Libya 'mji wa mashetani' - kwanini uitwe hivyo?

Abdel Manaam Mahmoud buries his brother Esmail
Maelezo ya picha,

Abdel Manaam Mahmoud anamzika kaka yake ingawa hawezi kuwa na uhakika wa asimia 100 kwamba ni yeye

Kama mtu mzima wa familia, Abdel Manaam Mahmoud hakuwa na budi zaidi ya kuzika mwili wa kaka yake Esmail katika nyumba yake ya milele. Lakini pia, huenda anayemzika hii leo, asiwe kaka yake kama anavyofikiria.

Waliomzunguka ni wanaume wa Tarhuna waliokusanyika pamoja wakifukia mwili huo.

Karibu na kaburi la kaka yake, baba yake Mahmoud, Hussin, kaka yake Nuri na mjomba yake Mohamed pia nao wamezikwa - kila mmoja wao ni mwathirika wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya, wote wakiwa wameuawa na wanamgambo wale wale waliotawala mji wao.

Miili yao ilipatikana na kuzikwa kwasababu Libya ilisaini mkataba wa kusitisha vita mwaka jana.

Lakini tangu mwaka 2011, alipouawa aliyekuwa mtawala wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na ghasia na baadaye ikatumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Vita hivyo viliongezeka katika miaka ya hivi karibuni wakati Jenerali Khalifa Haftar, ambaye ana miaka 77, aliposhambulia mji wa mashariki wa Benghazi na kujaribu kuondoa serikali inayotambuliwa kimataifa ya mji wa Tripoli.

Alikuwa na wafadhili wakubwa sana ambao walimuunga mkono: Falme za kiarabu, Misri, Syria, Jordan na Ufaransa pia.

Shambulio lake katika mji wa Tripoli , liliendelea na kuwa la kutisha, baada ya Uturuki kutuma jeshi lake la majini na anga kuunga mkono serikali iliyoko madarakani.

Jeshi la Syria pia likaunga mkono na kufanya sumu ya vita kuongezeka zaidi hasa upande wa serikali chini ya udhibiti wa Uturuki.

Jenerali Haftar alikuwa amekodi wapiganaji wake wenye silaha- Wakandarasi kutoka Urusi na wapiganaji kutoka Sudan na Chad. kutoka Urusi na wapiganaji kutoka Sudan na Chad.

Idadi ya watu waliokufa iliongezeka katika taifa hilo lililokuwa limefikia mengi kabla ya athari za janga hili kubwa la kinyama kuanza kujitokeza.

Lakini kusitishwa kwa mapigano kuliamuliwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, Libya kuwa na serikali ya pamoja.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Abdul Hamid Dbeibah, ambaye ni mfanyabiashara tajiri wa kutoka eneo la kibiashara Misrata.

Wakati familia yake inahusishwa na utawala wa Muammar Gaddafi, mambo machache yalifahamika kuhusu waziri mkuu huyo mpya ambaye ni mgeni kwenye siasa.

"Hakuna mtu ambaye alimkubali," alisema mmoja wa wanadiplomasia kutoka Magharibi akiwa Tripoli, ameelezea kuwa uteuzi wa bwana Dbeibah uliofanywa na Umoja wa Mataifa -ni mchakato uliounda serikali ya mpito tu.

Uchaguzi unapaswa kufanyika ndani ya miezi tisa, katika siku ya uhuru kwa raia wa Libya- Desemba 24 - ingawa tayari kuna mashaka.

"Kuna siku chache zimebaki, lakini si kwamba haiwezekani. Lakini tena inaanza na taasisi na mamlaka ya Libya," alisema Jan Kubis, mwakilishi wa UN nchini Libya.

"Ingawa wanaweza kuja na kile ambacho wanapaswa kuja nacho, kufanikisha hili. Kama si hivyo... watakuja na udhuru wa kushindwa kufanya hilo... Nategemea hili halitatokea kwasababu watu wa taifa hili wangependa kuwa na uchaguzi.

"Si suala la matamko tu ya viongozi au ahadi. Ni kile ambacho watu wa taifa hili wanataka, ni kuwa na uchaguzi ifikapo Desemba 24."

Baada ya mahojiano yetu, Bwana Kubis alielekea Benghazi kukutana na jenerali Haftar, watu wengi wa Tarhuna waliamini alikuwa amewezeshwa na ndugu saba wanaofahamika kama 'Kani brothers' (ambao bwana Mahmoud alishutumiwa kuua ndugu zake) katika mauaji ya mwisho waliyotekeleza kabla ya kuondoka mji huo.

Kuna baadhi ya watu wanahisi kuwa labda jenerali anawahifadhi baadhi ya ndugu walionusurika, baadhi wakishuku labda wameongezwa kwenye orodha ya vikwazo ya Marekani na Ulaya.

Maelezo ya picha,

Ndugu za Kani walitawala mji huo kwa muda

"Mji wa Tarhuna ulikuwa kitovu cha mashambulizi ambayo yalitokea Tripoli na janga la vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kuanzia hapo, Jeshi la jenerali Haftar kutoka mashariki, jeshi alilolitengeneza kutoka jeshi la kitaifa la nchini Libya, likafanya mashambulizi katika mji mkuu.

Mamluki kutoka Urusi pia walivamia mji huo pia.

Maelezo ya picha,

Familia ya 'Kani Brothers' na simba waliowafuga kama wanyama wa nyumbani

Ndugu wa Kani 'Kani Brothers' gerezani

Ndugu wa Kani waliofahamika kama 'Kani brothers' walitawala mji huo kwa miaka kadhaa.

Katika makaburi ya mji huo, kulikuwa na mazishi ya watu 13 leo.

Wanaume na wanavulana wa mji huo wako hapa kwa kulazimishwa, walitembea wakiwa mamia baada ya swala ya Ijumaa, baadhi wakitumia mikeka yao ya kusalia kujifunika na jua la mchana.

Baada ya shughuli hiyo bwana Mahmoud alisema: "Walichukua familia yangu kutoka nyumbani kwao. Walikuwa raia wa kawaida tu. Mwaka 2020 mwezi Oktoba wapiganaji wa al-Kani walikwenda nyumbani kwao wakiwa na magari yanayomilikiwa na serikali, waliwachukua na kuwauwa."

Alitafuta familia yake kwa muda wa miezi 10 bila mafanikio yoyote. Mwili wa kwanza kuupata ulikuwa wa Hussin, Nuri na Mohamed. Miezi miwili iliyopita walipata mwili wa Esmail.

"Hata katika miaka 42 ya utawala wake, Gaddafi hakuwahi kufanya mauaji ya kinyama kiasi kile ambayo yamefanyika baada ya kuondoka madarakani. Kama raia wa Libya, hakuna mtu wa kutulinda, maisha yetu hayana ulinzi wowote ,"Bwana Mahmoud alisema.

Ndugu saba wa Kani, ambao walifahamika kwa simba wao watatu ambao waliwaiba katika hifadhi ya wanyama mjini Tripoli na kuwaweka kama wanyama wao wa nyumbani, wakati wa utawala wao.

Unyama walioufanya wanamgambo wa Kaniyat ulibadilisha mtazamo na kuweka pande mbili za vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya.

Utawala wao ulimalizika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka jana, wakati jeshi la serikali likiwa linasaidiwa na Uturuki lilivyoweza kufanikiwa kuchukua mji huo.

Uturuki ilituma vikosi saba vya majeshi ya majini ili kuliondoa jeshi la jenerali Haftar katika maeneo ya fukwe na kuleta maelfu ya wanajeshi kutoka Syria kupigana eneo la Idlib, Aleppo na Deir Ezzor.

Katika sura ya shambulio, ndugu wa Kani waliobaki na familia zao walikimbilia mashariki na hawafahamiki wako wapi.

Maelezo ya picha,

Mwili wa Esmail Mahmoud umebainiwa kwa nambari ya vipimo vya vinasaba

Mwili wa Esmail Mahmoud ulibainika kwa vipimo vya vina saba DNA namba: 051-000066

Makaburi ya Tarhuna ambayo yalifuata taratibu za utamadumi wa Kiislamu, yamezungukwa na miti mirefu huku baadhi ya makaburi yakiwa yamewekewa mawe upande wa kichwa.

Lakini kaburi la Esmail lilikuwa na namba : 051-000066.

Hii ilikuwa namba ya DNA yaani vinasaba kwasababu mwili unaozikwa leo unaweza kuwa sio wa Esmail.

Ni nguo zake tu ndio zilipatikana au kugundulika katika makaburi ya pamoja katika mji wa kusini.

Barabara ya kuelekea nyumba za shambani zilizungukwa na miti kukiwa na alama iliyoandikwa: "Hakuna kuingia, kamati ya waliopotea tu ndio wanaruhusiwa."

Ukiachana na nyumba ya shambani, kuna udongo mwekundu na vilima vidogo.

Kuna vingi ambavyo si rahisi kuhesabu, vingine vidogo na vingine vikubwa.

Ilikuwa siku ya Ijumaa ambapo hakuna kazi inafanyika na eneo lilikuwa kimya, lakini jitihada za kubaini uhalifu huo ukiwa kila eneo.

Kukiwa na alama ya bendera nyekundu kwa miili ambayo ilikuwa haijatambuliwa bado.

Wanaume, wanawake na watoto walikuwa wamezikwa hapa, kuna waliouawa na risasi moja kichwani, miili mingine ikiwa inaonekana wamejeruhiwa. Ardhi ya eneo hilo kuwa kavu imefanya miili iliyokuwa imewekwa kwa pamoja kuvimba na kuharibika.

Utambulisho wa Esmail utathibitishwa kama vipimo vya DNA vitafanana na matokeo ya maabara ya Tripoli. Mpaka sasa miili 140 ilibainika kwa mujibu wa mamlaka ya Jenerali wa Libya katika zoezi la kutafuta watu waliopotea.

Wamethibitisha kutambua miili 22 kwa kutumia vipimo vya vina saba yaani DNA.

Miili hiyo imekuwa kama kitu fulani kutoka shambulio la ajabu.

Kwa ujumla, watu 350 hawajulikani walipo katika mji huo, ingawa miili kutok amaeneo mengine imekuwa ikiendelea kuzikwa.

Kote nchini Libya, zaidi ya watu 6,000 wametangazwa kutojulikana walipo tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi. Ni watu 1,950 pekee ambao wamepatikana.

Mwisho wa eneo la makaburi, Ahmad Abdel-Mori Saad amesimama na yuko eneo hili kumzika rafiki yake. Mji wa Tarhuna ni mji wa mashetani, amesema.

"Nina ndugu saba ambao walitekwanyara na Kaniyat. Tayari tumeshazika wawili waliopatikana katika makaburi ya halaiki," amesema.

Bwana Saad hajui ndugu zake wengine wako wapi lakini anaamini wamefariki dunia. Ameachwa kuwa mwangalizi wa watoto wote, 24, kwa ujumla.

"Hatuna chama chochote cha kisiasa tunachofuata; sisi sio polisi wala wanajeshi … kama unapesa, unafariki dunia; ikiwa una ndugu watano wadogo, unafariki dunia, ukifanya mazungumzo na mimi, unafariki dunia; hauniungi mkono, unafariki dunia.

"Unafariki dunia bila sababu yoyote, yaani ni kifo bila sababu."