Bung'eda: Mazishi ya kushangaza ya jamii ya Wabarbaig Tanzania

Bung'eda: Mazishi ya kushangaza ya jamii ya Wabarbaig Tanzania

Jamii ya wa Wabarbaigi ama Wadatoga wa Tanzania wana namna ya kushangaza ya kuwazika watu wanaoamini waliishi Maisha ya kupendeza ndani ya jamii yao, Ikiwa jamii itaridhia marehemu alikuwa ni mtu mwema basi atapewa heshima ya mazishi haya maalumu.

Mwili wa marehemu huviringishwa kwenye Ngozi mbichi ya ngo’mbe mweusi ambaye hunyongwa hadi kufa na nyama ngo’mbe huyu hutupwa msituni, Mwili wa marehemu hukalishwa ndani ya kaburi lenye umbo la duara na baada ya kufukiwa kaburi lake hujengwa kwa udongo na fito hatua kwa hatua kwa kipindi cha miezi tisa.