Mzozo wa Mto Nile: Je, mzozo wa Ethiopia, Misri na Sudani kuishia wapi?

Bwawa la Reinnesance nchini Ethiopia linapingwa na Misri na Sudani

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Bwawa la kufua umeme la Reinnacence nchini Ethiopia limezaa mgogoro baina ya nchi hiyo na Misri na Sudani.

Jaribio la rais wa DR Congo na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Felix Tshisekedi kuzipatanisha nchi za Misri, Sudan na Ethiopia kuhusu mzozo wa mto Nile limefeli siku ya Jumatano na kurejesha nyuma kabisa jitahada za kupata mwafaka kuhusu jinsi mataifa hayo yatavyomaliza malumbano ya kutumia maji ya Nile .

Ethiopia imjenga Bwa kubwa litakalotegemea mto Nile ili kuzalisha kawi na kuendeleza kilimo lakini Misri inasema bwawa hilo linahatarisha kiwango cha maji kitakachofika Misri nan chi jirani ya Sudan.

Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi anasema kuwa Misri inaheshimu hamu ya Ethiopia ya kujiendeleza kupitia maji yake ya Mto Nile, mradi masilahi ya maji ya Misri hayatatizwi.

El Sisi hata hivyo anaishtumu Ethiopia kwa kujaribu kupendekeza jambo ambalo haliwezekani kwa kusimama kidete kwamba lazima itajaza bwawa lake hilo na ahajachelea kuashiria kwamba Misri iko tayari kuchukua hatua yoyote kuyalinda maslahi yake - hatua inayoashiria uwezekano wa nchi hizo kujipata katika mgogoro wa kivita kuhusu maji ya Nile.

Akitoa hotuba yake katikati ya wiki El Sisi alionekana kuashiria kwamba Masiri bado ingali ipo wazi kwa majadiliano ya kupata suluhu la kudumu kwa mzozo huo lakini pia msimamo wake utawakanganya wengi wanaofuatilia suala hilo kwani alongeza kwamba kutakuwa na 'Athari' ambazo hakuzitaja iwapo maslahi ya Misiri katika Mto Nile hayatazingatiwa katika mwafaka utakaopatikana.

Mzozo huo kati ya Misri na Ethiopia pia umeiingiza Sudan katikati na waziri wa Unyunyuziaji Maji Mashambani Yasser Abbas amesema nchi yake itaamua kuchukua hatua kali ili kulinda usalama wake baada ya kufeli kwa raundi ya hivi karibuni ya kutafuta suluhisho la mzozo huo wa Mto Nile

waziri huyo amesema ' kila chaguo liko wazi' mezani ili kukabiliana na mzozo huo ikiwemo kwenda katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Waziri huyo aliishutumu Ethiopia kwa kusababisha kutofaulu kwa duru hiyo ya mazungumzo, baada ya kukataa mapendekezo yote yanayohusiana na kuwezesha mchakato wa mazungumzo

Abbas alielezea kuwa wizara yake imeweka hatua za kiufundi kutarajia hatua ya Ethiopia kujaza bwawa la Renaissance bila kufikia makubaliano, akibainisha kuwa idadi ya maji itatengwa nyuma ya mabwawa kadhaa ili kukabiliwa na uhaba wowote wa maji wakati wa majira ya joto.

Chanzo cha picha, EPA/MAXAR TECHNOLOGIES

Maelezo ya picha,

Ethiopia kwa sasa inaendelea kulijaza maji bwawa la Reinnacence.

Aliongeza kuwa sekta kadhaa zitaathiriwa ikiwa Ethiopia itajaza hifadhi ya bwawa bila makubaliano, pamoja na sekta ya kilimo, umeme na maji ya kunywa.

Waziri wa Maji wa Ethiopia, Slichi Bakli siku ya Jumatano, kwamba nchi yake inaendelea na mchakato wa kujazwa kwa mara ya pili kwa Bwawa la Renaissance, siku moja baada ya Misri, Sudan na Ethiopia kutangaza kutofaulu kwa mazungumzo kati yao.

Bagli pia alisisitiza kujitolea kwa nchi yake kubadilishana habari juu ya mchakato wa kujaza bwawa hilo.

Hilo lilijiri wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika na Bakli huko Addis Ababa kutoa maoni juu ya mazungumzo ya Kinshasa kuhusu Bwawa la Grand Renaissance la Ethiopia, ulioandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.

Bakli alisema, "Ujazaji wa pili utafanywa kwa wakati, kulingana na kile kilichopangwa," na kwamba nchi yake iko tayari kuondoa wasiwasi wa Sudan juu ya hilo.

Aliendelea, "Tulikuwa tumeafikia makubaliano ya kumaliza mazungumzo katika raundi inayofuata, na msukumo wa Sudan wa upatanishi haupatani na tangazo la makubaliano ya kanuni.

Chanzo cha picha, Reuters

Hii inakuja kufuatia matamshi ya Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi, kwamba kusisitiza kwa pande nyingine kuanzisha miradi mikubwa ya kutumia mito ya kimataifa kwa njia mbaya na bila kuzingatia umuhimu wa kuhifadhi usalama endelevu wa vyanzo vya maji unatishia mustakabali wa watu wa eneo hili na kuathiri usalama wao

Wakati wa hotuba yake, Sisi alitoa ofa ya kuandaa kikao kijacho cha Mkutano wa Vyama husika vya Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabianchi.

Jumanne, Misri ilitangaza kutofaulu kwa duru ya mazungumzo ya Bwawa la Renaissance, ambayo yalifanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na ushiriki wa Misri, Sudan na Ethiopia.

Kila nchi inaishtumu nyingine

Ethiopia ilishutumu Misri na Sudan kwa kuzuia mazungumzo juu ya Bwawa la Grand Rianissance la Ethiopia kwenye Mto Nile, ambalo lilimalizika kwa mashtaka ya pande zote na hatua chache kupigwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia ilisema, katika taarifa kwenye Twitter, kwamba mkutano huo ulishindwa "kwa sababu ya msimamo mkali wa Misri na Sudan katika kufanya mazungumzo na matokeo kuwa chombo cha kudhibitisha sehemu yao ya maji na kuhifadhi sehemu ya Ethiopia'.

"Nchi hizo mbili zimechukua mkakati ambao unatafuta kudhoofisha mchakato unaoongozwa na Umoja wa Afrika," iliongeza taarifa hiyo, na kuongeza kuwa Misri na Sudan zilitaka kuchelewesha na "kuzuwia mchakato" kwa kukataa rasimu ya taarifa hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais El Sisi amesema hakuna mtu atakayeruhusiwa kuchukua hata tone moja la maji ya Misri

Ethiopia ilisema itaendelea na awamu ya pili ya kujaza hifadhi ya bwawa kama ilivyopangwa wakati wa msimu ujao wa mvua Na nchi hiyo ilitangaza Julai iliyopita kwamba ilikuwa imefikia lengo lake katika mwaka wa kwanza wa kujaza, ambayo ilikasirisha Misri na Sudan.

Walakini, Wizara ya Mambo ya nje ya Misri ilitaja kufeli kwa mazungumzo hayo kwa kile ilichoelezea kama kutokujali kwa Ethiopia na kukosekana kwa dhamira ya kisiasa ya kufanya mazungumzo kwa nia njema. Misri ilikuwa imeelezea mazungumzo ya Kinshasa kama nafasi ya mwisho kuafikia makubaliano baada ya Rais Abdel Fattah El -Sisi kusema wiki iliyopita kwamba kanda hiyo inakabiliwa na "kutokuwa na utulivu usioweza kudhibitiwa " kuhusu mradi huo.

"Hakuna mtu atakayeruhusiwa kuchukua hata tone moja la maji ya Misri," alisema.

Jumanne, Waziri wa Mambo ya nje wa Sudan, Maryam Al-Sadiq Al-Mahdi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Ethiopia "inatishia moja kwa moja watu wa Bonde la Mto Nile na Sudan kwa jumla.'

Aliongeza, "Tunatumai kuwa uamuzi wa Rais Tshisekedi utaweza kumaliza ... mazungumzo haya yasiyokwisha na yasiyotosha ambayo upande wa Ethiopia unamweka kila mtu mbele ya mshtakiwa, kwa njia ambayo inakiuka sheria za kimataifa na kanuni za ujirani mwema.

Nchi hizo mbili zilizo chini ya mkondo wa mto Nile Misri na Sudan, zinashikilia kwamba ujenzi wa Bwawa la Renaissance la Ethiopia ambalo linatarajiwa kuwa mradi mkubwa zaidi wa umeme barani Afrika, ni tishio kwa usambazaji wao wa maji.

Ethiopia inasema nishati itakayozalishwa na GERD itakuwa muhimu kukidhi mahitaji ya maendeleo ya watu wake milioni 110. Lakini Misri na Sudan zinahofia kwamba hali ya maisha ya nchi zao ipo hatarini.