Terry Crews afunguka kuhusu jinsi uraibu wa ponografia ulivyokaribia kuharibu ndoa yake

Terry Crews

Chanzo cha picha, Terry Crews /Facebook

Ni taarifa iliyowashangaza wengi hasa kutokana na umaarufu wa mchezaji filamu maarufu wa Hollywood Terry Crews. Hata hivyo nyota huyu wa filamu amekuwa wazi kuhusu ni kwanini ameamua kueleza yaliyomsibu kwa umma: Lengo ni kuwasaidia watu wengine wanaopitia matatizo kama aliyokuwa nayo.

Bw Crews mwenye umri wa miaka 52 ambaye pia ni mchekeshaji maarufu wiki hii ameamua kufichua uraibu wake kwa ponografia ambao anasema nusura ukatize ndoa yake na mkewe wa miaka 30 Rebecca Crews, mwenye umri wa miaka 55.

Akizungumza kabla ya kutoa kitabu kipya kitakachotolewa kwa njia ya sauti alichokiita , Stronger Together, au( imara pamoja), ambacho Bw Crews alikiandika akishirikiana na mke wake.

Nyota huyo wa filamu pia alifunguka kuhusu tabia yake ya kutokuwa mwaminifu kwa mke wake.

Katika moja ya mahojiano aliyoyatoa siku za nyuma, Terry aliwahi kufichua kuwa uraibu wake wa ponografia uliendelea kwa miongo kadhaa. Hata baada ya kuoa na kupata watoto, aliweza kuendelea na tabia yake japo kwa siri.

Mchezaji filamu huyo anasema kuwa kwake nyota wa Hollywood kuliifanya hali hiyo hata kuwa mbaya zaidi. Alikiri kushawishiwa na watu wanaomzingira, katika mafanikio yake ya kibiashara na kikazi.

"Mafanikio ni sehemu nzuri sana ya kujificha. Nilikuwa na watu wengi sana walioniambia kuwa mimi ni mtu bora sana na ilikuwa ni tatizo. Na unajua nini?

Hollywood haikujali. Bado haijali iwapo utapoteza familia yako, inatokea kila siku ."

"Kwahiyo umaarufu ulifanya uraibu wake kuwa hata mbaya zaidi,"anasema Rebecca. " Na ni kweli kwamba mamlaka yale na mafanikio huchochea kile kinachoendelea ndani yako, na ndio maana nisingensaidia. Na ninashukuru na ninabahati kwamba alichukua uamuazi kufanyua hivyo."

Nyito huyo wa filamu Everybody Hates Chris alisema kuwa vitendo vyake vilikuwa vibaya sana kiasi kwamba mke wake alimwambia asirudi nyumbani.

Kwa kusikitishwa na athari za vitendo vyake, Terry alibadili maisha yake wakati rafiki yake mwema alipompatia ushauri mzuri wkuwahi kupatiwa maishani mwake.

Chanzo cha picha, Terry Crews/Facebook

Maelezo ya picha,

Terry Crews na mke wake, Rebecca wameandika kitabu kwa pamoja kuzungumzia matatizo waliyopitia

Alisema, "Terry, unahitaji kuwa bora kwa ajili yako mwenyewe."

Aliongeza kuwa, "Unajua, unafanya kazi kwa bidhii kwa ajili ya kupata fedha. Unafanya haya mambo kupata ngono. Lakini ili kujifanya kuwa bora kwa ajili yako, hilo lilikua ni jambo geni kwangu. Nilifikiria nikajiambia, hebu fikiria kidogo, kweli ninahitaji kuwa mtu bora kwa faida yangu mwenyewe ."

Baada ya hapo, Terry alilifanyia kazi jambo hilo.

Katika mahojiano, mwanamke mmoja alimuuliza mkewe Terry, Rebecca ndoa yao ilivyonusurika wakati wa kipindi kigumu walichopitia.

"Si mimi wa kuzungumzia mapambano yangu wakati niko ndani yake bado,' alifafanua Rebecca . Sitakutumia ujumbe wa Instagram huku nikiwa ndani ya mapambano yangu, lakini nitayazungumzia wakati nitakapoondoka kwenye mapambano haya na kuwa upande ule mwingine ."

Chanzo cha picha, Terry Crews/ Facebook

Maelezo ya picha,

Terry Crews na mke wake Rebecca wanakiri kuwa kupona kwake kumetokana na usaidizi wa kisaikolojia

Wanandoa hao wanasema njia ya kupona kwa Terry kwa uraibu wake wa ponografia imetokana na ushauri nasaha na tiba ya kisaikolojia, ambavyo alikiri kuwa ni mambo ambayo yalikuwa mwiko kuzungumziwa katika eneo alilokulia la Flint, Michigan.

"Nilifikiria nikasema, "huu ni ujinga, huyu sio mimi…na ghafla nikabaini kuwa nimerejea kuwa mimi ," alisema baada ya kukubali matatizo yake ambayo yalimfanya apewe tiba ya ushauri nasaha

Baada ya hapo, alikwenda katika safari (tour) ambako aliketi chini na watu kadhaa muhimu katika maisha yake chini wakiwemo watoto wake.

Chanzo cha picha, Terry crews/ Facebook

Maelezo ya picha,

Bw Crews anasemaaliamua aandike kitabu kwasababu anafahamu kuwa si yeye peke yake mwenye tatizo la uraibu wa ponografia

".Sababu iliyotufanya tuandike kitabu hiki ilikuwa ni ukweli kwamba ninafahamu kuwa siwezi kuwa peke yangu. Siwezi kuwa mwanaume mbaya peke yangu. Siwezi kuwa mimi tu ndiye mtu aliyepitia haya pekee ," alisema.

Terry aliongeza kuwa kuushirikisha umma hilo," mtazamo mmoja hautoshi juu ya kitu kama hiki, mitazmo miwili, hasa wa mume na mke wake. Mitazamo mitatu inafungua kweli kitu hiki kweli kweli, kwa mapana. "

Hii ndio sababu wawili hao waliandika kitabu pamoja.

Walimalizia kwa kufafanua kuwa kitabu kinaweza kuwa si cha kila mmoja, bali kwa ajili ya baadhi, inaweza tu kuwa hadithi inayofaa kusikia.