Dola bandia zilizotumika kwa miongo miwili na kupumbaza dunia

fedha bandia

Noti hiyo ya dola bandia haikuwa na makosa yoyote na hata maafisa wa kitengo cha ujasusi hawakuweza kubaini iwapo ilikuwa dola bandia ama nakala mbele yao.

Ni baada ya kipindi kirefu cha uchunguzi ndiposa waliweza kuthibitisha kwamba zilikuwa hela bandia.

Lakini noti hizo za dola mia moja zilikuwa hazina dosari yoyote hadi zikapewa jina ''The Super fake Dollars''.

Zilikuwa na rangi kama ile ya noti halisi za dola za Marekani.

Pia zilichapishwa katika karatasi iliokuwa sawa na ile ya pesa halisi ikiwa na robo tatu ya pamba na robo ya kitani{linen}.

Picha ya noti hizo ilikuwa safi zaidi ya zile zilizochapishwa na shirika la kuchapisha fedha Marekani.

Chanzo cha picha, IMAGE SOURCE,KIRILL KUKHMAR

Maelezo ya picha,

Mashine ya kuhesabu noti katika benki pia zilishindwa kubaini uhalisia wake

Zilikuwa na tofauti kidogo sana, wakati Gazeti la The New York Times liliporipoti kwamba fedha hizo hazikuwa halisi.

Marekani ilishangazwa kwamba fedha bandia ziliweza kupita benki zake bila kujulikana , kwasababu hakuna aliyeweza kubaini tofauti.

Fedha hizo za Super Dollars zilisambaa kote dunini kati ya miaka 1990 na 2000.

Wakati wa miaka hii , Marekani iliamua kubadilisha noti ya dola 100 mara mbili lakini watengenezaji wa fedha hizo bandia walifanikiwa kubadilisha fedha hizo na kufanana kama zile zinazochapishwa na serikali.

Zilipatikana nchini Denmark, Ufaransa, Austria, Ujerumani, Latvia, Urusi, Czech Republic , Ireland na Urusi.

Chanzo cha picha, IMAGE SOURCE,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wahalifu nchini Urusi walizitumia bila aibu

Kwa miaka kadhaa zilikuwa mwiba kwa shirika la ujasusi la Marekani FBI.

Hawakujua ni nani aliyekuwa akizichapisha . Ilichukua operesheni kali ya miaka minane ili kuanza kuwakamata wahusika.

Walifanikiwa kuwakamata washukiwa wa kwanza mjini California na New Jersy , baada ya wachunguzi kupata makasha ya fedha hizo kutoka katika meli kutoka kusini mashariki mwa bara Asia.

Wale waliokamatwa walikuwa na uhusiano na wahalifu wa kimataifa , lakini maafisa wa shirika la FBi walikuwa wakishuku kwamba mtandao huo ulikuwa mkubwa.

Fedha hizo hazikutengenezwa na wahalifu wa kawaida ama mtandao wa wahalifu , lakini zilitengenezwa na serikali ya Korea Kaskazini, mamlaka ya Marekani ilisema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Trump akiamkuana na rais Kim Jong un

Mara kwa mara fedha hizo zilipatikana katika mikono ya wanadiplomasia wa Korea Kaskazini , pengine kuongeza mapato ya taifa hilo , ambalo lilikuwa likikumbwa na matatizo ya njaa na kuanguka kwa mshirika wake mkuu Muungano wa Usovieti.

Hatahivyo, Korea Kaskazini inakana kuhusika katika kuchapisha fedha hizo.

''Korea Kaskazini imekana kuhusika katika usambazaji na uchapishaji wa sarafu bandia , lakini Ushahidi unaonesha wazi kwamba ni wao'', alisema Daniel Glazer naibu waziri wa masuala ya Uhalifu wa kifedha akizungumza na New York Times.

''Hakuna masuali yoyote juu ya kuhusishwa kwa Korea Kaskazini'', alisema.

Mamlaka nyengine zilitaja kughushi huko kama shambulizi baya l mfumo wa fedha wa Marekani.

Hatahivyo , kipaumbele cha FBI kilikuwa kusitisha usambazaji wa fedha hizo katika taifa la Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jumba la Playboy lilikuwa na jukumu muhimu katika kuangamiza mtandao huo wa uhalifu

Kuwasili kwa dola hizo bandia katika bandari zake kulitokana na kuwasili kimagendo kwa sigara na dawa za kulevya.

FBI ilitumia mbinu ya kuwavutia idadi kubwa ya wahalifu wanaohusishwa na njama hiyo: Harusi bandia na sherehe ya kutalakiana katika jumba la Playboy.

Mpango huo ulifanikiwa na watu 87 walikamatwa .Lakini idadi ndogo ya dola hizo bandia zinadaiwa kuendelea kusambaa hadi leo.

Jumba hilo la Playboy lilikuwa na jukumu muhimu la kusambaratisha matandao huo wa uhalifu.