo, hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Jopo hilo linajumuisha wataalamu wa mauaji makubwa katika mauaji ya raia wa Armenian katika vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia na katika sheria ya uhalifu kimataifa.

Wanaongozwa na mwanahistoria Vincent Duclert.

Juni 22 mwaka 1994 Umoja wa Mataifa iliagiza kupelekwa kwa wanajeshi wa Ufaransa kusini magharibi mwa Rwanda, katika kile kilichofahamika kama operesheni kubwa.

Ujumbe huo ukaibua utata: Eneo linalotoa msaada wa kibinadamu la Ufaransa likanusuru waliokuwa kwenye uwezekano wa kuwa waathirika dhidi ya wanaotekeleza mauaji ya kimbari, lakini baadaye, kukawa na madai kwamba usadizi wa Ufaransa ulichelewa mno na kuwa baadhi ya waliotekeleza mauaji walifanikiwa kujificha katika eneo hilo.

Mwaka 2015, aliyekuwa raia wa Ufaransa wakati huo, François Hollande alitangaza kwamba hifadhi ya Rwanda itakuwa wazi lakini miaka miwili baadaye, baada ya watafiti kuomba ruhusa ya kufanya utafiti wao, Baraza la Katiba Ufaransa likapitisha kwamba hifadhi hiyo isalie kuwa siri.

Serikali ya Rwanda imesema kuwa hivi karibuni itatoa taarifa yake, "ambayo itakuwa na umuhimu mkubwa katika yale yaliyoibuliwa na tume ya Duclert".