Jinsi rubani alivyokwepa nyoka na mamba kwa siku 36 katika msitu mnene wa Amazon

Antonio with the people who rescued him

Chanzo cha picha, Antonio Sena

Maelezo ya picha,

Antonio na wakulima ambao walisaidia kumuokoa

Akiwa amepotea na yuko peke yake katika moja ya eneo la msitu mzito zaidi nchini Brazil, Antonio Sena alijua anachokogiopa: "Wanyama wakali katika msitu wa Amazon - chui, mamba na nyoka wakubwa aina ya anakonda."

Lakini rubani huyo, 36, sio tu kwamba alihofia kuwa mlo ujao wa wanyama wa mwituni, pia alihitajika kutafuta chakula na makazi.

Ilikuwa jukumu kubwa sana kwake huku akihofia kwamba baada ya ndege kupata ajali, igemchukua siku kadhaa tu kuokolewa.

Kile ambacho Antonio hakukijua ni kwamba angepigania maisha yake kwa zaidi ya mwezi akiwa peke yake huku njaa na yao ikimkabili vilivyo.

Kuanguka kwa ndege

"Mayday, mayday, mayday… Papa, Tango, India, Romeo, Juliet ana anaanguka…" huo ndio ujumbe wa mwisho wa Antonio wakati ndege inaanguka.

Ndege ambayo alikuwa anaendesha peke yake mnamo mwezi Januari, ilikuwa kwenye matatizo.

"Ghafla injini ikaacha kufanyakazi ikiwa umbali wa mita 900. Nikalazimika kutua katikati ya jangwa," alisema, akizungumza na BBC World Service.

Ndege ikaanguka katika ya miti msituni lakini kwa miujiza ya Mwenyezi Mungu akafaulu kutua salama, kaskazni mwa mto Amazon.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ndege ya Antonio ilianguka kaskazini mwa mto Amazon

Lakini kuepuka kifo haikumaanisha kuwa matatizo yameisha, hapana, ndio mwanzo yalikuwa yanaanza.

"Sikuwa na budi zaidi ya kuondoka kwasababu nilijua niko mahali hatari sana," amesema.

Kwasababu hakuweza kuitumia ndege ile kama makazi yake ya muda, akasonga sehemu iliyo karibu akiwa na imani kwamba ujumbe wake wa mwisho umesikika na kuwa usaidizi unawadia.

"Nilichukua chochote nilichokiona ambacho kingenisaidia kuwa hai siku kadhaa zijazo."

"Wakati huo nikaanza kufikiria kwamba ningekuwa jangwani katika ya msitu kwa siku 5 hadi 8 muda ambao kawaida huwa unatumika katika shughuli ya uokozi na."

Lakini wiki moja ikapita bila kupata usaidizi wowote.

'Kuondoka msituni nikiwa peke yangu'

Antonio akaamua kwamba ikiwa atakuwa tayari kukutana tena na wapendwa wake itamlazimu aondoke kwenye eneo ndege ilipodondoka na ajaribu kutembea kutafiuta eneo salama.

"Nilibaini kwamba hawakuwa wameniona na sikuwa na namna nyingine zaidi ya kuondoka eneo hilo na kutafuta familia yangu."

Ilipofika asubuhi, akatumia mwanga uliochomoza kumuongoza kutoka eneo hilo: "Nikaamua kutoka na kuelekea upande wa mashariki, nikifuata jua, na nikawa ninatembea kila asubuhi kwa karibu saa mbili na nne."

"Na baada ya hapo - nikawa naanza kufikiria sehemu ya kulala na kutayarisha moto."

Ingawa msitu wa Amazon ni hatari kupita maelezo lakini ghafla mtu akajiona akiwa peke yake na bila mawasiliano, Antonio alikuwa amejifunza mbinu kadhaa ambazo zingemwezesha kunusurika.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mamba ni wanyama ambao Antonio aliwaogopa zaidi

"Nilikuwa nimemaliza kozi ya kuishi jangwani kwasababu ya kazi yangu."

"Pia mimi mwenyewe nilizaliwa na kuishi Amazon."

Na alikuwa amechukua muda wake kujifunza kutoka kwa watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini ya msituni - taarifa ambazo kipindi hicho zilimaanisha kuendelea kuwa hai au kufariki dunia.

"Kila wakati nilipopata muda nilipenda kuzungumza na watu wanaoishi maeneo hayo, kuna mengi unayoweza kujifunza kutoka kwao."

Kutafuta chakula

Mbinu ya kwanza aliyohitaji Antonio kuishi ni namna ya kupata chakula na alichofanya ni kuwinda wanyama anaoweza kula.

"Kulikuwa na tunda ambalo sikuwa nimewahi kuliona lakini nikaona tumbiri wakilila," anasema. "Nikafikiria ikiwa tumbiri wanaweza kula tunda hili basi pia mimi naweza kulila."

Pia alikutana na mmea wa kakao mara kadhaa lakini alitaka kitu zaidi ya tunda.

"Mayai ya nandu ," yalikuwa yametagwa na "ndege ambaye ni maarufu katikati ya jangwa," anasema.

Kuepuka kutoliwa na wanyama

Ingawa alikuwa anapata chakula chake kinachomwezesha kuwa hai, pia alihitajika kujikinga dhidi ya wanyama wanaoweza kumfanya nyama na kumla.

"Kila niliposimama na kutayarisha sehemu ya kulala, ilikuwa ni juu ya mlima," anasema.

"Kwasababu chui, mamba na anakonda wana uhusiano wa karibu na maji, Kwahiyo, sikuwahi kuishi kandokando ya vyanzo vya maji."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Anaconda ni nyoka wakubwa zaidi wanaopatikana Amazon

Antonio pia alikuwa makini sana asifanye fujo wakati anatembea katikati ya msitu.

Alijua kuwa wakati wa mchana, kuna uwezekano mkubwa wa kuvamiwa na wanyama ambao angewatia hofu wala sio na wale ambao angewasikia yeye wanakuja.

Hatimaye akapata matumaini

Ingawa mbinu za Antonio zilikuwa zinamfanyia kazi, uzito wa mwili upungua kweli.

Wiki kadhaa zilikuwa zimepita tangu ndege ilipoanguka.

Lakini baada ya siku 36, hatimaye akakutana na kundi dogo la watu.

"Baada ya kipindi chote hicho nikiwa napita milima, mabonde na mito, nilikutana na kundi dogo la watu wa Brazil waliokuwa wanakusanya njugu katika eneo lililojitenga," amesema.

Mara ya kwanza sikuwa nimewaona, lakini nikafuata sauti zilizokuwa ninazisikia.

Niliwasikia wakifanya kazi zao. "

Na hatimaye, safari yake ikawa inafika mwisho.

"Kilichonipatia hamasa na nguvu ya kuendelea na safari licha ya maumivu na njaa ya ajabu niliyokuwa nayo, ilikuwa ni hamu na nia ya kuona familia yangu."

"Na baada ya kuondoka msituni na hatimaye nikakutana nao uwanja wa ndege, huo ulikuwa ni muda ambao sitaweza kuusahau maishani mwangu.

Ndege na helikopta zilitumwa kumtafuta lakini zilisitisha operesheni yao wiki kadhaa kabla.

"Kila wakati nilikuwa nafikiria familia yangu, kila wakati."