Rais Samia Suluhu awateua mabalozi wapya 23 wa Tanzania

Miongoni mwa waliochaguliwakuwa mabalozi na Rais Samia ni pamoja na wanajeshi na wanawake

Chanzo cha picha, SAMIA SULUHU/TWITTER

Maelezo ya picha,

Miongoni mwa waliochaguliwakuwa mabalozi na Rais Samia ni pamoja na wanajeshi na wanawake

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mabalozi 23 wakiwemo wanajeshi na mlimbwende wa Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu.

Bi Samia amemteua pia Togolan Edrisss Mavura. Bw Mavura ni msaidizi wa rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Mei 22, 2021 na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza imewataja mabalozi hao wapya kuwa ni Luteni Jenerali Yakub Mohamed, Meja Jenerali Richard Makanzo, Pereira Ame Silima, Maulidah Hassan na Togolani Mavura.

Wengine ni Edwin Rutegaruka, Fredrick Kibuta, Noel Kaganda, Mindi Kasiga, Caroline Chipeta, Macocha Tembele, Agnes Kayola, Masoud Balozi, Ceasar Waitara, Swahiba Mndeme pamoja na Said Mshana.

Pia Rais Samia amewateua Alex Kallua, Mahmoud Kombo, James Bwana, Said Mussa, Elsie Kanza pamoja na Robert Kahendaguza.

Chanzo cha picha, hoycetemu/Instagram

Maelezo ya picha,

Miongoni ma walioteuliwa kuwa mabalozi ni mlimbwende wa Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu

Majina ya wanawake waliojitokeza katika orodha hii ya mabalozi wapya ni :

  • mlimbwende wa Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu, Mwandishi wa habari na Mjasiriamali
  • Bi Maulidah Bwanaheri Hassan, ambaye ni msaidizi wa rais Diplomasia , Ofisi ya Rais Ikulu
  • Bi Mindi H. Kasiga , ambaye ni Mkurugenzi masoko wa bodi ya Utalii Tanzania
  • Na Bi Caroline kitana Chipeta, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha sheria , Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  • BiElsie Sia Kanza,Mshauri wa Maalum wa rais kwenye jukwaa la Uchumi duniani
  • Bi Agnes Richard Kayola. ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya ushirikiano wa kikanda na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Unaweza pia kusoma:

"Uteuzi wa Mabalozi hawa umeanza leo Mei 22, 2021 na wataapishwa kwa tarehe zitakazotangazwa baadaye," imesema taarifa hiyo.

Uteuzi wa mabalozi wapya umefanyika baada ya kufanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa aliyoyafanya Jumamosi iliyopita.