BBC yakosolewa kwa mahojiano iliyoyafanya miaka 25 iliyopita

BBC imeomba "msamaha wa bila masharti " kwa jinsi ilivyothib itisha mahojiano na Diana

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

BBC imeomba "msamaha wa bila masharti " kwa jinsi ilivyothib itisha mahojiano na Diana

Serikali itaipatia BBC fursa ya kufanya mabadiliko baada ya ripoti inayohusu mahojiano na Bintimfalme Diana , BBC Newsnight imebaini.

BBC inakabiliwa na shinikizo kufuatia uchunguzi katika kesi, iliyobaini kuwa Martin Bashir alitumia udanganyifu katika kupata mahojiano maarufu na Binti mfalme mwaka 1995.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema Shirika hilo la habari la Uingereza linapaswa kuhakikisha kitu kama hiki hakitokei tena-huku baraza la mawaziri likipindekeza kuwa utawala wake unahitaji mageuzi. BBC inasisitiza kuwa imekwishafanya mabadiliko kwenye utawala wake tangu miaka ya 1990.

Kwa mujibu wa kipindi cha BBC cha News night, mawaziri wanataka kutekelezwa kwa pendekezo lililotolewa na Mwenyekiti wa zamani wa BBC Lord Grade la kuanzisha tume mpya , huru ya kuripoti kuhusu utawala wa sasa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson BBC inapaswa kuhakikisha kitu kama hiki hakitokei tena

Mahojiano ya Mwanamfalme Diana na mwandishi wa habari wa kipindi cha BBC cha Panorama, Bashir yalikuwa ni mara ya kwanza kwa Ufalme wa Uingereza kuzungumza wazi juu ya maisha ya familia ya ufalme.

Katika mahojiano haya Diana alisema kuwa hadurahishwa na ndoa yake na Mwanamfalme Charles, na awali alisema katika taarifa kwamba: "Tuko watatu katika ndoa hii."

Uchunguzi kuhusu mahojiano hayo, uliotangazwa siku ya Alhamisi, uliagizwa na BBC mwaka jana, baada ya Earl Spencer - kaka yake Diana- kuelezea hofu ya umma juu ya mbinu zilizotumiwa na BBC kupata mahojiano na Diana.

Ijumaa, Waziri Mkuu Johnson alisema kuwa anatumai BBC itachukua "kila hatua iwezekanayo kuhakikisha kitu kama hiki hakitokei tena ".

Wakati huo huo Meanwhile, Ofcom - shirika linalotetea vyombo cya habari amesema Diana alikuwa akizungumza na mwandishi wa BBC na hakuna za ziada zinazopaswa kuchukuliwa .

Chanzo cha picha, BBC/Reuters

Maelezo ya picha,

Bintimfalme Diana (kushoto) na mwandishi wa habari Martin Bashir (kulia)

Uchunguzi wa ndani wa BBC juu ya madai ya kile kilichotokea mwaka 1996 ''haukuwa wa ufanisi'', kulingana na uchunguzi.

Mwanamfalme William amesema: "mahojiano yalikuwa na sehemu kubwa katika kuharibika kwa ''uhusiano'' wa wazazi ," na kuongeza kuwa " baada iliwaumiza watu wasiohesabika ."

"Lakini kilicho nishangaza zaidi ni kwamba BBC ilikuwa imefanya uchunguzi ipasavyo wa malalamishi katika mwaka 1995, mama yangu angefaha,mu kwamba alikuwa amedanganywa," alisema.

Lord Dyson alibaini kuwa Bashir alikuwa amemdanganya kaka yake Earl Spencer kumfundisha dada yake Diana kwa kuonesha noti gushi za benki akidai kuwa watu fulani walikuwa wamelipwa kumlinda Bintimfalme huyo.

Mwanamfalme William amesema iliaminiwa kwamba mbinu ya ulaghai ya kupata mahijiano "ilikuwa na athari juu ya kile mama yangu alichosema" katika kumjibu Bashir.

Alisema kuwa kipindi cha Panorama "hakikufaa" na kisingelitangzwa baadaye.

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Mwanamfalme William (katikati) na Harry (kulia) walikuwa watoto wakati mahojiano ya BBC yalipotangazwa

Bashir alisema "kitu cha kijinga" ndicho alichokijfanya na ndicho anachojutia, lakini akasema hakikuwa na athari juu ya uamuazi wa Diana wa kuhojiwa.

BBC iliitisha uchunguzi huru mwaka jana, baada ya kaka yake Diana, Earl Spencer ktoa madai juu ya jinsi mahojiano yalivyofanyika.