Mzozo wa Israel na Palestina: Ramani sita zinazoonesha jinsi eneo la Palestina lilivyobadilika

Tanque con la bandera de Israel (foto de archivo)

Chanzo cha picha, Reuters

Zaidi ya miaka 70 baada ya taifa la Israel kutangazwa , mipaka katika eneo hilo haijafafanuliwa .

Vita, mikataba na ukaliaji wa maeneo yamebadilisha mipaka ya kile kilichojulikana kuwa koloni ya Uingereza ya Palestine.

Katika picha hizi sita tunaelezea mabadiliko ya mipaka ya eneo hilo karibia karne moja sasa.

Eneo ambalo lilibadilika likawa Israel kwa karne kadhaa lilikuwa chini ya miliki ya tome.

Baada ya vita ya kwanza ya dunian na kuanguka kwa ufalme huo, eneo hilo lilijulikana kuwa Palestine ambayo upande wake wa magharibi wa mto Jordan ulijukana kuwa ardhi ya Waisraeli ya Wayahudi iliokabidhiwa Uingereza..

Masharti ya mamlaka hayo yalikabidhi Waingereza kuanzisha "Taifa la Israel la Wayahudi huko Palestina , ili mradi iwapo kuchukua hatua hiyo hakutaumiza haki za kiraia na za kidini za jamii zisizo za Kiyahudi zilizopo.

Kuongezeka kwa utaifa wa Waarabu wa Palestina, pamoja na ukuaji wa haraka wa idadi ndogo ya Wayahudi wa Palestina - haswa baada ya ujio wa Wanazi katika miaka ya 1930 - ulisababisha kuongezeka kwa vurugu kati ya vikundi hivyo viwili.

Waingereza walipeleka tatizo hilo kwa Umoja wa Mataifa, ambao mnamo 1947 ulipendekeza kugawanya Palestina katika majimbo mawili, moja la Kiyahudi na jingine la Kiarabu, na eneo la Jerusalem-Bethlehem likageuzwa kuwa mji wa kimataifa.

Mpango huo ulikubaliwa na uongozi wa Kiyahudi wa Palestina, lakini ulikataliwa na Waarabu.

Uongozi wa Kiyahudi huko Palestina ulitangaza kuanzishwa kwa Jimbo la Israeli mnamo Mei 14, 1948, wakati ambapo utawala wa Uingereza iulikuwa umekwisha, ingawa haikutanagaza mipaka yake.

Siku iliyofuata, Israeli ilivamiwa na majeshi matano ya nchi za Kiarabu, ikiashiria mwanzo wa vita vya Kiarabu na Israeli, vilivyojulikana miongoni mwa Waisraeli kama vita vya uhuru.

Vita hivyo vilimalizika mnamo 1949 huku makubaliano yaliowekwa yakitengeneza fursa za kushika silaha katika mipaka ya Israeli na majimbo jirani na kuunda mipaka ya kile kilichojulikana kama Ukanda wa Gaza (ulichukuliwa na Misri) na Yerusalemu. Ukingo wa Mashariki na Magharibi (ulichukuliwaa na Jordan).

Nchi jirani za Kiarabu zilikataa kuitambua Israeli, na kuacha mipaka yake bila kuthibitika.

Mabadiliko makubwa katika mipaka ya eneo hilo yalitokea mnamo 1967, wakati mzozo unaojulikana kama Vita ya Siku Sita vilipoisha huku Israeli ikinyakua rasi ya Sinai, Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, Jerusalem Mashariki na sehemu nyingi za Nyanda za Ju una milima ya Golan nchini Syria, hatua ilioifanya Israel kudhibiti mara tatu ya ukubwa wa eneo lililokuwa chini ya udhibiti wake.

Vitendo hivi havikutambuliwa na jamii ya kimataifa, hadi Marekani ilipobadilisha msimamo wake rasmi juu ya jambo hilo chini ya serikali ya Donald Trump, na kuwa taifa la kwanza lenye uwezo mkubwa kufanya hivyo.

Kwa wingi, jamii ya kimataifa inaendelea kutambua mashariki mwa Jerusalem na milima ya Golan kama maeneo yaliokaliwa.

Mpaka wa kwanza wa ardhi ya Israel ulitambuliwa rasmi 1979, wakati Misri ilipokuwa nchi ya kwanza ya KIarabu kulitambua taifa hilo la.

Chini ya makubaliano hayo, mpaka uliopo kati ya mataifa hayo mawili uliwekwa na Israel ikaamua kuondoa wanajeshi wake na walowezi kutoka rasi ya sinai mchakato uliokamilika 1982.

Hatua hiyo iliifanya Israel kukalia ukanda wa Gaza , mashariki mwa Jerusalem, milima ya Golan huku mipake yake ikiwa bado haijafafanuliwa na makubaliano ya mipaka ya 1949.

Mwaka 1994, Jordan ilikuwa nchi ya pili ya Kiarabu kuitambua Israel , likiendelea kuweka rasmi mipaka yake mirefu na taifa hilo la Kiyahudi. Ijapokuwa mpaka kati yake na Syria haujatatuliwa rasmi.

Vivyo hivyo, Israeli imekuwa na mpaka rasmi na Gaza tangu ilipoondoa wanajeshi wake na walowezi mnamo 2005, lakini UN inachukulia Gaza na Ukingo wa Magharibi kuwa eneo moja, na mipaka rasmi haijaamuliwa.

Hali ya mipaka ya West Bank, Gaza na mashariki mwa jerusalem inapaswa kuamuliwa katika majadiliano kati ya Israel na WaPalestina wanaoishi chini ya usimamizi wa Israel, lakini mazungumzo mengi yaliofanyika hayajazaa matunda.