Mwili wa Mkuu wa majeshi wa Nigeria Ibrahim Attahiru aliyeuawa katika ajali ya ndege wazikwa

Ibrahim Attahiru

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jenerali Attahirualikuwa amechaguliwa kushikilia wadhifa huo mwezi Januari mwaka huu

Mwili wa Mkuu wa majeshi ya Nigeria Luteni Jenerali Ibrahim Attahiru, aliyefariki dunia katika ajali ya ndege iliyoanguka katika jimbo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo la Kaduna, umezikwa. Luteni Jenerali Ibrahim Attahiru walikuwa katika ziara kutoka Abuja alielekea Katuna.

Tukio hilo lilitokea wakati ndege aliyokuwa akisafiria ilipojaribu kutua katika hali mbaya ya hewa, jeshi limesema. Maafisa wengine pia wamefariki, pamoja na muhudumu wa ndege.

Rais Muhammadu Buhari amesema "amesikitishwa sana " na ajali hiyo.

Jenerali Attahiru, aliyekuwa na umri wa miaka 54, alichukua wadhifa huo tu mwezi Januari wa kuliongoza jeshi la Nigeria.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Miezi mitatu iliyopita ndege nyimgine ya jeshi la Nigeria ilianguka na kuwauwa watu 7 katika mji mkuu Abuja

Ilikuwa ni sehemu ya mpango wa serikali kuinua kiwango cha ufanisi wa jeshi katika kupambana na uasi wa zaidi ya muongo mmoja wa makundi ya jihadi.

Kikosi cha anga cha Nigeria kimesema kuwa tukio hilo lilitokea wakati ndege ilipokuwa ikitua kwenye Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kaduna.

Kwenye Twitter, rais alisema ajali hiyo ni "pigo kubwa.. wakati vikosi vyetu vimejiandaa kumaliza changamoto za kiusalama zinazoikabli nchi ".

Ajali hiyo ya Ijumaa inakuja miezi mitatubaada ya ndege ya kijeshi kuanguka katika mji mkuu Abuja , na kuwauwa watu saba waliokumwemo ndani.