Je,Wanaume watakubali kutumia vidonge au njia za kupanga uzazi?

Hombre con una pastilla

Chanzo cha picha, Getty Images

Hadi sasa hakuna kidonge cha kupanga uzazi kwa wanaume , licha ya juhudi nyingi za hapo awali kukitengeza.

Utengezaji wa kidonge cha kupanga uzazi kilibadilisha ulimwengu wakati kilipoletwa katika jamii mnamo miaka ya 1960.

Hivi sasa, vidonge hivi hutumiwa na wanawake wapatao milioni 214 ulimwenguni kote na wana soko la kila mwaka karibu la Dola za Marekani milioni 18,000.

Hata hivyo, ingawa zaidi ya miongo sita imepita tangu "uwasilishaji rasmi" wa kidonge, kati ya orodha ya njia 20 za kupanga uzazi ambazo Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) inazo, ni mbili tu zinazoweza kutumiwa na wanaume.

Kwa nini hakuna kidonge cha kudhibiti uzazi kwa wanaume ?

Chanzo cha picha, Getty Images

"Wazo la kutengeza mpango wa uzazi kwa wanaume limekuwepo karibu kwa muda mrefu kama utengezaji wa mbinu ya upangaji uzazi kwa wanawake ," Adam Watkins, profesa wa biolojia ya uzazi katika Chuo Kikuu cha Nottinghan, aliiambia BBC World.

Kulingana na Watkins, changamoto kuu ya matibabu imekuwa kwamba, wakati mwanamke anatoa yai moja kwa mwezi, mwanaume hutoa mamilioni ya mbegu kila siku.

Hiyo ndiyo changamoto, kwamba hata kama mwanamume atapoteza 90% ya uwezo wake wa kuzalisha manii, bado ana rutuba, anasema mtaalam huyo.

Ingawa hii sio sababu kuu kwa nini kidonge chenye ufanisi na salama hakijatengenezwa.

"Nadhani ikiwa haijatengenezwa vyema imekuwa kwa sababu ya mafanikio ya kidonge cha upangaji uzazi kwa wanawake.

Inafanya kazi vizuri na ni bora sana kwamba, kwa mtazamo wa kiuchumi, kampuni nyingi za dawa hazihisi kuwekeza katika kidonge cha wanaume'

Chanzo cha picha, Getty Images

Mbinu mbili za upangaji uzazi kwa wanaume kwenye orodha ya WHO ni kondomu na vasektomi.

Kwa mtaalam, hii imesababisha kampuni za dawa kutowekeza katika utafiti na maendeleo ya miradi ambayo inasababisha mfano wa kidonge salama cha kupanga uzazi kwa wanaume .

"Kwa sababu tofauti, mzigo wa upangaji uzazi ulitwika wanawake .

Wao ndio wamekuwa wakiwajibikia jukumu hilo pekee yao hatua ambayo sio sawa'ameongeza msomi huyo.

Historia ya kidonge

Chanzo cha picha, Getty Images

Labda mpango wa uzazi wa zamani kabisa katika historia ni kondomu: kwani karibu miaka 2,000 kabla ya Kristo kuna kutajwa kwa njia hii ya kudhibiti uzazi iliyounganishwa na anatomia ya kiume, kupitia nyenzo ambayo huwa kama kizuizi cha mwili na kuzuia ujio wa manii kwenye yai.

Katika karne ya 18, hatua ya mwisho katika mchakato wa kutafuta mbinu ya kiume ya kupanga ilipatikana: vasektomi, utaratibu wa upasuaji ambao unakata ugavi wa manii kwa shahawa, kuanzia kuziba kwa kibiomba kidogo kwa jina 'vas deferens'.

Halafu, katika nusu ya pili ya karne ya 20, baada ya hatua kubwa kupigwa katika utengezaji wa kidonge cha wanawake ,safari ya kutengeza kile cha kutumiwa na wanaume ilianza Hivi sasa kuna sehemu mbili za utafiti katika uwanja huu.

Kwa upande mmoja, kupanga uzazi kutumia homoni, ambao hutegemea homoni bandia kusimamisha ukuaji wa mbegu za kiume kwa muda.

Kondomu ni moja wapo ya njia kongwe za upangaji uzazi

Chanzo cha picha, Getty Images

Na ya pili ni njia isiyo ya homoni, kwa kutumia mbinu zingine kuzuia mbegu za kiume zenye afya kuingia ukeni na kuweza kupandikiza.Hata hivyo , tafiti zinazolenga kukuza kidonge bora cha kiume zimeathiriwa na changamoto kama vile athari zinazosababishwa na viungo vyake.

Kwa mfano, mnamo 2016, utafiti ambao uliwadunga wanaume na testosterone na projestojeni, sawa na homoni zilizopatikana kwenye kidonge cha kike ulikomeshwa mapema . Ilibainika kuwa kulikuwa na athari kama vile chunusi kwenye ngozi, shida za mhemko na kuongezeka kwa libido, ambayo wanaume waliona ni kali sana na haiwezi kuvumilika, kwa hivyo uchunguzi ulifutwa.

"Walakini, wataalam wengi wanaweza kuona athari hizi kama ndogo ikilinganishwa na zile zinazopatikana kwa wanawake wanaotumia kidonge, pamoja na wasiwasi, kuongezeka uzani, kichefuchefu, maumivu ya kichwa, kupunguza libido na kuganda kwa damu."Kwa hili, wataalam wanasema, inaongezwa kuwa kondomu imeingizwa kama njia ya bei rahisi na isiyokuwa na athari.

"Kondomu pia haitumiki tu kwa uzazi, lakini pia kuzuia magonjwa ya zinaa," anasema Watkins.

Kondomu hutumiwa sana na wanaume, lakini haina ufanisi kama vidonge.

Tishio la nguvu za kiume

Hata hivyo kwa wataalam wengine wa afya ya uzazi, ni muhimu kwenda zaidi ya ukosefu wa hamu ya kampuni za dawa kusaidia katika utafiti na ugumu wa kibaiolojia wa kuunda kidonge cha kupanga uzazi cha wanaume.Kwa Dkt Lisa Campo-Engelstein, mkurugenzi wa Taasisi ya Maadili na Afya ya Binadamu katika Chuo Kikuu cha Texas na mtaalam wa utafiti wa siku zijazo za afya ya uzazi, kwamba hakuna kidonge cha kupanga uzazi kwa wanaume sio kushindw kwa sayansi kupata kidonge hicho.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Ni wazi kwamba kutokuwepo kwa kidonge cha wanaume cha kupanga uzazi sio kwa sababu ya suala la kisayansi, lakini kwa ajili ya suala la kijinsia, la kanuni za kijamii. Kazi hii ilikuwa ya wanawake tu," Campo-Engelstein anaiambia BBC."Siku hizi , wanawake hubeba mzigo mkubwa wa kifedha na kiafya unaohusiana na upangaji uzazi. Kwa ujumla, njia za kike huwa za bei ghali zaidi kuliko za kiume kwa sababu nyingi zinahitaji kumuona daktari zaidi ya mmoja na nyingine zinahusisha dawa zinazofaa kumezwa kwa kipindi fulani. Kwa kweli, mtaalam huyo anaonyesha katika nakala yake "Kwanini panafaa kuwa na kidonge cha upangaji uzazi kwa wanaume na huko Amerika, mipango mingi ya bima ya afya haitoi upangaji uzazi Ndio kwa sababu Campo-Engelstein anatoa wito mkubwa wa kuwepo kidonge cha kupanga uzazi kwa wanaume hivi karibuni. "Wanawake wengi wanataka kuacha kunywa kidonge kwa sababu ya nguvu na athari za homoni kwenye mwili wao, lakini mara nyingi hawafanyi hivyo kwa sababu mwanamume hutumia kondomu tu, ambayo haifanyi kazi kwa 100%," anasema msomi huyo. "Lakini Iwapo hakuna mabadiliko katika mitindo ya kawaida ya majukumu ya kijinsia kuhusiana na upagaji uzazi huenda wanaume hawatatumia njia hizo kwa kiwango sawa na wanawake hata Iwapo njia na vidonge vya kuafikia upangaji uzazi kwao vipatapatikana' anatamatisha daktari huyo.