Mabadiliko ya tabia nchi Uganda: Watu wakabiliwa na tisho la barafu inayoyeyuka milimani

A hiker looking over to the summit of Margherita Peak, Rwenzori.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Barafu na theluji juu ya milima ya Rwenzori, iliyokuwa ikionekana mwaka 2016, imeanza kuyeyuka

Ronah Masika anakumbuka nyakati alikuwa aakijionea theluji ikifunika milima ya Rwenzori, eno la urithi wa dunia lilitambaliwa na Shirika la Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa Unesco, katika mpaka kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Muenekano wake ulikuwa wa kupendeza sana kila wakati alipozuru eneo hilo kutoka nyumbani kwao mjini Kasese kuelekea mji mkuu wa Uganda, Kampala - na haikuwa kitambo hivyo.

Lakini sasa hawezi kuona barafu kwasababu inayeyuka kila uchao.

Na sasa muonekano wa eneo hilo umebadilika.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jamii zinazoishi chini ya milima ya Rwenzori zinakabiliwa na mafuriko na ukame

Bi Masika anakumbuka nyanya yake alikuwa akikima maharage kulisha familia yake, na zingelitumika hadi msimu mwingine wa upanzi na mavuno ya mimea.

"Ssa mimi na watu wengine tonaona vigumu kujikimu kwa mazao tunayopanda nyumbani, kwasababu zinaharibiwa na mafuriko au ukame. Inaweza kuwa ukame wa muda mrefu au mvua byingi kupita kiasa.

"Inanitia hofu sana, nikifikiria jinsi kizazi kijacho kitakavyoathiriwa na hali hii siku zijazo," anasema Bi Masika, ambaye sasa anajishughulisha na mradi wa kupunguza athari za mazingira yanayobadilika.

Mabadiliko ya tabia nchi inaathiri mlima Rwenzori kwa njia tofauti.

Athari inayoonekana bayana ni ya kupotea haraka kwa barafu milimani, amnayo imepungua katika eneo la kilomita 6.5 mraba mwaka 1906 hadi chini ya kilomita moja mraba mwaka 2003, na huenda ikatiweka kabisa kabla ya mwisho wa muongo huu, utafiti unaonesha.

Mwaka 2012, moto wa misitu ulifikia mwinuko zaidi ya mita 4,000, hali ambayo haikushuhudiwa zamani, na kuharibu mimea ambayo ilidhibiti mtiririko wa mito kuelekea chini.

Tangu wakati huo, jamii zinazoishi chini ya mlima Rwenzori zimeathiriwa na mafuriko mabaya kuwahi kushuhudiwa ikiambatana na viwango vya chini vya mvua ambayo ikinyesha inakuwanyingi kupita kiasi.

Chanzo cha picha, Kisa Kasifa/ CCFU

Maelezo ya picha,

Mafuriko makubwa yaliyoshuhudiwa mwezi Mei mwaka 2020 yaliharibi nyumba karibu 25,000

Mwezi Mei mwaka uliopita, mito mitano katika eneo hilo zilivunja kingo zake kufuatia mvua kubwa iliyonyesha. Maji yalimiminika kutoka milimani na kusomba kila kitu ikiwa ni pamoja na nyumba na shule katika mji wa Kalembe.

Karibu nyumba 25,000 ziliharibiwa na watu 173,000 kuathiriwa.

Japo sayansi huenda ikatoa ufafanuzi wa matukio haya, utamaduni wa wakazi wa eneo hilo wanaufafanuzi wao wenyewe - kulingana na na imani yao, majanga kama hayo hutokea kwasabu miungu ina hasira.

"Bakonzo wana uhusiano mkubwa sana na theluji na maji," anasema Simon Musasizi, msimamizi wa programu katika wakfu wa tamaduni mbalimbali nchini Uganda (CCFU).

"Wanaamini mungu wao, Kithasamba, anaishi kwenye theluji, na kwamba theluji ni mbegu za uzazi zilizohifadhiwa za mungu wao."

Map

Jina Rwenzori linatokana na na neno rwe nzururu, linalomaanisha "eno la theluji" kwa lugha ya Bakonzo. Kuna miungu 30 inayohusishwa na maliasili tofauti zinazoishi mlimani, kulingana na kosmolojia ya Bakonzo.

Lakini ukataji misitu na ongezeko la haraka la idadi ya watu katika eneo takatifu la milima, pamoja na kuyeyuka kwa barafu ni vitu vinavyobadilika.

Wakati wa mafuriko ya mwaka jana, maji yaliziba eneo la chimi chemi na kusomba mimea karibu na mteremko wa maji ambayo yalitumika kama sehemu ya kufanyia matambiko. Tangu wakati huo, viongozi wa kiroho wameshindwa kufanya matambiko hayo.

Maeneo mengine takatifu pia yameharibiwa huku uharibifu wa misitu ukichangi akudhoofisha kingo za mito katika meneo mengi.

Vyote hivi vinatishia karne za- mila za zamani.

"Huenda, baadhi ya tamaduni hizi zikapotea pole pole hadi zakatokomea kwasababu ya mabadiliko haya ," Bw. Musasizi.

Chanzo cha picha, Kisa Kasifa/CCFU

Maelezo ya picha,

Miteremko ya maji ya Ekisalhalha Kya Kororo imeharibiwa na mafuriko ya hivi karibuni

Jamii ya Bakonzo inajumuisha watu milioni moja wanaoishi pande zote za mpaka kati ya Uganda na DR Congo, na utamaduni wao unaweza kupotea kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

"Athari za matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa ni mabaya sana katika maeneo ya tropiki," anasema Richard Taylor, mtaalam wa jiografia katika Chuo Kikuu cha London, ambaye ameongoza utafiti juu ya Milima ya Rwenzori.

Profesa Taylor, ambaye pia aliongoza safari kutoka 2003 hadi 2007 kupima mabadiliko katika barafu za Rwenzori, anasema upotezaji wa uwanja wa barafu katika maeneo ya tropiki ni ishara ya visa vya ongezeko la kiwango cha joto duniani.

Kuhifadhi na kulinda maeneo yalioathirika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ni hatua muhimu katika juhudi za kutunza maeneo ya turathi za kale.

Chanzo cha picha, Kisa Kasifa/CCFU

Maelezo ya picha,

Uelewa wa jamiiya Bakonzo kuhusu mazingira umechangi akubuniwa kwa baadhi ya sera za mazingira kukabiliana mabadiliko ya hali ya hewa

Licha ya kuanzisha na mradi wakufanya hilo, Bw. Musasizi anasema wamefikia makubaliano na jamii zinazoishi katika eneo hilo kuhusu aina ya miti inayostahili kupandwa katika kingo za mito, ikiwebo myanzi na miti mingine asilia.

Bi Masika, ambaye kazi yake ni kushirikiana na wakazi wa eneo hilo, anasema watu tayari wana majibu ya matatizo yanayowakabili

"Kwa mfanno wanajua ni mimea ya aina gani inastahili kupandwa milimani. Wanajua ni miti gani imara zaidi kupanda kando ya mito ili kuzuia mafuriko.

"Wanafahamu kuwa wanatakiwa kupanda mimea kando ya kingo za mito kwasababu chakula kwa miungu wa majini. Na wakati mungu wa maji, ameridhirika hasababishi mafuriko.

Chanzo cha picha, Kisa Kasifa/CCFU

Maelezo ya picha,

Chemi chemi ya maji ya Embugha au Rwagimba zinaaminika kuwa na uwezo wa uponyaji kimwili na kiroho, hasa magonjwa ya ngozi