Tetesi za soka Ulaya Jumatano 31.03.2021: Kane, Lukaku, Haaland, Aguero, Messi, Grealish, Konate, Rodrigo, Ramsey

Harry Kane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 27, atakuwa mlengwa wa Manchester City ikiwa viongozi wa Ligi ya Primia watashindwa kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland msimu huu. (The Times)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Romelu Lukaku akisherehekea goli na wenzake

Manchester City na Chelsea zote zimembaini mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku, 27, raia wa Ubelgiji kama mchezaji wao mbadala ikiwa zitashindwa kumsajili Haaland, 20. (Eurosport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Erling Braut Haaland

Hata hivyo, City ina inami kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway Haaland msimu huu kama mbadala wa Sergio Aguero. (Manchester Evening News)

Nahonda wa Aston Villa Jack Grealish, 25, huenda akakosa kuhamia upande wa Pep Guardiola, huku City ikikatishwa tamaa na thamani yake ya pauni milioni 100 kwa kiungo huyo wa kati wa England. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero

Manchester United imetoa ofa kwa mshambuliaji wa Argentine Aguero, 32, ambaye ataondoka Manchester City msimu huu, huku Chelsea, Inter Milan na Paris St-Germain pia wakiwa miongoni mwa vilabu vyenye nia ya kumsajili. (Foot Mercato, via Star)

Barcelona, inaonekana kama yenye uwezekano mkubwa wa kumnyakua Aguero, ingawa klabu hiyo haijampa kipaumbele badala yake inawafuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Lyon raia wa Uholanzi, 27, Memphis Depay, Haaland wa Dortmund na Lukaku wa Inter kama vijana wadogo bado na machaguo yanayofaa zaidi. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Maelezo ya picha,

Messi

Mshambuliaji Lionel Messi, 33, hatahivyo, ameiambia Barcelona kumsajili Aguero, na Mwajentina mwenzake kunaashiria hitaji la msingi kuendeleza mkataba wake na klabu hiyo ya Kikatalani . (Football Insider)

Mlinzi wa RB Leipzig na kiungo wa Ufaransa wa chini ya miaka 21 defender Ibrahima Konate, 21, amefanyiwa na kupita baadhi ya uchunguzi wa kimatibabu anapojiandaa kujiunga na Liverpool. (RMC Sport - in French)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya RB Leipzig Mfaransa Ibrahima Konate

Mchezaji nyota wa Leeds United ambaye usajili wake ulivunja rekodi Rodrigo, 30, hajaridhika katika uwanja wa Elland Road na huenda akarejea La Liga katika juhudi za kujaribu kujiimarisha tena katika kikosi cha Uhispania. Real Betis na Sevilla zinamnyatia mshambuliaji huyo. (Fichajes - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Argentina Rodrigo de Paul, 26, anapania kuhamia Leeds United ikiwa ataondoka klabu ya Udinese ya Italia msimu huu, licha ya Atalanta ambayo imejikatia tikiti ya Champions League kumtaka. (Tutto Atalanta via Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa Ufaransa Kylian Mbappe

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, amewaambia wasimamizi wa soka wa Ufaransa kwamba hataweza kushiriki michezo ya Olimpiki mjini Tokyo, kwani anataka muda wa kutafakari hatma yake ya baadae katika klabu hiyo. PSG imepatiaofa ya mkataba mpya, huku Liverpool, Manchester City na Real Madrid zikimng'ang'ania. (Le Parisien, via Mirror)

Burnley huenda wakamsajili mkufunzi wa zamani wa Sheffield United Chris Wilder, 53, wakimkosa Sean Dyche, 49 - ambaye analengwa na Crystal Palace na Newcastle - ataamua kuondoka Turf Moormsimu huu wa joto. (Daily Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa Stoke City na Australia Harry Souttar

Crystal Palace, West Ham na Wolves wanamfuatilia mlinzi wa Stoke City na Australia Harry Souttar, 22. (Express)

Kiungo wa kati wa Sassuolo na Italia Manuel Locatelli, 23, ambaye amekuwa akivutia Manchester City na Real Madrid katika miezi ya hivi karibuni, anatarajiwa kujiunga na Juventus msimu ujao. (Tuttosport - in Italian)

Manchester United, Chelsea na Paris St-Germain wako katika kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wa kati wa Rennes Eduardo Camavinga, 18 japo nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka -21 hana mpango wa kuhamia Real Madrid ikiwa Zinedine Zidane ataondoka uwanja wa Bernabeu. (AS - in Spanish)

Arsenal, Leicester City na Strasbourg wanamtaka mlinzi wa Valencia Mfaransa Ismael Doukoure,17. (Foot Mercato - in French)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Houssem Aouar

Juventus itatafuta kitita cha kumhamisha kiungo wa kati wa Lyon, Houssem Aouar, 22, kwa kumuuza mchezaji raia wa nchi yake ya Ufaransa Adrien Rabiot, 25, na Aaron Ramsey, 30 wa Wales. (Calcio Mercato)

Peterborough United wameweka kitita cha angalau pauni milioni 5 kwa mfungaji wa mabao maarufu Jonson Clarke-Harris, 26, katika Ligi One, ambaye amehusishwa na Bournemouth na Sheffield United. (Bristol Post)