Unywaji wa pombe una athari mbaya kwa ubongo, utafiti wabaini

Watafiti wanasema hata unywaji kiasi wa pombe unahusishwa na kuenea zaidi kwa athari kwa athari mbaya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Watafiti wanasema hata unywaji kiasi wa pombe unahusishwa na kuenea zaidi kwa athari kwa athari mbaya

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford wanasema hata unywaji kiasi wa pombe unahusishwa na kuenea zaidi kwa athari mbaya kwenye ubongo kuliko ilivyotambuliwa awali.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford wanasema hata unywaji kiasi wa pombe unahusishwa na kuenea zaidi kwa athari kwa athari mbaya kwenye ubongo kuliko ilivyotambuliwa awali.

Utafiti huo umebaini kwamba kiasi chochote cha unywaji wa pombe kinaweza kukuletea madhara kwenye ubongo wako

Utafi huo uliofanyika kwa watu 25,000 kwa kutumia hazina ya sampuli ya Ulaya unasema : "Hakuna kiasi salama cha pombe kwa ubongo kilichobainika.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiwango cha 'hatari ya chini ' cha miongozo ya unywaji wa pombe kinapaswa kuangaliwa upya

Unywaji wa kiasi wa Pombo unahusishwa zaidi na kusambaa kwa athari mbaya kwenye ubongo kuliko ilivyotambuliwa awali ."

Uliongeza kuwa: "Watu binafsi wanaokunywa pombe au wenye shinikizo la damu na unene wa kupindukia wanaweza kuathirika zaidi. Athari za kuathiriwa kwa ubongo kutokana na unywaji wa pombe huonekana kuwa kubwa zaidi athari za mabadiliko .

Kiwango cha 'hatari ya chini ' cha miongozo ya unywaji wa pombe kinapaswa kuangaliwa upya kwa kuzingatiwa athari zake kwa ubongo'' unasema utafiti huo

PICHA

Waandishi wa utafiti huu walisema kuwa utafiti wao ni wa kiuchunguzi, na waathiriwa hawawezi kubainika kutokana nao. Lakini utafiti huo umekubaliwa na 'waasisi wenza' au vigezo ambavyo vinaweza kuwa na matokeo ya athari mbaya, kama vile umri, afya na uzito wa mwili wa kupindukia.

Utafiti bado haujatathminiwa na watafiti wengine.

Utafiti huo uliwahusisha washiriki 25,378 kwa kutumia data kama vile umri, jinsia, elimu , ripoti binafsi ya kiwangio cha unywaji wa pombe, ukubwa wa ubongo na afya kwa kutumia scan za MRI, taarifa kuhusu hospitali na matibabu ya bila kulazwa , pamoja na vipimo vya kumbukumbu.

Washiriki 11,854 walikuwa ni wanawake, na asilimia 60 ya washiriki walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 50.

Utafiti ulibaini nini

Huku unywaji wa kawaida wa pombe ni jambo la kawaida na mara nyingi huonekana kama usiokuwa na athari kwa afya ya ubongo , utafiti huu ulibaini kuwa kila unywaji hupunguza uwezekano wa kutoathiriwa kwa ubongo . "Unywaji wa kawaida wa pombe unahusishwa na usambaaji zaidi wa athari mbaya kwa ubongo kuliko ilivyotambuliwa awali ," ulisema.

Maelezo ya picha,

Watafiti walibaini kuwa hapakuwa na kiwango "salama" cha unywaji wa pombe

Unywaji wa kiwango cha juu cha pombe kwa wiki ulihusishwa na athari mbaya zaidi karibu kote duniani ," ulisema utafiti . Pia ulibaini kuwa unywaji wa pombe ulichangia kwa kiasi kikubwa athari nyingine zilizosababishwa na mambo mengine, ikiwa ni pamoja na uvutaji wa sigara.

Haijalishi unakunywa aina gani ya pombe.

Kikundi cha watafiti pia kilichunguza aina za unywaji, aina nyingine za vinywaji na hali nyingine za kiafya zilizoleta mabadiliko katika athari za pombe kwa afya ya ubongo.

Walibaini kuwa hapakuwa na kiwango "salama" cha unywaji wa pombe -ikimaanisha kuwa unywaji au aina kiasi chochote cha pombe ni kibaya kuliko kutokunywa kabisa pombe.

Walibaini pia kuwa hakuna ushahidi kwamba aina ya kinywaji fulani -mfano mvinyo, spiriti au bia indiyo iliyoleta madhara kwa ubongo.

Hatahivyo, hali fulani alizonazo mtu kama vile, shinikizo la juu la damu, unene wa kupindukia wa mwili au unywaji wa pombe, vinaweza kuwaweka watu katika hatari ya juu, Watafiti waliongeza .

Wataalamu wa magonjwa ya ubongo wanasema wakati bado hatujapata dawa za tiba kwa magonjwa yanayoathiri ubongo kama dementia, kufahamu juu ya mambo yanayoweza kuzuia madhara ya ubongo ni muhimu kwa afya ya umma.