Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 07.04.2021: Aguero, Konate, Lingard, Lacazette, Sabitzer, Walcott

City Sergio Aguero

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 32

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 32, anataka kupandisha chati ya ufungaji Ligi ya Primia, hatua ambayo inaweza kusaidia Chelsea katika azma yao ya kumsajili Muajentina huyo wakati mkataba wake unamalizika msimu wa joto. (Evrning Standard)

Aguero yuko tayari kukosa ligi ya mabingwa msimu ujao ili asalie ligi ya primia huku Chelsea na Tottenham zikiwa miongoni mwa vilabu atakavyovifikiria. (Telegraph)

Manchester United inaweza kujiunga na Liverpool katika mbio za kupata sahihi ya mlinzi wa kati wa RB Leipzig Ibrahima Konate. Mchezaji huyo,21 anatarajiwa kugharimu kiasi cha takribani pauni milioni 34. (Eurosport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester United huenda ikajiunga na Liverpool kumsaka Ibrahima Konate wa RB Leipzig

West Ham itajaribu kumsajili kiungo wa kati Jesse Lingard kwa mkataba wa kudumu msimu huu, lakini wanahofia Manchester United watataka dau la juu kumuachia mchezaji huyo mwenye miaka 28. (Mail)

Arsenal itafikiria kumuuza mshambuliaji wa Kifaransa Alexandre Lacazette katika dirisha la usajili katika majira ya joto. Inter Milan, Roma, Sevilla na Atletico Madrid zinataka kumnyakua mchezaji huyo mwenye miaka 29. (90min)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Arsenal itafikiria kumuuza mshambuliaji wa Kifaransa Alexandre Lacazette(Kushoto)

Tottenham wanajiandaa na uhamisho wa kiungo wa kati wa RB Leipzig Marcel Sabitzer,27. (Football Insider)

Juventus, Arsenal na Chelsea wanamtolea macho kiungo wa kati wa AC Milan, Mturuki Hakan Calhanoglu, 27, ambaye anaweza kupatikana kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu. (Sky Sports-in Italian)

Mshambuliaji wa Villarreal Gerard Moreno, 28 ni miongoni mwa wachezaji muhimu msimu huu-hata hivyo gharama ya uhamisho ya Mhispania huyo ni pauni milioni 85.6 (Marca-in Spanish)

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha,

uventus, Arsenal na Chelsea wanamtolea macho kiungo wa kati wa AC Milan, Mturuki Hakan Calhanoglu

Mshambuliaji Theo Walcott,32, atajiunga na Southmpton kwa mkataba wa kudumu , mara mkataba wake wa kucheza kwa mkopo Everton utakapokwisha (Talksport)

Everton itahitaji kiasi cha pauni milioni 21.4 ikiwa watamuuza mlinzi wa kati Yerry Mina (Team Talk)

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amemtaka mshambuliaji Ousmane Dembele,23, kusalia kwenye klabu hiyo, ingawa Manchester United imeonesha nia ya kumnyakua mchezaji huyo. (Metro)

Chanzo cha picha, Reuters

Manchester City inamtolea macho kiungo wa kati wa Sheffield United Sander Berge,23,wakati wakitafuta mbadala wa kiungo wa Brazil Fernandinho,35, (Voelbal24-in Dutch)

Baba wa kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira ameitaka Arsenal kumruhusu mchezaji huyo, 25, anayecheza kwa mkopo Atletico Madrid, kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu.