Rais Samia Suluhu Hassan afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri Tanzania

Chanzo cha picha, Habari Maelezo Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan afanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri Tanzania

Rais wa Tanzania Samia suluhu Hassan ametaja baraza jipya la mawaziri wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango.

''Nimefanya mabadiliko madogo ndani ya baraza la mawaziri na nitalitaja baraza ambalo nimelipanga hapa, zege hailali wanasema ni hapahapa,'' Alisema Rais Samia.

Kabla ya kuzungumzia mabadiliko ya baraza, Rais Samia alitangaza kuwa amefanya uteuzi wa wabunge watatu;

Balozi Dkt. Bashiru Ally kuwa mbunge, kabla ya uteuzi huo Dkt Bashiru alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Liberata Mulamula, na Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kuwa mbunge.

Na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Balozi Hussein Yahya Katanga ameteuliwa kushika nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi.

Mawaziri waliongia katika baraza jipya la mawaziri chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu ,Wizara ya Fedha ni Mwigulu Nchemba, ambaye anajaza nafasi ya Makamu wa Rais wa sasa Dkt Philip Mpango.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, pia amewahi kuhudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Palamagamba Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Mawaziri waliobadilishiwa wizara zao ni pamoja na Waziri Ummy Mwalimu aliyekuwa Muungano na Mazingira amehamishiwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na aliyekuwa kwenye wizara hiyo, Ofisi ya Makamu wa rais ni Selemani Jafo

Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ameteuiliwa Mohamed Mchengerwa, na aliyekuwa Waziri katika Wizara hiyo George Mkuchika, atabaki kuwa Waziri ndani ya Ofisi ya Rais kwa ajili ya kazi maalum.

Rais Samia amesema ameona afanye mabadiliko hayo kwa kuwa ni muda mfupi kufahamu nani kashindwa na nani amefanya vizuri katika eneo lake.